Bahati mbaya ni kwamba Adam na Hawa pamoja na nyoka walilaaniwa onthe sport lakini mr sheth akaachwa akipeta.
Matusi haya yote yanasababishwa na ndugu zetu wakristo wenyewe kwa kugeuziwa maandiko nao wakakubali kufuata. Ona sasa wakina zabron na wenzake wanavyojipatia points kwajili ya huo upotevu wenu.
Sasa bwana Zabron ngoja nikuweke sawa kwa upande wa waislamu... ni kwamba Adam na Hawa waliumbwa wakawekwa peponi (siyo bustani za hapa duniani)
Kwanza nikurudishe nyuma kidogo ni kwamba mola aliumba dunia na vilivyomo kitambo kidogo kabla ya kumuumba mwanadamu. Sasa inasemekana (kwa mujibu wa maelezo ya wanazuoni wengine) kwamba majini waliumbwa wakaishi duniani lakini walifanya ufisadi na kumwaga damu hata ikafika siku hiyo wanapambana na kuuana wao kwa wao ndipo malaika wakashuka kutoka mbinguni wakakuta katoto kadogo ka kijini kametelekezwa kamebaki peke yake wengine wote wamekufa. Malaika wakasepa na kile kitoto mbinguni kwa idhini ya mola wao, kikawa kinaishi na malaika kule mbinguni na mambo mengi ya kule kikishiriki nao mpaka kikawa kikubwa kijini kile. Stori hii huikuti kwenye Quran ila ni juhudi za wafasiri wa mambo ya dini kama tutavyoona mbeleni
Pili sasa ndo tuingie kwenye historia kamili ya huyu shetani (ambapo hii na nitakayoandika yote yanayofuata yanapatikana katika Quran). Ni kwamba yeye bwana ibilisi(jini) na malaika walikuwa wachamungu sana huko mbinguni. Siku hiyo Mola akawaambia nataka nipeleke kiongozi kule ardhini yaani duniani, malaika na yule jini wakamjibu Mola wao "kwanini upeleke viumbe ambao watafanya fisadi na kumwaga damu burebure bila sababu wakati sisi tupo hapa tunakusabihi (tunakusifu) na kukuabudu wala hatukuasi hata mara moja?" Mola akawaambia "mimi najua yale msiyoyajua". Hiyo hoja waliyotoa malaika hapo ndio baadhi ya wasomi wakasema kwamba maneno hayo yanaashiria wale malaika na yule jini kuna wanachokijua mpaka kusema vile (kwamba walihofia kisije kikatokea kama nilichosema hapo mwanzo)
Basi mola akamuumba Adam (na kuumba kwake siyo huko mnavyofikiria au mnavyoaminishwa bali ni kwa tamko la kusema tu KUWA na kitu kinakuwa). Kisha akamfundisha Adam majina ya vitu vyote na akamleta mbele ya malaika na yule jini. Mola akahudhurisha yaani akavileta vitu vyote mbele yao na kuwaambia malaika na yule jini "nitajieni majina ya vitu hivi-kimoja baada ya kingine" malaika wakajibu "hatuna ujuzi wa elimu yoyote sisi ila ile uliyotufunza" (wakimaanisha hawajui majina ya vitu) basi Adam akaambiwa ataje akataja vyote bila kukosea wala kuchanganya wala kukosea wala kukwamakwama ndipo Mola akasema tena "je sikuwaambia kuwa mimi najua msiyoyajua?". Ndipo wakaamrishwa na Mola wao wampe heshima Adam na hapo ndipo kimbembe kilipoanza. Wale malaika wote walionesha ishara ya utii kwa Adam isipokuwa ibilisi tu(jini) yeye alikataa na alipoulizwa kwanini akasema live bila kupepesa "mimi siwezi kumsujudia/kutoa salamu ya utii mtu ambae umemuumba kwa udongo uliovunda, mimi nimeumbwa kwa miali ya moto hivyo mimi ni bora kuliko yeye" (hapa anasema haya kwakuwa kama nilivyosema kabla yeye amekulia mbinguni na mambo mengi akawa anayajua kwahiyo hata kuumbwa kwa Adam aliona nk)
