Sio kweli, Dubai wameweza kushawishi watu kwenda Dubai sio kwa maneno tu bali vitendo. Kitu kikubwa wameifanya Dubai kuwa salama, ni sehemu pekee nenda na family yako tembea usiku na mchana na na usiwe na hofu ya chochote, wamejenga malls kubwa kabisa za kisasa na brand kubwa duniani wapo, hotel za kisasa na viwango. Leo hii Dar unaweza kwenda kulipa Hotel dola 200 standard ya kawaida kwa maana ya quality lakini Dubai ukaa Hotel kama King same price au low.
Wame set quality kwa service zote nenda kale KFC ya Dubai halafu njoo KFC ya Bongo ni mbingu na ardhi. Uber zao order ni Lexus model mpya hawaruhusu gari chini ya 5 years model na ni Lexus mpya huku Tz unaweza kukuta matajiri wachache sana wanamiliki. Kiujumla standard iko juu na hata huko chini kama Deira kwa watu wa chini au wafanya biashara standard iko chini kulinganisha na maeneo mengine ya Dubai lakini bado standard iko juu kulinganisha na Hotel zetu za Dar. Dubai ni wewe mwenyewe utaenda na ukirudi utaenda tena na tena na tena, kwanini? wanakupa unachokitaka wewe na kama sio wewe mke wako na mpaka watoto.