Kwanini familia ya Kikwete inapendekeza mishahara kwa wake wa viongozi wakati tayari wengi wao wako serikalini?

Kwanini familia ya Kikwete inapendekeza mishahara kwa wake wa viongozi wakati tayari wengi wao wako serikalini?

JF ifike wakati mtu avune alichopanda , kurekebisha heading ya uzi huu kumeondoa uhalisia , uzi ulihusu Tamaa ya hiyo familia na kiukweli wanayo tamaa iliyopitiliza , kitu ambacho na nyinyi mnajua , sasa mnapomsitiri mnakuwa mnalenga kuokoa nini ?

Acheni nyeusi iitwe kwa rangi yake halisi
Mimi mwenyewe nimeshangaa heading imebadilika wakati haikuwa na shida kabisa.
 
Kwa kweli mama Salma hapa alitukosea sana.

Hivi kwa mfano mama Salma ana shida gani ya pesa hadi akadai nyingine?

Mipesa ya ubunge anayo, mipesa ya mumewe, mipesa ya shughuli zake binafsi, halafu bado anataka nyingine?

Wakati mwingine tuweke masilahi ya umma mbele
 
1710663675965.jpg
 
Tatizo sio mpeleka hoja. TATIZO NI HAO WALIOIPITISHA HIYO HOJA. Wabunge ndio walaumiwe
 
Kikwete tena; wazo la salma kikwete km salma, lkn matusi anayavaa kikwete na familia yake......Pole sana mzee wetu.
 
Ridhiwani atakuwa rais 2030 ili aendelee kuchuma. Moende au msipende.
Asiyependa ama atakayependa ni wewe na nafsi yako.

Haujatubebea dhima ya mawazo ya Watz wote.

na wewe siye Mwenyezi Mungu wa kuliamulia taifa lipitie mkondo wa kutawaliwa na mtu gani.
 
Moja kati ya makosa makubwa yaliyowahi kufanyika nchi hii ni kumpa Jakaya Kikwete madaraka ya uraisi. Pamoja na mapungufu makubwa aliyoonyesha kiungozi bado aliingiza familia nzima katika urais huku wakipigana vikumbo kutafuta fursa na kujipenyeza.

Mengi yanajulikana, lakini kinachoniuma zaidi ni familia yake kupeleka hoja ya kuwalipa pensheni wake wa viongozi. Kwa wasiofahamu hoja hii ilipelekwa bungeni na Mama Salma Kikwete ambaye ni mke wa Rais Kikwete. Hiki ni kiwango kikubwa zaidi cha tamaa zaidi hata tamaa ya fisi. Bila shaka hiki ndio legacy anayoacha Kikwete kwa familia yake, kutotosheka.

Pamoja na kufuja rasilimali za nchi katika kipindi chake, pamoja na mauwekezaji rasmi na yasiyo rasmi katika familia yake bado watu hawa hawatosheki?

Familia inakosa utu kabisa. Nchi ina ukata kutwa kuchwa kupokea misaada. Lakini kuna watu baba raisi, mama mbunge, kaka waziri bado hawatosheki wakaja na pensheni kwa wake wa viongozi.

Familia hii haikuona kabisa pesheni ndogo wanazolipwa watumishi wa umma, pengine ipeleke hoja bungeni na kutia ushawishi kwa Rais. Haikuona mishahara midogo yenyewe ikaona walichonacho waongezewe maradufu.

Kuna wakati Rais Magufuli alionyesha chuki ya wazi kwa Kikwete, pengine alichukia sana tamaa za Kikwete na familia yake.
Naunga mkono hoja
 
Duh..
 
🤔🤔🤔🤔🤔🤔Kuna watu na mambo yao ni mishangazo kwa jamii yenye kutafakari.Na ukiwaza kama mleta uzi utaulizwa maswali ya kijinga sana.
-Kwani hawana haki ya kuwa viongozi?
-Una wivu wa kike?
-Kwa nini baba yako hakuwa raisi ili mama yako awe first-lady mwenye ubunge na wewe ukawa mbunge mwenye uwaziri?
-Nini maana ya demokrasia na haki kwa kila mmoja bila upendeleo?
-Kwani sheria hutungwa na kupitishwa na mbunge mmoja tu?
-Ni dhambi mtu kueleza na kuomba hitaji lake kwa kutoa mawazo huru?
..and the blah blah questions go on and on!
📝🔊🆒👌👍👌👏👊🤝🙏🎁🗼🛡️
 
[emoji404][emoji344][emoji684][emoji108][emoji106][emoji108][emoji122][emoji109][emoji1666][emoji120][emoji320][emoji556][emoji2924]
Utakuwa unafaidi sehemu ya huu ufisadi wa awamu hii ya sita. Mawazo ya kipuuzi kabisa kwako ndio unayapigia vigelegele!.
 
Nyerere kama angewaona kina kikwete ni wahuni kwanini aliwaacha madarakani wakawa mawaziri huku aliona ? Unless na yeye alikuwa muhuni
Huyo nyerere hakuna anaweza kwepa lawama za nchii, kila kitu kilioriginate kutoka kwake
 
Hili la mama Salma Kikwete kujenga hoja ya kujenga ubinafsi kwa gharama za wananchi limemuweka hata Kikwete katik nafasi ya ufisadi.
Wanawatumikia wananchi kwa malipo, si kwa moyo.
Ikija tena....... ooooh Tanzania nakupenda......... tutasema kwa msingi upi?
Mkuu acha chuki! Chuki haimuachi mwenye nayo salama!
 
Inawezekana hata Nyerere alikuwa mhuni Ila uhuni wake haufanani na huyu Jamaa wa Msoga, mtu wa kujilisha na kujitwalia mema yote ya nchi na watu wake awapendao.
Hebu tujuzeni mabaya makubwa ya huyo bwana
 
Back
Top Bottom