Kwanini Dar kuna shida ya maji wakati bahari ipo hapo hapo?

Kwanini Dar kuna shida ya maji wakati bahari ipo hapo hapo?

ngebe

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2020
Posts
1,789
Reaction score
5,117
Nimetanguliza neno sielewi kwamaana hiyo nimeuliza ili mnieleweshe.

Dar kuna bahari ya Hindi imeizunguka sasa inakuaje mkoa huo unakua na shida ya Maji?

Kama maji ya bahari labda yanahitaji kuchakatwa sana kuondolewa chumvi na kama ni ghali sana kununua mitambo hiyo, kwanini tunapoteza hela nyingi kununua mandege yasiyo na faida kwa mtanzania na tukaacha kufanya jambo la msingi kama hilo?

Au basi hizo tirioni kadhaa za kununua mandege yasiyo na tija, tungetoa maji ziwa victoria likahudumia nchi nzima hii
 
Niliwahi kunywa maji ya bahari hapo feli kwa imani ya kuwa ni maji hayo ni dawa kwa sababu hukusanya uchafu wooote lkn hutakaswa na kiwango cha chumvi iliyopo. Kimsingi hayakati kiu labda hadi yachakatwe.
 
Nimetanguliza neno sielewi kwamaana hyo nimeulizabili mnieleweshe

Dar kuna bahari ya hindi imeizunguka sasa inakuaje mkoa huo unakua na shida ya Maji?....
Jambo hapa kwetu ni kukosa vipaumbele vya kitaifa, fikiria hakuna upungufu wa mvua umeme shida, itakuwaje Kuna upungufu wa mvua hapo kwenye umeme, je vipi kuhusu maji ambayo kwetu hata kama mvua inanyesha watu hawana maji safi na salama. Pindi tukiamua Kwa dhati kama taifa, kuifanya siasa safi na kuuzingatia kanuni za uongozi Bora, ndio itakuwa PONA ya taifa hili.
 
Nimetanguliza neno sielewi kwamaana hyo nimeulizabili mnieleweshe

Dar kuna bahari ya hindi imeizunguka sasa inakuaje mkoa huo unakua na shida ya Maji?


kama maji ya bahari labda yanahitaji kuchakatwa sana kuondolewa chumvi na kama ni ghali sana kununua mitambo hiyo kwanini tunapoteza hela nyingi kununua mandege yasiyo na faida kwa mtanzania na tukaacha kufanya jambo la msingi kama hilo?

Wafanya maamuzi ni vilaza, wenye akili Kama wewe wanapigwa vita huko maofisini.

Maradhi, ujinga na umasikini--Mlm JkN-
Mimi naongeza--akili mdogo(IQ) ndogo.

Ikitokea mimi nikapata nafasi ya kufanya maamuzi, cha kwanza Nita restructure utumishi, wata ajiriwa tu wenye high IQ na hao ndo watakuwa watumishi Serikalini.
 
Nafikiri mwaka huu itabidi baadhi ya shughuli zinazotumia maji zithibitiwe, mfano waosha magari wengi wanatumia maji hovyo hovyo. Unakuta maji ambayo yangeosha gari hata thelathini, jamaa anatumia kwenye gari moja.

Wangwekewa masharti ya kutumia vifaa vinavyonyunyiza maji kidogo au mvuke siyo kumwaga mwaga tu maji bila mpangilio.....kule south afrika walipata shida ya maji kutokana na ukame uliodumu muda mrefu ilikuwa patashika, nakumbuka kipindi hicho nilienda huko, hotelini unakutana na tangazo la kutumia maji kwa uangalifu ikiwemo kuoga chini ya dakika tatu na mara moja kwa siku.....

Sasa ni bora wizara ya maji kuanza kuelimisha watu kutumia maji kwa usahihi na pale tu penye uhitaji.​
 
Jambo hapa kwetu ni kukosa vipaumbele vya kitaifa, fikiria hakuna upungufu wa mvua umeme shida, itakuwaje Kuna upungufu wa mvua hapo kwenye umeme, je vipi kuhusu maji ambayo kwetu hata kama mvua inanyesha watu hawana maji safi na salama. Pindi tukiamua Kwa dhati kama taifa, kuifanya siasa safi na kuuzingatia kanuni za uongozi Bora, ndio itakuwa PONA ya taifa hili.
Unasema 'hakuna upungufu wa mvua'
Mvua imegoma kabisa kunyesha ndugu yangu
 
Nimetanguliza neno sielewi kwamaana hiyo nimeulizabili mnieleweshe

Dar kuna bahari ya hindi imeizunguka sasa inakuaje mkoa huo unakua na shida ya Maji?

Kama maji ya bahari labda yanahitaji kuchakatwa sana kuondolewa chumvi na kama ni ghali sana kununua mitambo hiyo kwanini tunapoteza hela nyingi kununua mandege yasiyo na faida kwa mtanzania na tukaacha kufanya jambo la msingi kama hilo?
Ndege hazina Faida?

Wazo a kimasikini,
 
Dar es salaam ina maji kibao ardhini maendeo ya Kigamboni, Kiwanda cha maji cha Afya kinayapata huko hadi kuuza lita 1.5 kwa jero. Ni mipango tu, huwezi kuwa na jiji la watu 7m unategemea maji ya mto.

Water desalination ni gharama kubwa ndugu mtoa hoja, kutibu tatizo ni kuchimba visima na kuyaingiza maji hayo kwenye mfumo mkuu.
 
Mto Rufiji unapita takribani km 150 kutoka Dar. maji yake ni mengi lakini cha ajabu yote yanaelekea baharini. nafikiri tungemaliza huduma za jamii kwamza kabla ya kurukia miradi mikubwa isiyo na tija kwa watu wengi. shule hazina vyoo na madawati wewe unajenga reli ya mwendokasi!!!!
 
Nafikiri mwaka huu itabidi baadhi ya shughuli zinazotumia maji zithibitiwe, mfano waosha magari wengi wanatumia maji hovyo hovyo. Unakuta maji ambayo yangeosha gari hata thelathini, jamaa anatumia kwenye gari moja. Wangwekewa masharti ya kutumia vifaa vinavyonyunyiza maji kidogo au mvuke siyo kumwaga mwaga tu maji bila mpangilio.....kule south afrika walipata shida ya maji kutokana na ukame uliodumu muda mrefu ilikuwa patashika, nakumbuka kipindi hicho nilienda huko, hotelini unakutana na tangazo la kutumia maji kwa uangalifu ikiwemo kuoga chini ya dakika tatu na mara moja kwa siku.....sasa ni bora wizara ya maji kuanza kuelimisha watu kutumia maji kwa usahihi na pale tu penye uhitaji.​
Nchi haijafikia huko hebu tulia, tuna maziwa na mito ya kutosha ni serikali yako tu yakiPumbafu, kama umemuelewa mleta mada lakini¿
 
Nchi haijafikia huko hebu tulia, tuna maziwa na mito ya kutosha ni serikali yako tu yakiPumbafu, kama umemuelewa mleta mada lakini¿
Kwa hiyo huamini kwamba kuna upungufu mkubwa kwenye vyanzo vya maji, au ndo ile kenge hasikii hadi damu itoke masikioni......
 
Back
Top Bottom