Baada ya kusema vile Mola akamwambia "basi toka na kuanzia leo laana iwe juu yako mpaka siku ya malipo (siku ya kiama)". Ili ujue kuwa jamaa alinuia kweli kweli badala ya kuomba msamaha yeye akasema "mola wangu basi nifanye nichelewe kufa mpaka siku ya kufufuliwa viumbe" Mola akamwambia kwa ombi lako hilo limekubaliwa -hutakufa mpaka siku ya wakati maalumu ikifika hiyo utakufa tu... ibilisi akasema "Mola wangu kwakuwa umenihukumia mimi hukumu mbaya hivi (kwajili ya haka kajamaa) basi nitahakikisha huko duniani nawapambia maovu (wayaone mazuri) na niwapoteze wote! Isipokuwa waja wako wachamungu waliosafika kweli kweli. Baada ya kupewa laana hiyo na yeye kusema aliyoyasema basi akaachwa akichanganyika na malaika kama kawaida huku Adam na mkewe (Hawa) wakipelekwa peponi kuishi
Wakaambiwa na Mola (Adam na Hawa) kaeni humo na kuleni kila kilichopo humo "na wala msiusogelee mti huu" (yaani kuna mti walikuwa wakiuona wenyewe kipindi wanaambiwa maneno haya- wala haukutajwa jina kwahiyo kama ni kuujua huo mti anaujua mwenyewe aliyekataza na aliyekatazwa kuusogelea)
Shetani akawatia wasiwasi akawashawishi wakausogelea ule mti na kula matunda yake (na hapa haijasemwa aliwadanganya kwa njia ya nyoka wala nini- yawezekana alitumia njia hizihizi anazotudanganya sasa kupitia moyoni mwa mtu tu).
Baada ya kula ndipo aibu zikawadhihirikia sasa wakaanza kujiziba kwa majani ya miti ya huko peponi. Palepale na akili ya kumbukumbu "wala msiukurubie mti huu" ikarudi sasa akawa haelewi bwana Adam itakuwaje maana ameshavunja sheria. Basi walipoulizwa kwanini wamekula kwenye ule mti wakatubia haraka sana kwa mola wao na Mola akawasamehe palepale. Baada ya hapo akawaambia shukeni ardhini mkaishi, nyinyi kwa nyinyi ni maadui. Ndipo Adam na Hawa wakaletwa duniani na shetani nae (bwana ibilisi) ukawa ni mwisho wake wa kuchanganyika na malaika, naye akaletwa duniani kazi yake kubwa ikiwa ni ileile aliyojinadi mbele ya Mola wake kuwa ataifanya duniani.
Tatu ndo nirudi sasa Kuhusu ishu ya ibilisi na Adam na mkewe kwa maelezo hayo utaona wakristo tunatofautiana. Misimamo yao wakristo ndo inawapa nguvu wakina Zabron Kiranga Kenzy Scars nk kuzidi kutukana watu humu
-ibilisi ni jini muasi wao wanasema malaika muasi... hivi kweli malaika anaasi
-mti haujatajwa jina wala kufafanuliwa baadhi yao wanasema eti tunda lenyewe ni ngono eti "mti wa katikati"... hivi kweli Mola afiche namna hiyo kuhusu ngono
-Adamu na Hawa walitubia na wakasamehewa kabla ya kushushwa ardhini wao wanasema Adam na Hawa walilaaniwa yaani hata kuja duniani ni laana... utaona hata memes nyingi watu wanamlaumu Adam na Hawa eti bila wao kula tunda tungekuwa tunapiga misele peponi tu saivi, thubutu!
-Kuletwa duniani ilikuwa planned tangu Adam hajaumbwa ila wakristo wanaamini kuletwa duniani ni laana kwahiyo wote sisi tumelaaniwa eti
Nakaribisha maswali kuhusu nilichoandika kama mtu ataleta matusi sitahangaika nae