Kwanini China nchi ya kidikteta ina maendeleo makubwa kuliko Kenya na Zambia?

Kwanini China nchi ya kidikteta ina maendeleo makubwa kuliko Kenya na Zambia?

Umesah
Sababu ni nyingi,
Kwanza lazima ufahamu China wana msingi mkubwa wa uvumbuzi na ubunifu wa miaka mingi, Dira, gunpowder, karatasi na mashine za kale za kuchapa ziligunduliwa China.

Pili udikteta wa China ni udikteta wa mfumo wa meritocracy, sio udikteta kama wa Waafrika wa "unanijua mimi ni nani" au baadhi ya familia kuhodhi utawala wa nchi.

Lingine demokrasia ni muhimu sana lakini haikupi kila kitu, ili demokrasia ikusaidie inahitaji mazingira wezeshi pia ambayo hayako kwa nchi nyingi za Africa.
Mfano ni kutokuwepo utamaduni wa rushwa, nepotism, ukabila, raia wengi wajinga n.k
umesahau pointi moja muhimu sana. Uchumi wa Afrika unasimamiwa na mabepari. Nchi ikienda speed kimaendeleo, itapigwa tukio ili kuipunguza kasi.

Hii ndiyo sababu kubwa ya umaskini wa nchi zetu.
 
Alitumia mbinu ambayo mpaka leo China wanaitumia kupata maendeleo, aliwapa watu wake uhuru wa kufanya wanachokipenda kila mtu afanye kwa vile anavyopenda unapenda kilimo lima, unapenda ufugaji fuga, nk watu walifanya kazi kuendana na constellation zao bila kuchanganywa snake afanye kazi za snake na rabit afanye kazi za rabit bila kuwamix huyu unamuweka huku na huyu unamuweka huku
Sawa sawa sawa
 
China hawacheki na kima ujue. Mfano, jengo lililoporomoka Kariakoo jana; asubuhi ya leo wananchi wangekuwa wamekusanyika viwanja vya Mnazi Mmoja kushuhudia mass execution ya wote walioshiriki ujenzi ule! Mko tayari au ni siasa za kulindana?
Basi hatari hawana mchezo
 
Demokrasia ni nzuri, ukiwa na maendeleo na Demokrasia pamoja ni vizuri zaidi. Ukiwa na Demokrasia na maendeleo kidogo kuna afadhali, ukiwa na maendeleo bila Demokrasia kuna afadhali, ukiwa huna Demokrasia na huna maendeleo ni sawa na uko jehanamu.

Pia Demokrasia haizuii maendeleo ila udikteta sehemu nyingi unazuia maendeleo na kusababisha machafuko na vurugu pia.
Nakuelewa
 
Maendeleo ya China, licha ya mfumo wa chama kimoja, yamefanikiwa kwa sababu ya mchanganyiko wa sababu za kihistoria, kijamii, kiuchumi, na kisiasa.

1. Utawala wa Muda Mrefu na Mpango Endelevu
- Mfumo wao wa chama kimoja wa unawawezesha viongozi kupanga mipango ya muda mrefu bila vikwazo vya kisiasa vinavyosababishwa na chaguzi za mara kwa mara.

- Mpango maarufu kama Five-Year Plans umewezesha maendeleo endelevu kwenye sekta kama viwanda, teknolojia, na miundombinu.

Kwa mfano, miradi mikubwa kama Reli ya Kasi ya Juu ya China ilifanikiwa kutokana na umoja wa kisiasa na maono ya muda mrefu.

2. Vipaumbele vya Ufanisi wa Uchumi
- China imeweka mkazo kwenye uchumi wa soko huria unaodhibitiwa na serikali. Mfumo huu huruhusu uwekezaji mkubwa wa umma kwenye miundombinu na sekta za kimkakati kama teknolojia na viwanda.

- Serikali inahakikisha rasilimali zinatumiwa kwa ufanisi, huku ikihamasisha sekta binafsi kushiriki kwenye ukuaji wa uchumi.

Hii ni tofauti na nchi kama Kenya na Zambia, ambako mara nyingi siasa zao zinaweza kuathiri ugawaji wa rasilimali kwa sababu ya ushindani wa kisiasa au ufisadi.

