Last_Joker
Senior Member
- Nov 23, 2018
- 174
- 261
- Thread starter
- #21
Ni bora uende ukapige msuli mwenyewe boss. Me ntakusaidia kukuongoza wapi pakupata hiyo elimu. Nenda binance wana nondo kibaoTuoeni basi maujuzi hapa hapa JF wajuzi au tuka gogo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni bora uende ukapige msuli mwenyewe boss. Me ntakusaidia kukuongoza wapi pakupata hiyo elimu. Nenda binance wana nondo kibaoTuoeni basi maujuzi hapa hapa JF wajuzi au tuka gogo
bora umesema ukweli kuwa ulijaribu na sio kufanya kwa uhakika, suala la mtaji si lazima uwe na mamilioni. Muhimu uwe na elimu kwanza sahihiNilishawahi jaribu kuyafuatilia nikaona haya mambo yapo , ila yanahitaji mitaji mikubwa ni uwekezaji tu ila kwa mtu wakawaida ni kama kubashiri tu .
Elimu niliipata mkuu.bora umesema ukweli kuwa ulijaribu na sio kufanya kwa uhakika, suala la mtaji si lazima uwe na mamilioni. Muhimu uwe na elimu kwanza sahihi
kama hunna elimu na huku lazima utaona kupoteza muda ila ukiwa na elimu hupotezi muda. Na kingine fanya unachokipenda usije ukafanya jambo sababu ya kufata mkumbo. Kama online hupawezi kauze chapati.mimi nimeshauza chapati na mama na nimeshashinda na laptop., asikwambie mtu kuuza chapati mbona easy tu izi ela za mitandaoni mpaka kuzipata aisee energy yake sio ndogo. Ela zipo ila sio rahisi ata kidogo umesema kweli vijana wengi ata mi nashauri wauze tu chapati uku watapoteza muda tu
Kwa muda gani ulisoma mkuuElimu niliipata mkuu.
Mwaka mmoja na nusu huku nikiwa nafanyaKwa muda gani ulisoma mkuu
Naona mnataka kuokota wagunyaSikiliza, kuna maneno ambayo yamekuwa yakizunguka sana kwenye mitandao siku hizi – blockchain, crypto, Bitcoin. Na mara nyingi, watu wanavyosikia haya mambo, wanahisi ni kwa ajili ya matajiri au wataalam wa teknolojia tu. Lakini ukweli ni kwamba, blockchain siyo tu kwa wenye pesa au magwiji wa teknolojia – ni kwa ajili ya kila mtu, na inaweza kubadilisha maisha yetu kwa namna ambayo hatujawahi kufikiria.
Sasa, blockchain ni nini hasa? Fikiria kama daftari kubwa, la umma, ambalo linarekodi taarifa zote za miamala inayotokea, na linaonekana na kila mtu. Lakini tofauti na mabenki au serikali ambazo zinadhibiti taarifa, blockchain haidhibitiwi na mtu mmoja au taasisi moja. Kila mtu anaweza kuona na kushiriki kwenye miamala hiyo, lakini hakuna anayeweza kubadilisha au kuharibu taarifa hizo bila makubaliano ya watu wengine. Hii inamaanisha uwazi wa hali ya juu, usalama zaidi, na udhibiti zaidi kwa watu binafsi. Hapo sasa!
Kwa sasa, wengi wanajua blockchain kwa kupitia pesa za kidijitali kama Bitcoin, Ethereum, na zinginezo, lakini blockchain ni zaidi ya sarafu hizi za kidijitali. Ina uwezo wa kubadilisha jinsi tunavyohifadhi na kusimamia taarifa zetu binafsi, mikataba yetu, hata namna tunavyopiga kura. Hii teknolojia inaweza kupunguza udanganyifu na kuongeza uwazi kwenye karibu kila sekta, kuanzia afya, elimu, hadi biashara.
Hivi unajua kuwa blockchain inaweza kutumika hata kulinda haki za wasanii? Kwa mfano, kama wewe ni msanii wa muziki au mchoraji, unaweza kutumia blockchain kusajili kazi zako na kuhakikisha kwamba kila mtu anayenunua au kutumia kazi zako anafanya hivyo kihalali, na wewe unalipwa haki yako moja kwa moja. Sio kwamba wasanii hawahitaji tena kupigana na wizi wa kazi zao au mawakala wasioaminika – blockchain inawaletea uwazi na usalama.
Pia, kwenye biashara, blockchain inaweza kuondoa madalali na kuwawezesha watu kufanya biashara moja kwa moja. Hebu fikiria kununua nyumba bila kupitia kwa mawakala, au kununua bidhaa kutoka kwa muuzaji bila kupitia kwa kampuni za kati. Blockchain ina uwezo wa kufanya biashara iwe ya moja kwa moja, ya haraka, na isiyo na gharama za ziada ambazo zinakuja na madalali au mawakala.
