Kwanini Chato iwe Mkoa kutoka kwenye Mkoa mchanga wa Geita ulioundwa 2012?

Mkipata mtawala mwenye laana, laana hutanda nchi nzima. Angalia sasa, wajumbe wa RCC wote, akili zimekimbilia kwenye nyayo.
 
Kwa nafsi yangu naamini kabisa marehemu Magufuli hakufaa kuwa kiongozi wa nchi. Alikuwa mbinafsi mkubwa, hana busara wala hekima.

Ameondoka lakini madhara yake bado yametamalaki. Tuzidi kumwomba Mungu, Mama Samia abakiwe na hekima, asiwe kama Pilato, ambaye alijua kuwa Yesu hakuwa na kosa lakini akakubali ahukumiwe kifo kwa sababu ya kuogopa sauti za waovu, ziluzodai, asulibiwe.

RCC ya Geita imeingiwa na shetani. Raos Samia ajitenge na shetani, ajishilamanishe na Mungu wa kweli.
 
Mkoa hautengwi kwa kutazama ukubwa ma ardhi. Ingekua ukubwa wa ardhi Dar Es Salaam ingejua wilaya tu.
Argument imekosa weledi. Unavifahamu vigezo vya kuunda mkoa? Kama hujui, ukubwa wa eneo ni sababu mojawapo, japo siyo pekee. Vigezo vingine ni pamoja na uwingi wa watu, umbali kutoka kwenye huduma za kimkoa na ukubwa wa uchumi. Chato haikidhi kigezo hata kimoja.

Wametengeneza vigezo vya kwao, tena vya kijinga - kumuenzi marehemu, na kwamba marehemu mwenyewe alitamka kuwa Chato utakuwa mkoa. Ujinga mtupu!!
 
Hivi mbona mnaisena geita tu wakati inamegwa mikoa mitatu?? Hivi population ya Lindi ukiitenga si utaunda mkoa wa mapori tu??
Poor argument. Chato ipo wapi? Wanaposema mkoa mpya umemegwa toka mkoa fulani, hatuangalii maeneo ya kujazilizia. Wewe unajua kuwa maeneo kama ya Mbogwe yalikuwa Shinyanga lakini baada ya kuimega Geita toka Mwanza, yakaingizwa Geita? Umewahi kusikia hata siku moja ikitamkwa kuwa Geita ilimegwa toka Mwanza na Shinyanga?
 
Well said!!!! Mtu anakuja na akili zake eti mbona Lindi ni kubwa hawajaitenga huku akijua eneo kubwa ni pori
Ni uwendawazimu na ujinga wa hali ya juu kufikiria kuwa mahali pakiwa na watu wengi lazima pawe mkoa.

Chato haikidhi hata kigezo kimojakuwamkoa. RCC members nadhani wote ni low IQ.
 
Ni ujinga kufikiria kukiwa na mikoa mingi ndiyo maendeleo.
 
Ndo maana nasema hawaangalii factor moja, mkoa kama Kagera una watu wengi ila bado ni mkubwa pamoja jiografia yake imekaa vibaya. Sasa ukisema utenge Dar au Kilimanjaro haiwezekani huko
Ukubwa wa mkoa wa kagera ni upi? Na jiografia gani iliyokaa vibaya kama kwa siku moja unaweza kuzifikia wilaya zote za mkoa huo.
 
Nikuulize swali. Tazama mkoa wa Dar,Tazama mkoa wa Kilimanjaro,tazama mkoa wa Tanga. Hii ni mikoa yenye wilaya nyingi Sana pamoja na kuwa na eneo dogo hiv Kwa nini.

Population, population na population density!!! Huwezi ukata mkoa wa Lindi mkoa wenye 1m people na density ya 12 per square metre utengeneze mkoa mpya. Hiv utatengeneza mkoa wenye mbuga navichaka. Hivyo hivyo Kwa tabora,singida nk



Hapa mnachangia kisiasa Sana Kwa sababu mnaangalia chato Tu. Kumbuka mkoa huu utatengenezwa na wilaya mbili kongwe za mkoa wa kagera. Mkoa wenye population ya 3.1 million ukiwa wa tatu nchini nyuma ya Dar na mwanza, na wenye population density ya 124 people per square km.pia ukiwa nyuma ya Dar na mwanza.

Naunga mkono Sana mkoa mpya Ila husiitwe chato uitwe biharamulo au jina lingine
 
Kwani Nyakanazi iko Mkoa wa Kigoma ? Nyakanazi iko wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera, kwanini uwaze kuunganisha na Kakonko na Kibobdo ?
 
Hata kama ni population inaonyesha chato haina population sana hivyo inawalazimu kuchukua maeneo mikoa mingine. Ukiangalia sehemu kubwa ya mkoa wa Chato itatoka kagera hivyo wilaya ya Biharamulo yenye population kuizidi chato ndio itaonyesha chato kukidhi vigezo.
Kama chato inakidhi vigezo ya nini sehemu kubwa ya mkoa huo itoke kwingine (Biharamulo,ngara na Kakonko)?.
Hapo chato kuwa mkoa ni sababu za kisiasa wala si vinginevyo.
Ukielewa Andiko jipige kifuani sema umefumbuka, ila usipo elewa chukua maji kunywa harafu pumzika kwa mbali ukiskia pini za Dizasta vina
Asante
 
Tueleze ubora wa Nyakanazi kuzidi Chato ambayo pia iko kwenye mwambao wa Ziwa Victoria
Binafsi na mimi sipendezwi na makao ya mkoa kuwa chato, nyakanazi ndo pazuri kabisa lakini kama imetokea pakawa chato waache kakonko wajumuishwe maana ni afadhali kuliko kwenda Kigoma
 
Wizara ndio yenye mamlaka. Siyo hao waha wa Kakonko
 
Kwa hiyo wew ulitaka wakikata mkoa wasiombe wilaya nyingine kutoka mikoa mingine?

Mbona ni kawaida hii kwenye kuunda mikoa?

Hata huo mkoa wa geita uliichukua chato kutoka kagera mbona hakuwepo haya malalamiko.



Watu wapo kisiasa hapa sio kiuhalisia
 
Sengerema kiuhalisia ilitakiwa kuwa Geita maana ilikuwa ndani ya wilaya ya Geita hadi 1975.
Mkuu wa mkoa anakama siku 10 mkoa hapo ila anajifanya kujua mambo.
Ngoja tusubiri akina Msukuma waliongelee hili
 
Geita ulistahili ila kwa chato bado sana hapo utaanza kujiuliza kwa nini mzee alipendelea chato zaidi ya Geita yenyewe?
Hapo utajua haya yapo kisiasa sana nasi vigezo husika
 
Sengerema kiuhalisia ilitakiwa kuwa Geita maana ilikuwa ndani ya wilaya ya Geita hadi 1975.
Kweli mkuu.
Ila kanda ya ziwa kutakuwa na utitili wa mikoa, au chato itakua kanda ya magharibi ikijumuishwa kigoma na Tabora?
 
Hata walipokuwa wanaunda mkoa wa Rukwa mwaka 1974 walichukuwa Sumbawanga kutoka Mbeya na Mpanda kutoka Tabora. Au ulikuwa hujazaliwa ?
 
Geita ulistahili ila kwa chato bado sana hapo utaanza kujiuliza kwa nini mzee alipendelea chato zaidi ya Geita yenyewe?
Hapo utajua haya yapo kisiasa sana nasi vigezo husika
Ndo maana nasema wengi hapa wanachangia hoja kisiasa.


Mkoa utengenezwe lakin makao makuu ya wilaya yawe nyakanazi au biharamulo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…