Kwanini Eva hakushtuka alipoanza kusemeshwa na nyoka pale bustani ya Eden?

Kwanini Eva hakushtuka alipoanza kusemeshwa na nyoka pale bustani ya Eden?

Ni kwamba kipindi hicho wanyama walikuwa wanaongea au?

Kama sivyo, kwanini huyo bibi yetu hakushtuka na kukimbia kwa Adamu kuomba msaada?
,
FMY-rRBXEAIAZmQ.jpg
 
Pale bustanini walikuwa watu wawili. Unadhani alikuja na umbo gani? Na kwanini Mungu alimhukumu nyoka kama hakuja na umbo la nyoka?
Ibilisi ni jinni,katika umbo ambalo jinni hupenda kujiweka ili binaadam amuelewe ni umbo la nyika,yeah jinni anaweza kuongea
 
1. Hivi kama kweli wanyama walikuwa wakiongea kama binadamu kwenye biblia kuna mstari unaoeleza kukoma kwa uwezo wao wa kuongea?
2. Ni nyoka tu "mwerevu kuliko wanyama wote" ndiye alikuwa na uwezo wa kuongea au wanyama wote?
3. Hata wadudu kama sisimizi nao walikuwa na uwezo wa kuongea? Kwa udogo wake sisimizi sauti yake ilikuwa na ukubwa gani ili aweze kusikika?

Ila kiukweli kuna mengi katika imani zetu tusiyo na majibu yake.
Kwa mujibu wa Qur'an huyo alikua ibilisi,ibilisi ni jinni,jinni ana uwezo wa kuongea na kujibadili,hakuna ajabu hapo
 
Bahati mbaya ni kwamba Adam na Hawa pamoja na nyoka walilaaniwa onthe sport lakini mr sheth akaachwa akipeta.
Matusi haya yote yanasababishwa na ndugu zetu wakristo wenyewe kwa kugeuziwa maandiko nao wakakubali kufuata. Ona sasa wakina zabron na wenzake wanavyojipatia points kwajili ya huo upotevu wenu.

Sasa bwana Zabron ngoja nikuweke sawa kwa upande wa waislamu... ni kwamba Adam na Hawa waliumbwa wakawekwa peponi (siyo bustani za hapa duniani)

Kwanza nikurudishe nyuma kidogo ni kwamba mola aliumba dunia na vilivyomo kitambo kidogo kabla ya kumuumba mwanadamu. Sasa inasemekana (kwa mujibu wa maelezo ya wanazuoni wengine) kwamba majini waliumbwa wakaishi duniani lakini walifanya ufisadi na kumwaga damu hata ikafika siku hiyo wanapambana na kuuana wao kwa wao ndipo malaika wakashuka kutoka mbinguni wakakuta katoto kadogo ka kijini kametelekezwa kamebaki peke yake wengine wote wamekufa. Malaika wakasepa na kile kitoto mbinguni kwa idhini ya mola wao, kikawa kinaishi na malaika kule mbinguni na mambo mengi ya kule kikishiriki nao mpaka kikawa kikubwa kijini kile. Stori hii huikuti kwenye Quran ila ni juhudi za wafasiri wa mambo ya dini kama tutavyoona mbeleni

Pili sasa ndo tuingie kwenye historia kamili ya huyu shetani (ambapo hii na nitakayoandika yote yanayofuata yanapatikana katika Quran). Ni kwamba yeye bwana ibilisi(jini) na malaika walikuwa wachamungu sana huko mbinguni. Siku hiyo Mola akawaambia nataka nipeleke kiongozi kule ardhini yaani duniani, malaika na yule jini wakamjibu Mola wao "kwanini upeleke viumbe ambao watafanya fisadi na kumwaga damu burebure bila sababu wakati sisi tupo hapa tunakusabihi (tunakusifu) na kukuabudu wala hatukuasi hata mara moja?" Mola akawaambia "mimi najua yale msiyoyajua". Hiyo hoja waliyotoa malaika hapo ndio baadhi ya wasomi wakasema kwamba maneno hayo yanaashiria wale malaika na yule jini kuna wanachokijua mpaka kusema vile (kwamba walihofia kisije kikatokea kama nilichosema hapo mwanzo)

