Kwanini Chato iwe Mkoa kutoka kwenye Mkoa mchanga wa Geita ulioundwa 2012?

Daaaah! Nchii hii inasikitisha Sana ndio maana huwa nasema kushabikia "kijani" ndio kipimo Cha mental disorder
 
Kakonko watakuwa wamesaidiwa sana, maana kutoka Kakonko mpaka Kigoma ni karibu kilometa 400. Aidha serikali haigawi mikoa kwa kigezo cha ukabila, hiyo ni hoja nyepesi sana. Katika karne hii bado unawaza ukabila ? Pole sana.
 
Kwani wakati wanaunda mkoa wa Rukwa mwaka 1974 wakati wa Rais Nyerere walifanyaje ? Mkoa huo ulianza na Wilaya mbili Sumbawanga kutoka mkoa wa Mbeya na Mpanda kutoka mkoa wa Tabora, kinachofanyika katika hoja hii ya Mkoa tarajiwa wa Chato siyo kitu kigeni au ulikuwa hujazaliwa ?
Pwani ni kubwa sana hiyo ndio iliktakiwa kugawanywa. Wanaenda kuunda mkoa ambao hata wilaya hazijitoshelezi wanaziomba mikoa mingine. Huu ni ujinga n upuuzi.

Sent from my PBAT00 using JamiiForums mobile app
 
Kuna watu wanacomment hata geographia ya maeneo hawajui. Kakonko ni mbali sana kwenda Kigoma bora hata Chato
Kwani wenyewe kakonko wamesema hawataki kutenganishwa na ndugu zao?? Au ni mawazo yako??? Mbona kuna uzi humu wakiomba mkoa wa nyakanazi kwa sababu kwenda Kigoma mjini ni mbali sana??
 
Mikoa mingi mtakufa na njaa kwa utawala huo wa majimbo mnaoutaka maana hata Rasilimali hakuna.
Chato iliandaliwa iwe Mkoa na ndio maana wakaweka kila kitu ili iwe na hadhi ya Mkoa
Ila kama tutaendelea hivi tutajikuta kila Rais ataamua anavyotaka

Bora majimbo machache na kila jimbo kujitegemea kwa uzalishaji wake na maendeleo pia
 
Mmmhmm kwani ulikua na upungufu
 
Hiyo ni hoja nyepesi sana
 
Sasa kwanini tusianze kuugawa Dar kwanza kama sababu ni idadi ya watu.
 
Kiukweli chato na hiyo geita hazina hadhi kuwa kipaumbele cha kuwa mkoa kwa sasa maana mikoa mikubwa zaidi ipo mingi tu; ni kutuongezea gharama tu kama taifa
 
Aisee...

Inaonesha ulimchukia sana na sasa unachukia hadi kivuli na pengine kaburi lake...

Calm down ndugu...

He's no more. He's not coming back again. Your nightmare is gone forever....

So why don't you enjoy your life now?. Don't let the deceased to ruin your life...
 
Angekuwepo nadhan Kila mmoja angeunga mkono juhudi...na watu wangesema inastaili..
If you know how quick people forget,.you could not live by impressing others...
 
Sasa kwanini tusianze kuugawa Dar kwanza kama sababu ni idadi ya watu.
Ndo maana nasema hawaangalii factor moja, mkoa kama Kagera una watu wengi ila bado ni mkubwa pamoja jiografia yake imekaa vibaya. Sasa ukisema utenge Dar au Kilimanjaro haiwezekani huko
 
Kakonko watakuwa wamesaidiwa sana, maana kutoka Kakonko mpaka Kigoma ni karibu kilometa 400. Aidha serikali haigawi mikoa kwa kigezo cha ukabila, hiyo ni hoja nyepesi sana. Katika karne hii bado unawaza ukabila ? Pole sana.
Kutoka Kakonko(wilaya mpya) hadi Kigoma ni kilomita 284.2 wakati kutoka Kibondo(wilaya kongwe) kwenda Kigoma ni kilomita 238.0 Kuna tofauti ya kilomita 46.2 kati ya Kakonko na Kibondo zikihudumiwa kutoka mkoa wa kigoma. Suruhisho ili kuunda mkoa wa Chato ni kumega huko huko Geita bila kuingilia mkoa wa Kigoma. Kama Kakonko na Kibondo wakiamua kwenye RCC Yao, suruhisho ni kuunganisha Ngara na nyakanazi kufanya mkoa mpya wa Nyakanazi au Kibondo.....Siyo hii habari ya mkoa wa Chato.
 
Ungebalance hoja yako kwa kuweka na umbali wa kakonko hadi chato ili tuone ni wapi kunafikika haraka bila kusahau na miundombinu rafiki ya kufika
 
Ungebalance hoja yako kwa kuweka na umbali wa kakonko hadi chato ili tuone ni wapi kunafikika haraka bila kusahau na miundombinu rafiki ya kufika
Mbona umeng'ang'ania Chato wakati Nyakanazi ndio suruhisho la hao watu wa Kakonko jomba?.
 
Mbona umeng'ang'ania Chato wakati Nyakanazi ndio suruhisho la hao watu wa Kakonko jomba?.
Binafsi na mimi sipendezwi na makao ya mkoa kuwa chato, nyakanazi ndo pazuri kabisa lakini kama imetokea pakawa chato waache kakonko wajumuishwe maana ni afadhali kuliko kwenda Kigoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…