Kwanini binadamu wasingekuwa wanataga mayai?

Kwasababu Binadamu ni Mamalia. Ukitaka Atage ni sawa na Tembo nae Atage ushawaza Yai la Tembo litakuwaje na ataliatamiaje kulipa Joto mpaka litotoe?

Pia kumbuka, viumbe wanaotaga hawatagi Yai 1 ni Mayai. Sasa uwe unafikiria cha kuandika humu ndugu.
Hahaha!!haya ni majibu mujaraabu kabsaa
 
Siyo mpaka aatamie. Mamba haatamii. Tungekuwa tunataga ile kazi ya kuijaza dunia ingeshakamilika. Ila najiuliza iwapo kuna social animals ambao wanataga, wapo?
Hata ya mamba yanatamiwa sidhani kama yatakaa sehemu ya wazi halafu apate vifaranga, anafukia shimoni ndiko kutamia kwenyewe.
 
hivi dinosaurs wanazaa au wanataga?.
 
Yeeeh inaathiri,, release ya oxytocin hormone during pregnancy ni muhimu for any social bonding,,

Sio mtazamo hiyo ni explanation ya kisayansi
Bila shaka mayai ya kware ukiyachanganya na mayai ya kuku yatahatamiwa na kutotolewa,je kati ya vifaranga wa kware na kuku kutakuwa na social bond?
 
Mkuu mwisho wa yote hayo mayai yangekaangiwa na chipsi halafu ingeleta hekaheka
 
Kinacho tupambanua wanaadamu ni akili tulizopewa, sasa ajabu ni pale mwanaadamu anaposhindwa kuona umbile bora alilopewa na namna bora ya namna anavyopatika.

Na kuanza kuona ni bora angekuwa anapatikana kama wanavyopatikana ndege!! Unamkufuru muumba wako.

Kama hoja ni kuwa kwa kutaga basi mama hatopata taabu kama anazozipata anapo beba mimba na kuzaa basi hujafikiria mara mbili, maana hoja yako ni ya kijinga.
 
Yangekuwa makubwa sana, kuna mamtu yangekuwa yanachemsha au kuyakaanga kunywea chai
 
Kwanini binadamu hawatagi mayai? Zipi faida za kuzaa dhidi ya kutaga?
 
Nimejikuta nacheka...huyu naye ukute familia inamtegemea.
 
Mutation hizo za kuweza kuzaa na sio kutaga mayai zilitoka miaka zaidi ya milioni 100 iliyopita
 
Kwa viumbe wote wanaotaga, huwa yai linapotagwa halikui nje ya mwili wa kiumbe husika, Bali linakulia ndani katika size maalumu Kisha linakuja kudevelop nje baada ya kutagwa na kutoa kifaranga, na ukubwa wa kifaranga unategemea na ukubwa wa yai.

Sasa tukija kwa mwanaadamu yaani atage yai ambalo ndani yake atoke kichanga kwa ukubwa huu tunaoufahamu, huoni hiyo kazi ngumu zaidi ya hiyo ya kuzaa?

Maana kiungo kikubwa kwa kichanga huwa ni kichwa sasa imagine mwili wote wa kichanga uwe ndani ya yai halafu alitage!!!

Labda utasema mayai yawe madogo, maana yake ukubwa wake usizidi ukubwa wa kichwa cha kichanga anapozaliwa(maana ndio upana ambao uke anaweza kitanuka), sasa hivyo vichanga vitakuwa na ukubwa gani?

Hukufikiria
 
Hapo hakuna kitu rahisi ndg yangu..
Umewahi kumuona kuku anavyohangaika akitaka kutaga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…