Hata kama unafikiri blockchain ni teknolojia ngumu, inakuja na fursa nyingi ambazo unaweza kuzitumia hata kama huna ujuzi mkubwa wa teknolojia. Hivi sasa, kuna mipango ya fedha na miradi mingi inayotumia blockchain, na unaweza kujihusisha kwa njia rahisi tu, kama vile kuwekeza kwenye sarafu za kidijitali au hata kushiriki kwenye miradi ya blockchain ambayo inaendeshwa na watu wa kawaida kama wewe na mimi.
Kwa hiyo, usikubali neno blockchain likutishe au likufanye uamini kwamba ni kwa ajili ya matajiri tu au wataalam wa IT. Hii ni teknolojia yenye uwezo wa kuleta mapinduzi kwa kila mtu. Ni sawa kabisa kama ulivyoona intaneti ikibadilisha maisha yetu miaka ya nyuma, blockchain inaweza kuwa na athari kubwa zaidi ya hiyo.
Sasa, unachohitaji ni kuanza kuchunguza zaidi, kujifunza na kujiingiza kwenye ulimwengu huu mpya wa blockchain. Maana ni dhahiri, teknolojia hii haikuja kwa ajali – imekuja kutupa fursa mpya za kufanya mambo kwa njia bora zaidi. Wewe uko tayari kuchukua nafasi yako?
Hakuna anaetaka kumuokota mtu, ukiona jambo limekupendeza we lichunguze, lisome kisha utajua kama linakufaa ama laNaona mnataka kuokota wagunya
Kama kawa
Wew ni mpumbavu.. TuFanyeni kazi madogo .uzeni hata chapati acheni kushinda na laptop hakuna hela rahisi
Wacheze hata ngomaFanyeni kazi madogo .uzeni hata chapati acheni kushinda na laptop hakuna hela rahisi
Aisee ww jamaa hamna kitu kbs kichwani, hii ni technology ambayo niya wkt wasasa km vile unavyo sikia Software na hz apps km unayo tumia sasahv hapo ktk simu yako, inakuunga na banks na namengineyo mangi tu,km miamala ya simu inavyo fanyika kwa wepesi .... yaani mpaka uelewe 😅😅😅Hyo Blockchain sio ya matajiri.ni ya mafala tu.matajiri hawana muda WA kipuuzi na utapeli
Kbs na atupishe, mtu huwez ropoka kwa kitu ambacho ndio kina ongoza dunia sasahv....jamaa ni mjinga kbs, wenzetu kupiga kura huu mfumo wa #Blockchain ndio unatumika sasahv, na mengine mangikama hunna elimu na huku lazima utaona kupoteza muda ila ukiwa na elimu hupotezi muda. Na kingine fanya unachokipenda usije ukafanya jambo sababu ya kufata mkumbo. Kama online hupawezi kauze chapati.
Tofauti yake na ile forex ya ontario iliyoliza watu humu ni niniSikiliza, kuna maneno ambayo yamekuwa yakizunguka sana kwenye mitandao siku hizi – blockchain, crypto, Bitcoin. Na mara nyingi, watu wanavyosikia haya mambo, wanahisi ni kwa ajili ya matajiri au wataalam wa teknolojia tu. Lakini ukweli ni kwamba, blockchain siyo tu kwa wenye pesa au magwiji wa teknolojia – ni kwa ajili ya kila mtu, na inaweza kubadilisha maisha yetu kwa namna ambayo hatujawahi kufikiria.
Sasa, blockchain ni nini hasa? Fikiria kama daftari kubwa, la umma, ambalo linarekodi taarifa zote za miamala inayotokea, na linaonekana na kila mtu. Lakini tofauti na mabenki au serikali ambazo zinadhibiti taarifa, blockchain haidhibitiwi na mtu mmoja au taasisi moja. Kila mtu anaweza kuona na kushiriki kwenye miamala hiyo, lakini hakuna anayeweza kubadilisha au kuharibu taarifa hizo bila makubaliano ya watu wengine. Hii inamaanisha uwazi wa hali ya juu, usalama zaidi, na udhibiti zaidi kwa watu binafsi. Hapo sasa!
Kwa sasa, wengi wanajua blockchain kwa kupitia pesa za kidijitali kama Bitcoin, Ethereum, na zinginezo, lakini blockchain ni zaidi ya sarafu hizi za kidijitali. Ina uwezo wa kubadilisha jinsi tunavyohifadhi na kusimamia taarifa zetu binafsi, mikataba yetu, hata namna tunavyopiga kura. Hii teknolojia inaweza kupunguza udanganyifu na kuongeza uwazi kwenye karibu kila sekta, kuanzia afya, elimu, hadi biashara.
