Nafikiri mwaka huu itabidi baadhi ya shughuli zinazotumia maji zithibitiwe, mfano waosha magari wengi wanatumia maji hovyo hovyo. Unakuta maji ambayo yangeosha gari hata thelathini, jamaa anatumia kwenye gari moja.
Wangwekewa masharti ya kutumia vifaa vinavyonyunyiza maji kidogo au mvuke siyo kumwaga mwaga tu maji bila mpangilio.....kule south afrika walipata shida ya maji kutokana na ukame uliodumu muda mrefu ilikuwa patashika, nakumbuka kipindi hicho nilienda huko, hotelini unakutana na tangazo la kutumia maji kwa uangalifu ikiwemo kuoga chini ya dakika tatu na mara moja kwa siku.....
Sasa ni bora wizara ya maji kuanza kuelimisha watu kutumia maji kwa usahihi na pale tu penye uhitaji.