Kwanini Bosi wa TAKUKURU anavaa sare za Jeshi? Nini taswira ya Utawala wa Kiraia?

Nilichoka aliposema rushwa kwenye ndini ya uchaguzi CCM inawaachia wenyewe kwa kuwa wana taratibu zao za kushughulikia, kizunguzungu hadi leo nikiona kombati zile!
 
Kikwete na Kinana walistaafu JWTZ mwaka 1992
 
Sasa mbona pale lugalo wanauza mtofali wakati wameanbiwa shughuli za uzalishaji ni JKT JWTZ mbona hata gambe wanauza? Najua ni hatari kushirikisha Mwanajeshi katika shughuli za biashara kwani nidhamu ya jeshi itapungua kwani ataona nibora kufanya biashara.
 
Hivi vyote ni vyombo vya ulinzi na usalama kwa hiyo kuva au kutovaa ni ihali yake!Hakuna kosa angekuwa yupo kwenye tume ya uchaguzi au tume ya haki za binadamu asingevaa sale.
 
Kwani TAKUKURU ni chama cha siasa?hapo kuna SMG zakutosha usijidanganye kuwa kile ni chombo kama wizara ya kilimo pale ni chombo cha ulinzi na usalama hivyo utii ni wakiasikari.
 
usisahau hao JKT ni JWTZ pia, yaani ni hao hao tu
 
Kitu huelewi ni kwambae hawa wanajeshi licha ya kuwa askari wanataaluma zao kama raia wengine

Kuna wanasheria,madaktari,wahasibu.nk .So kuteuliwa kwenda idara za serikali kutumikia taaluma zao si vibaya . Kuna wakati madaktari askari wanapelekwa hospital za kawaida kutibu.
 
Kikwete, pamoja na kuwa mjeshi, lakini alijitahidi sana kutoonekana hivyo....kwa matendo, mavazi na hata nyaraka.

Namkumbuka bado mwendazake alivyokuwa "anashobokea kombati.....wakati mwingine miguuni ana kandambili! Nchi hii haiiishi vituko.
 
Tuna amini jeshi halishindwi na kitu chochote mpaka hapooo! Raiya wameshindwa kwenye hiyo position mpaka hapoo! Unachotakiwa ni kusima kwa utulivu uwone mambo yanavyokwenda kiutalam, hizo bakiti zisikusumbue saaana ukakosa amani
 
Hili halina muda... Kuna mabadiliko mengi makubwa yanakuja... Jeshi litatengwa na shughuli na siasa na utawala libaki na dhima yake ya ulinzi na usalama
Halotel aka viatel kampuni ya Jeshi la Vietnam.....
Au unabisha mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…