Kwanini Demokrasia ilishindwa kuleta maendeleo China?

Sasa, hao jamaa mbona kimaendeleo wako mbali sana kinyume kabisa na wengi wanavyoamini kwamba, Demokrasia ndiyo huleta maendeleo?

Ni chaguo la nchi mfumo gani wanautaka kuna nchi tajiri zina demokrasia na nchi maaikini dikteta. North Korea wana dikteta na ni masikini . Mfumo wa kidemokrasia nchi yetu ndiyo imeona unatufaa na kama tumeamua hili tufuate misingi yake na sio kujichanganya. Kama hatutaki demokrasia basi tubadilishe katiba na kufuata misingi ya hiyo system nyingine lakini hatuwezi kuwa na katiba ya kidemokrasia na utekelezaji ukawa udikteta hapo ndipo unapata tabu
 
Wee kilaza tangu lini China iliwahi kuwa na demokrasia?
 
Usipotoshe: Uchumi wa Tanzania umeharibika kwa sababu ya Corona
Halafu hili linasahaulika sana kwa watu, na hata hivyo, endapo nchi yetu ingewekwa lockdown kipindi kile cha Corona ya awali kabisa, hali ingekuwa ni mbaya kuliko ukilinganisha na tulipo sasa
 
usilinganishe CHINA na TANZANIA. Wenzetu hata kielimu wapo juu, nchi inaongozwa na sayansi. Sasa bongo elimu haizingatiwi tunajiendea tu no direction.
 
Nani alikudanganya uongo huo dogo?

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 

Kitu ambacho wengi hawakijui, ni kuwa demokrasia inaenda sambamba na desturi za watu husika. Kikiletwa kitu kigeni, halafu unakilazimishia kikubalike na jamii husika haraka haraka, matokeo yake hayawi mazuri. China wanafanikiwa na wanaendelea kufanikiwa kwa sababu hawaruhusu kuingiliwa na watu kutoka nje. Wakitaka jambo jipya kutoka nje, basi watalichunguza na kuamua walichukue kwa kiasi gani na walitumieje. Hiyo ni tofauti na Afrika. Shida ya Afrika ni kuwa kila mtu kutoka nje anadhani ana uelewa mkubwa wa kutuambia nini waAfrika tunapaswa kufanya. Hilo limepelekea kila mtu kutoka nje anayehisi ana jambo anatuletea. Matokeo yake Afrika imechanganyikiwa haijui inaelekea wapi. Inasikitisha sana.
 
U aelewa nini maana ya demokrasia?(
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana, bila ya kuwaburuza mambo hayaendi...
 
Demokrasia ndo mdudu anaetutafuna kwenye nchi masikini za kiafrika vijana hawafanyi kazi wanaacha maeneo, mabonde ya kulima mpunga wanakimbilia mijini (machinga) wanachochangia kwenye Pato la Nchi ni kidogo Sana .viongozi ni wezi wanalindana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…