Kwanini binadamu yeyote akikata roho (akifa) tu ni lazima atoe haja kubwa hata kama ni kiduchu?

Kwanini binadamu yeyote akikata roho (akifa) tu ni lazima atoe haja kubwa hata kama ni kiduchu?

Katika uislamu tunafundishwa kuwa kuna maumivu mtu anapata wakati roho inatoka. na haya tunapata wote iwe kwa mtu mwema au mtu mwenye dhambi. Na hayo maumivu huwa yanazidi au kupungua kutokana na wingi wa madhambi aliyo nayo mtu.

Na kwa mujibu wa Mtume Muhammad S.A.W maumivu ya kutoka roho mfano wake ni kama mnyama kuchunwa ngozi akiwa hai yani yale maumivu yake anayopata akichwa ngozi ndio sawa na maumivu ya kutoka roho na ikiwa anayetolewa roho ni mtu muovu maumivu ni zaidi ya hayo.

Wakati wa kufa ukifika huwa wanakuja Malaika kutoa roho yako na kuondoka nayo kuirudisha kwa Muumba wako, na wewe unaye kufa huwa unawaona na unaongea nao hao Malaika, na watu wengine wote waliokuzunguka hawaoni wala hawasikii. utayajua haya tu pale siku yako ya kufa itakapofika.
 
QURAN 56: 83-

83. Yawaje basi roho itakapo fika kwenye koo,


84. Na nyinyi wakati huo mnatazama (mgonjwa wenu)!


85. Na Sisi tuko karibu naye zaidi kuliko nyinyi; lakini nyinyi hamuoni.


86. Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka Yangu,


87. Kwanini hamuirudishi hiyo roho yake, ikiwa nyinyi mnasema kweli (kwamba hakuna Mungu)?


88. Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa,(wenye matendo mema mengi)



89. Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema.



90. Na akiwa katika watu wa upande wa kulia, (watu wema )



91. Basi ni amani kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia.


92. Na ama akiwa katika walio kanusha; wapotovu,



93. Basi karamu yake ni maji yanayo chemka,



94. Na kutiwa Motoni.



95. Hakika hii ni kweli yenye yakini.



96. Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu".


Tusome vitabu vyetu vya dini vinaeleza vizuri safari ya mwanadamu kutoka hapa duniani mpaka atakapokuwa anakata roho na atakapo fufuliwa na kulipwa kwa aliyoyatenda. Haya ni kweli na usisubiri uyafahamu wakati wako wa kufa ukifika, it will be too late!
 
Nangoja kwa hamu sana kusoma maoni yenu ya kitaalamu enyi wajuvi wa JamiiForums, kwani nimedokezwa tendo la mwanadamu kujisaidia haja kubwa Wazaramo wanasema kuukweka) pale tu akikata roho ni la kisayansi zaidi. Hivyo nitafurahi nikielimishwa juu ya hili.
ile ni vita kama vita zingine unasimama katikati ya uzima na mauti hivyo kishindo chake lazima zi triger homones za mwili hasa kwenye brain hivyo impact yake lazima kinyesi kitoke
 
Siyo kweli, labda kwa nadra sana.

Niliwahi uguza na kufiwa na watu watatu ila hicho kitu hakikuwepo.

Mfano hosp kubwa mtu akifariki wanamvua nguo zote ndo wanambeba kwenda mortuary, sikuwahi ona.

Mtani wangu njoo saidia huku Mshana Jr
 
Ukweli ni kwamba mtu akifa, viungo vya nyuma vinalegea, hivyo inategemea alikua na hali gani muda wa kufa.
kuna mgonjwa anakula kwa dripu. huyu akifa hawezi kujisaidia.
kuna mgonjwa kula ni shida , au ni kidogo , huyu nae akifa kama alijisaidia kabla, haja haiwezi kutoka kwa kuwa tumbo halina kitu. kwa hiyo inategemea
 
Umekurupuka kwa kifupi Wala hakuna haja ya kujitetea we jua si kweli
 
[emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom