MWANAHARAMU
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 4,041
- 10,699
Najibu ila kama nitakuwa nimekwenda op mtanikosoa.Hivi kuna tofauti gani kati ya askari na mwanajeshi? Huwa nasikia wengine wanaita askari wa jeshi la... kwa nini hawasemi mwanajeshi au polisi tu?!
Askari ni mtu yeyote aliyepitia Mafunzo rasmi ya Kijeshi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivyo kama mtu alijifundisha vichochoroni hatambuliki hata akiwa na Mafunzo ya special force, atapewa majina mengine Kama itaonekana inafaa.
Mwanajeshi ni member wa jeshi fulani linalotambulika kisheria. Hapa tuweke mazoea na desturi pembeni.
Hivyo kwa Tanzania Police wote ni wanajeshi, Magereza wote ni Wanajeshi, Wahifadhi ni Wanajeshi [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Turudi kwenye mazoea yetu Watanganyika
Enzi za ukoloni wananchi waliona shida kuwaita wote wanajeshi wakatafuta namna ya kuwatofautisha hivyo kuwaita walio askari kwenye jeshi la mkoloni kuwa wanajeshi na walio polisi askari.
Ila uhalisia wote hawa ni askari na pia ni Wanajeshi.
Sasa jamii imezoea kuwaita askari wa jeshi la uhifadhi kuwa Wahifadhi kutokana na nature ya shughuli zao.
Ila hawa ni askari Magereza na polisi ila jamii hiyo hiyo inapendelea kuwaita walio Immigration maafisa uhamiaji.