Hivi unajua kuwa blockchain inaweza kutumika hata kulinda haki za wasanii? Kwa mfano, kama wewe ni msanii wa muziki au mchoraji, unaweza kutumia blockchain kusajili kazi zako na kuhakikisha kwamba kila mtu anayenunua au kutumia kazi zako anafanya hivyo kihalali, na wewe unalipwa haki yako moja kwa moja. Sio kwamba wasanii hawahitaji tena kupigana na wizi wa kazi zao au mawakala wasioaminika – blockchain inawaletea uwazi na usalama.
Pia, kwenye biashara, blockchain inaweza kuondoa madalali na kuwawezesha watu kufanya biashara moja kwa moja. Hebu fikiria kununua nyumba bila kupitia kwa mawakala, au kununua bidhaa kutoka kwa muuzaji bila kupitia kwa kampuni za kati. Blockchain ina uwezo wa kufanya biashara iwe ya moja kwa moja, ya haraka, na isiyo na gharama za ziada ambazo zinakuja na madalali au mawakala.
Hata kama unafikiri blockchain ni teknolojia ngumu, inakuja na fursa nyingi ambazo unaweza kuzitumia hata kama huna ujuzi mkubwa wa teknolojia. Hivi sasa, kuna mipango ya fedha na miradi mingi inayotumia blockchain, na unaweza kujihusisha kwa njia rahisi tu, kama vile kuwekeza kwenye sarafu za kidijitali au hata kushiriki kwenye miradi ya blockchain ambayo inaendeshwa na watu wa kawaida kama wewe na mimi.
Kwa hiyo, usikubali neno blockchain likutishe au likufanye uamini kwamba ni kwa ajili ya matajiri tu au wataalam wa IT. Hii ni teknolojia yenye uwezo wa kuleta mapinduzi kwa kila mtu. Ni sawa kabisa kama ulivyoona intaneti ikibadilisha maisha yetu miaka ya nyuma, blockchain inaweza kuwa na athari kubwa zaidi ya hiyo.
Sasa, unachohitaji ni kuanza kuchunguza zaidi, kujifunza na kujiingiza kwenye ulimwengu huu mpya wa blockchain. Maana ni dhahiri, teknolojia hii haikuja kwa ajali – imekuja kutupa fursa mpya za kufanya mambo kwa njia bora zaidi. Wewe uko tayari kuchukua nafasi yako?
Baadae wanaanza kuona wivu vijana wakifanikiwaAisee ww jamaa hamna kitu kbs kichwani, hii ni technology ambayo niya wkt wasasa km vile unavyo sikia Software na hz apps km unayo tumia sasahv hapo ktk simu yako, inakuunga na banks na namengineyo mangi tu,km miamala ya simu inavyo fanyika kwa wepesi .... yaani mpaka uelewe 😅😅😅
watanzania wengi biashara ni zero wako fixed dunia inaenda kasii kama unapenda kuendesha baiskeli miaka yote wenzako wanapanda ndege daily..Tofauti yake na ile forex ya ontario iliyoliza watu humu ni nini
Hiyo uliyosema siifaham ila tofauti ya mfumo huu humtegemei mtu ila ni uwezo wako wa maamuzi, ni kama soko la hisa. Uwe na elimu sahihi na mtaji wako kisha ujipambanie. Hii sio pyramid scheme kwamba huku na huku elfu 90 sijui ukileta mtu unapata kamisheniTofauti yake na ile forex ya ontario iliyoliza watu humu ni nini
kiukweli wengi wetu hatupendi kusoma na tunataka slope kwenye mambo yetu, ndio maana tunapigwa. Mtu akiskia kuna pesa basi anaingia kichwa kichwawatanzania wengi biashara ni zero wako fixed dunia inaenda kasii kama unapenda kuendesha baiskeli miaka yote wenzako wanapanda ndege daily..
Unapataje pesa sasaHiyo uliyosema siifaham ila tofauti ya mfumo huu humtegemei mtu ila ni uwezo wako wa maamuzi, ni kama soko la hisa. Uwe na elimu sahihi na mtaji wako kisha ujipambanie. Hii sio pyramid scheme kwamba huku na huku elfu 90 sijui ukileta mtu unapata kamisheni
Njia zipo nyingi. Unaweza ukawa trader, unaweza ukawa wakala wa kuuza na kununua coins, unaweza ukawa unanunua na ku-hold coins kwa muda mrefu, unaweza ukawa una hunt Airdrops. Tafuta uisome kwanza kisha utajua wapi kunakufaa na vipi utapiga mtonyoUnapataje pesa sasa
Uwekezaji mtaji kuanzia shiling ngapiNjia zipo nyingi. Unaweza ukawa trader, unaweza ukawa wakala wa kuuza na kununua coins, unaweza ukawa unanunua na ku-hold coins kwa muda mrefu, unaweza ukawa una hunt Airdrops. Tafuta uisome kwanza kisha utajua wapi kunakufaa na vipi utapiga mtonyo