Basi mola akamuumba Adam (na kuumba kwake siyo huko mnavyofikiria au mnavyoaminishwa bali ni kwa tamko la kusema tu KUWA na kitu kinakuwa). Kisha akamfundisha Adam majina ya vitu vyote na akamleta mbele ya malaika na yule jini. Mola akahudhurisha yaani akavileta vitu vyote mbele yao na kuwaambia malaika na yule jini "nitajieni majina ya vitu hivi-kimoja baada ya kingine" malaika wakajibu "hatuna ujuzi wa elimu yoyote sisi ila ile uliyotufunza" (wakimaanisha hawajui majina ya vitu) basi Adam akaambiwa ataje akataja vyote bila kukosea wala kuchanganya wala kukosea wala kukwamakwama ndipo Mola akasema tena "je sikuwaambia kuwa mimi najua msiyoyajua?". Ndipo wakaamrishwa na Mola wao wampe heshima Adam na hapo ndipo kimbembe kilipoanza. Wale malaika wote walionesha ishara ya utii kwa Adam isipokuwa ibilisi tu(jini) yeye alikataa na alipoulizwa kwanini akasema live bila kupepesa "mimi siwezi kumsujudia/kutoa salamu ya utii mtu ambae umemuumba kwa udongo uliovunda, mimi nimeumbwa kwa miali ya moto hivyo mimi ni bora kuliko yeye" (hapa anasema haya kwakuwa kama nilivyosema kabla yeye amekulia mbinguni na mambo mengi akawa anayajua kwahiyo hata kuumbwa kwa Adam aliona nk)

Baada ya kusema vile Mola akamwambia "basi toka na kuanzia leo laana iwe juu yako mpaka siku ya malipo (siku ya kiama)". Ili ujue kuwa jamaa alinuia kweli kweli badala ya kuomba msamaha yeye akasema "mola wangu basi nifanye nichelewe kufa mpaka siku ya kufufuliwa viumbe" Mola akamwambia kwa ombi lako hilo limekubaliwa -hutakufa mpaka siku ya wakati maalumu ikifika hiyo utakufa tu... ibilisi akasema "Mola wangu kwakuwa umenihukumia mimi hukumu mbaya hivi (kwajili ya haka kajamaa) basi nitahakikisha huko duniani nawapambia maovu (wayaone mazuri) na niwapoteze wote! Isipokuwa waja wako wachamungu waliosafika kweli kweli. Baada ya kupewa laana hiyo na yeye kusema aliyoyasema basi akaachwa akichanganyika na malaika kama kawaida huku Adam na mkewe (Hawa) wakipelekwa peponi kuishi

Wakaambiwa na Mola (Adam na Hawa) kaeni humo na kuleni kila kilichopo humo "na wala msiusogelee mti huu" (yaani kuna mti walikuwa wakiuona wenyewe kipindi wanaambiwa maneno haya- wala haukutajwa jina kwahiyo kama ni kuujua huo mti anaujua mwenyewe aliyekataza na aliyekatazwa kuusogelea)

Shetani akawatia wasiwasi akawashawishi wakausogelea ule mti na kula matunda yake (na hapa haijasemwa aliwadanganya kwa njia ya nyoka wala nini- yawezekana alitumia njia hizihizi anazotudanganya sasa kupitia moyoni mwa mtu tu).

Baada ya kula ndipo aibu zikawadhihirikia sasa wakaanza kujiziba kwa majani ya miti ya huko peponi. Palepale na akili ya kumbukumbu "wala msiukurubie mti huu" ikarudi sasa akawa haelewi bwana Adam itakuwaje maana ameshavunja sheria. Basi walipoulizwa kwanini wamekula kwenye ule mti wakatubia haraka sana kwa mola wao na Mola akawasamehe palepale. Baada ya hapo akawaambia shukeni ardhini mkaishi, nyinyi kwa nyinyi ni maadui. Ndipo Adam na Hawa wakaletwa duniani na shetani nae (bwana ibilisi) ukawa ni mwisho wake wa kuchanganyika na malaika, naye akaletwa duniani kazi yake kubwa ikiwa ni ileile aliyojinadi mbele ya Mola wake kuwa ataifanya duniani.

Tatu ndo nirudi sasa Kuhusu ishu ya ibilisi na Adam na mkewe kwa maelezo hayo utaona wakristo tunatofautiana. Misimamo yao wakristo ndo inawapa nguvu wakina Zabron Kiranga Kenzy Scars nk kuzidi kutukana watu humu

-ibilisi ni jini muasi wao wanasema malaika muasi... hivi kweli malaika anaasi

-mti haujatajwa jina wala kufafanuliwa baadhi yao wanasema eti tunda lenyewe ni ngono eti "mti wa katikati"... hivi kweli Mola afiche namna hiyo kuhusu ngono

-Adamu na Hawa walitubia na wakasamehewa kabla ya kushushwa ardhini wao wanasema Adam na Hawa walilaaniwa yaani hata kuja duniani ni laana... utaona hata memes nyingi watu wanamlaumu Adam na Hawa eti bila wao kula tunda tungekuwa tunapiga misele peponi tu saivi, thubutu!

