Kwanini Biblia ilituficha kuhusu uzao wa majitu/Wanefili?

Pia soma torati 3 10;11 miji yote ya nchi tambarare, na Gileadi yote, na Bashani yote, mpaka Saleka na Edrei, nayo ni miji ya ufalme wa Ogu katika Bashani. 11 (Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho kingali kiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni dhiraa tisa, na upana wake dhiraa nane, kwa mfano wa mkono wa mtu).

Nahitimisha kukwambia hawa jamaa walikuwepo hata Goliath vitabu vingin vimemuandika ni mabaki ya hao wanefili
 
Sawa hitimisha
 
MARKO naye angeandika INJILI yake historia ya maisha ya Yesu kuanzia alipofikisha umri wa miaka 12 mpaka 29 kwamba (Yesu) alikuwa anaishi wapi,
Kwenye agano jpya huwa nahisi kuna uchakachuaji mkubwa sana wa maandiko .Kuna muda unasoma kisa fln mara ghafla bin vuu hicho kisa kinaisha chap bila hitimisho na kuibuka kwa habari nyingine tofauti kabisa.
Agano la kale ni kweli lina eleweka na ndio maana walokole huwa hawapendi kulitumia na kujifichia kwenye injiri maana injili haijafafanua wazi mambo kama ulivyosema, .......

Hatuwezi badilisha kitu mkuu mambo mengi tumeyakuta hivyo ni wewe na mimi kung'amua kipi cha kuondoka nacho. Mimi sio mjinga unambie kuwa kuna mambo mengi yesu alifanya ambayo yasiandikwa yote yakaisha huu ni UONGO WA KIJINGA SANA.K wanini Musa kaandika kisa chote cha wana wa israeli kwa mpangilio mzuri kabisa na hata alipokufa joshua akaendeleza alipoishia Musa kwa uzuri kabisa.

Ukumbe story ya wana wa israeli imechukua miaka 400 na zaidi na ya yesu hata miaka35 haifiki na haieleweki janja janja nyingi.Kulikuwa na ulazima gani wakuliacha gape la miaka kuanzia akiwa na miaka13-29 ? Siamini kama waandishi wote hawa hawakuandika bali wahuni walitoa na kufanya yao!!!
 
Apuuzwe anajichanganya sana. Huyo akiulizwa maswali magumu anakimbia kipindi
 
Achaneni na Biblia za kiswahili, someni za Kiingereza… lugha ya kiswahili ngumu haswa kwa nyie vijana wa dotcom

Plus waliotafsiri sijui walikua wanatumia misamiati ya kwenye kamusi gani maana sehemu pakuandikwa ndege utaona wameandika shoro.. sasa unabaki unajiuliza lengo lao haswa lilikua ni kutufundisha misamiati au neno la Mungu, yaan ni masumbuko!!
 
Kwa ufahamu wangu kuna history ya miaka maefu na maefu haijulikana kutokana na kutokuwepo na technology ya uandishi na utunzaji habari habari nyingi za kale zilikuwa zinatunzwa kwa masimulizi ya kizazi adi kizazi
Na kuna vizazi vilivyotoweka na kumbukumbu nyingi
Kitabu cha mwazo kinataja ni kitabu cha musa ,musa alikulia msri na kusoma chini ya taratibu za kimsri habari za musa mi miaka mia nne na thelasini baada ya israeli baba wa taifa kuhamia misri
Mtiliko wa biblia ulitumia uzao wa Israeli yani yakobo
Kwa hiyo habari zote nyingi zinatokama na jamiii ya yakobo na hii ni ya juzi kulinganisha na kule dunia ilipotoka
Huko nyuma kuna mambo mengi mno yasiyoelezeka ya binadamu wa kwanza na hali ya technology iliyokuwepo
Ikiwa mika ya 1961 hapa tanzania tunaona wanamama matiti i yalikuwa wazi yani hakukuwa na kuvaq nguo je miaka 5000 iliyopita dunia ilikuwa katika hali gani watu wali walikuwa wa namna gani walikuwa majitu hasa
Katika hali ya kisayasi inaonyeaha mazingira uchangia umbo la mwanadamu na sio tu binadamu walikuwa wakubwa hata wanyama pia
Je walitoka wapi? Jibu ni waliubwa katika mazigirq yao
Je walitokana na malaika kujamiana ma wanadamu nadhalia hii inatokana na adiko la mwanzo

Mwanzo 6:1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,
Mwanzo 6:2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.

Mwanzo 6:4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.
Katika mistari hii inaonyesha manefili kama ndio wanadamu na kizazi cha adamu kama wana wa Mungu kwa hiyo hapa sio malaika
kwani malaika hawakuubwa kuzaliana

Naweza kusema ni viumbe wa kale walioubwa ikiwa pamoja na wanyama wakubwa sana na dunia ile iliangamizwa na kufanya dunia mpya na watu wapya pya wa namna ya leo maana dunia ya kwanza iliangamizwa

2 Petro 3:5 Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;
2 Petro 3:6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.
Kwa hiyo wanefili wanotajwa kama mabaki ni mabaki ya watu waliokuwa hasa katokq mji wa kaanani ambapo wana wa Israeli kwa size walijiona kama mapazi

Hesabu 13:2 Tuma watu, ili waende wakaipeleleze nchi ya Kanaani, niwapayo wana wa Israeli; katika kabila ya baba zao mtamtuma mtu mmoja, kila mtu na awe mkuu kati yao. Send thou men, that they may search the land of Canaan, which I give unto the children of Israel: of every tribe of their fathers shall ye send a man, every one a ruler among them.
Hesabu 13:33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi
Ingawa kuna vitabu vingine kama cha enock ambacho kina Habari za kale zaidi kimefichwa na vingine vingi sana
Mambo ni mengi mda ni mchache sana kifupi nyuma yetu kulikuwa kulefu mno kuliko adamu adi leo
 
Sawa mkuu lakini tusaidie sasa hiyo ya kiingereza hao Giant wametokana na uzao wa nani?
 
Umegusia mambo ya msingi sana
 
Hao watu hawana mwili bali ni roho hivyo kuzaa na binadamu unahitaji kuwa na mwili. Hapo wamewezaje kuzaliana na binadamu ikiwa hawana miili?
Mkuu kwa uelewa wangu mdogo nafahamu ya kwamba mapepo/majini yanauwezo wa kujibadirisha na kuvaa umbo la binadamu yoyote.

Rejea kisa cha lutu hadi aliwapikia chakula wale malaika waliokuwa wanaenda kuiteketeza sodoma na gomora
 
ila we jamaa..... lakini bado sijakusoma hapo
 
2 Petro 2:4
Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;
Huyo Mungu wenu kipindi anawaumba hao malaika waliokosa hakujua kama watakuja kukosa asiwaumbe ikiwa huwa mnatuaminisha ya kuwa yeye anayajua yajayo kabla ya kuyafikia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…