3. Udhibiti wa Kisiasa na Nidhamu

Mfumo wao unazuia mgawanyiko wa kisiasa, migogoro ya vyama, au machafuko yanayochelewesha maendeleo.

Serikali ina uwezo wa kutekeleza sera bila changamoto kubwa za mgawanyiko wa kisiasa au vikwazo vya kisheria.

Mfano, Kenya na Zambia mara nyingi hukumbwa na changamoto za kisiasa kama migawanyiko ya kikabila na migogoro ya kisiasa inayochelewesha maendeleo.

4. Uwekezaji Mkubwa katika Teknolojia na Elimu
- China imewekeza sana kwenye utafiti wa kisayansi, elimu ya hali ya juu, na maendeleo ya kiteknolojia. Uwekezaji huu umeiwezesha kuwa kiongozi wa ulimwengu katika sekta za viwanda, nishati mbadala, na teknolojia za mawasiliano.

- Kwa upande mwingine, nchi nyingi za Afrika bado zinawekeza kidogo katika sekta hizi, zikikabiliwa na changamoto za bajeti na utegemezi wa misaada kutoka nje.

5. Idadi Kubwa ya Watu na Soko Lenye Ushindani
- Idadi kubwa ya watu wa China imeunda soko kubwa la ndani na nguvu kazi ya gharama nafuu. Hili limevutia wawekezaji wa kimataifa kuhamisha viwanda na uzalishaji kwenda China.

- Kenya na Zambia, zikiwa na idadi ndogo ya watu na masoko madogo, mara nyingi hazivutii kiwango sawa cha uwekezaji wa kigeni.

6. Udhibiti Mkali wa Ufisadi
- Ingawa China imekumbwa na changamoto za ufisadi, serikali imeanzisha kampeni kali za kudhibiti tatizo hili, ikiwemo hatua dhidi ya maafisa waandamizi wa chama na sekta binafsi.

- Kwa upande mwingine, ufisadi ni changamoto kubwa kwa maendeleo ya nchi za Afrika, huku ukisababisha kupotea kwa fedha nyingi zinazoweza kutumika kwa maendeleo.

7. Miundombinu ya Kisasa na Uwekezaji wa Umma
- China imefanikiwa kujenga barabara, reli, na miji ya kisasa kupitia uwekezaji wa moja kwa moja wa serikali. Miradi hii ni sehemu ya mkakati wa kukuza uchumi na biashara.

- Afrika, ingawa inafanya juhudi, mara nyingi haina rasilimali za kutosha na ina utegemezi mkubwa kwa misaada ya kimataifa.

Ova
Sawa sawa sawa
 
Udikteta (kutoka neno lenye asili ya Kilatini: dictator; pia: imla kutoka Kiarabu) ni mfumo wa utawala wa nchi ambapo mtu mmoja asiyebanwa na sheria wala katiba anashika madaraka ya serikali na ana uwezo wa kuyatumia jinsi anavyoamua mwenyewe.
Sasa mbona China inaendeshwa tofauti kabisa na hiyo definition yako hiyo?
China ukizingua haijalishi ww ni nani una cheo gani utakula kitanzi na mchakato wao wa kula kitanzi huwa sio mrefu ,hukumu ya kitanzi inatoka leo na inaelelezwa ndani ya wiki.
 
Udikteta (kutoka neno lenye asili ya Kilatini: dictator; pia: imla kutoka Kiarabu) ni mfumo wa utawala wa nchi ambapo mtu mmoja asiyebanwa na sheria wala katiba anashika madaraka ya serikali na ana uwezo wa kuyatumia jinsi anavyoamua mwenyewe.
kwa tafsiri hii china sio nchi ya kidikteta......
wana katiba bora, wana sheria bora, wala neno la Xi sio sheria.......

magharibi ndio wameharibu tafsiri ya dikteta kwa kumwita dikteta kila mtu wanae mchukia
 
Sasa mbona China inaendeshwa tofauti kabisa na hiyo definition yako hiyo?
China ukizingua haijalishi ww ni nani una cheo gani utakula kitanzi na mchakato wao wa kula kitanzi huwa sio mrefu ,hukumu ya kitanzi inatoka leo na inaelelezwa ndani ya wiki.
Amekosea kidogo kusema mtu mmoja, kuna
Junta dictatorship,
Party dictatorship,
Theocracy
 
Back
Top Bottom