-Kuletwa duniani ilikuwa planned tangu Adam hajaumbwa ila wakristo wanaamini kuletwa duniani ni laana kwahiyo wote sisi tumelaaniwa eti

Nakaribisha maswali kuhusu nilichoandika kama mtu ataleta matusi sitahangaika nae
 
Asee mambo mengi muda mchache nyoka anaweza ongea? kama ni shetani aliingia ndani yake kwann nyoka ahukumiwe nyoka?kwann nyoka leo haongei?
 
Ni kwamba kipindi hicho wanyama walikuwa wanaongea au?

Kama sivyo, kwanini huyo bibi yetu hakushtuka na kukimbia kwa Adamu kuomba msaada?
Shetani ni roho hivyo ili ajidhihirishe katika ulimwengu wa mwili(physical world) anahitaji physical body. Kwa pale bustanini aliamua kumwingia nyoka na kumtia werevu ili kutimiza azma yake. Ni kama ambavyo leo hii tunaona watu wakiingiwa na mapepo kisha mapepo hayo kunena kwa kutumia vinywa vya watu hao waliovamiwa.

Ifahamike kwamba kila chenye mwili kina roho ndani yake. Hivyo siku zote mwili ni container la roho.

Mti wa katikati(wa ujuzi wa mema na mabaya) uliwekwa ili;

1.Kuwapa Adam na Hawa uhuru wa kuonesha commitment yao kwa Mungu(Kumbuka Mungu anapenda kutumikiwa kwa hiyari siyo shuruti) na ili kuthibitisha hili basi Mungu hata leo hii huwapa watu wake conditions(masharti) kadha wa kadha ili kuwapa fursa ya kuonesha utii na upendo wao kwake.

2. Mti ule uliwekwa kama ishara ya kimwili inayoashiria kwamba katika ulimwengu wa roho(ulimwengu ambao Adam na Hawa hawauoni ingawa upo) kuna tawala mbili kinzani yaani utawala wa mema(Mungu) na utawala wa mabaya(Shetani) na kwamba kila utawala unafanya kampeni juu yao ili waishi kwa kutumikia kusudi lake. Hivyo wanapaswa kuishi wakilitambua hilo na kuchukua tahadhari.

ZINGATIA: Kuwapa watu wake masharti ni utamaduni wa Mungu tangu vizazi na vizazi. Ukiacha Adama na Hawa kupewa amri ya kutokula matunda ya mti wa katikati ya bustani,Samsoni aliambiwa asinyoe nywele zake,Maria aliambiwa asinywe kilevi n.k. Dhumuni kuu likiwa ni kuweka nidhamu ya kumfanya muhusika atimize mapenzi ya Mungu kama Mungu atakavyo lakini pia kumpa fursa ya kuonesha utii na upendo wake kwa Mungu ambayo ni haki ya msingi ya katiba ya Mbinguni.

Furaha na Raha ya maisha ipo kwenye UHURU wa kuchagua ingawa kuna kubeba na kulipia gharama ya machaguo yetu.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu nimekuelewa kwenye maelezo yako mengine ila swali hapa ni kwanini bibi yetu Eva hakushtuka alipoanza kusemeshwa na nyoka physically?
 
Mkuu nimekuelewa kwenye maelezo yako mengine ila swali hapa ni kwanini bibi yetu Eva hakushtuka alipoanza kusemeshwa na nyoka physically?
Putin kuamua kuishambulia Ukraine hakukurupuka alianza kwanza kwa kukusanya taarifa muhimu kuhusu Ukraine ikiwemo nguvu na madhaifu yake vivyo hivyo shetani akitaka kuvamia mtu,ndoa,familia,ukoo n.k huwa hakurupuki. Anakusanya taarifa muhimu kwanza ili kumsaidia kuandaa SILAHA na MBINU muafaka kabla hajavamia na kushambulia.

Alipoujua udhaifu wa Hawa kwamba hana uwezo wa kusimamia msimamo wake consistently hadi apewe back up ya mumewe ndio maana akamvizia akiwa peke yake na kumrubuni. Umewahi kujiuliza kwa nini hakumwendea Adam?.

Hata leo hii haka ni kamchezo ambako shetani anakatumia kunasa watu wengi sana. POINTS OF STRENGTHS AND WEAKNESSES. Alijua STRENGTHS na WEAKNESSES za wote wawili na akaona mlango wa kuingilia ni Hawa.

Vita ni mchezo wa Timing.

Okay nashukuru sana mkuu, nimekuelewa.
 
isije ikawa nyoka anaezungumziwa ni huyu hapa chini. Maana akiamua kukuingiza kwenye msala. Utakujaju juta akisha haribu ananywea anajifanya tukio halimhusu kabisa.
Anakuponza mazima wakati asali alikula yeye. Na sometimes wewe ulikuwa huhitaji ni kiherehere chake.
 
Back
Top Bottom