Ninachohisi ni kuwa nani aliyeanza kuendelea kati ya mjapan na mchina. Zamani nchi na alikuwa akitawaliwa na mjapan.
Japan ilishaendelea sana, kuanza na vitu vidogo vya majumbani na hatimae kwenye machine kubwa ikiwamo magari.
Wachina wameanza kuingia miaka si mingi, na kwa hulka yao ya kuagiza vitu, Walianza kujiimarisha kwa bidhaa za ndani, za kielektroniki na umeme n.k. wakawa ni wasambazaji wakubwa si Afrika tu bali hata Marekani.
Magari wameanza kutengeneza, ila kwa soko la Afrika na aina ya uchumi wa watu binafsi, magari ya kijapan ndio tunayamudu kwa upatikanaji wake na vipuri pia. Pengine ni suala la wakati tu, baadae Wachina nao watapata soko la magari madogo Afrika.