DOKEZO Kwanini fremu Dodoma zinafungwa sana na biashara kufa kila uchwao?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mbona mkuu unacomment kimwamba sana?

Fuatilia kujua frem anazolalamikia kufungwa ni za biashara za mtaji wa kiasi gani.

Let say umefungua biashara ya duka la vyakula na vinywaji kwa mtaji wa sh. Millioni 5, hiyo kodi ya pango pamoja na kodi zingine za manispaa pamoja na kulipa msaidizi, utaziweza na ubaki na faida?

Wafanyabiashara wengi mjini mitaji yao ni midogo, hivyo ukubwa wa kodi za pango pamoja na utitiri wa kodi nyinginezo haziwezi kumwendeleza mfanyabiashara mdogo.

Na land lords wasipobadilisha misimamo yao kwa over expectations za kipato walizonazo kwa wapangaji wao, milango ya frem zao zitabakia closed bila faida yoyote.
 
Dodoma Pagumu ila kuna baadhi ya biashara kama ya Nafaka na vyakula unawezaza ifanya. Na uifanye kwa ukubwa mzunguko utauona, hukuna sehemu watu hawali.

Uza mchele jumla na reje toa shamba.

Ngano, Sukari na mafuta toa Dar kwenye mastoo ya wahindi waletee Wagogo uza chee kidogo kwa bei inayotembea sokoni.

Sabuni za miche na unga za kutosha jumla na rejareja

Malizia na Maji na vinywaji vya kutosha huu mji maji ni chumvi

Tia mzigo wa maana fremu tafuta mahali panafikika kirahisi na uwe na wasambazaji utapiga pesa mpaka utaikimbia..
 
Umekuja na mumeo au uko pekee?
 
Mkiambiwa biashara ni mfumo mnabisha...biashara sio ya kila mtu...yaan unakuta familia nzima hamjawah fanya biashara afu unajipendekeza lazima uchochore haswa...
Sasa turudi nyuma kwenye hizo familia za wafanyabiashara ni lazima kuna mwana familia wa kwanza kabisa kuanza kufanya biashara kisha ndio wengine wakafuatia. Hoja yako haina mashiko.
 
Ukiweza kulipa kodi 700k basi lazima mtaji pia utakua mkubwa sana.. si chini ya 50M. Alafu pia mfanyabiashara siku anataka aonewe huruma apige faida nyingi.
 
Tatizo la bongolala ni low purchasing power ya watu, wale wanaojiita middle class wakiwemo watumishi mishahara yao ni kiduchu na wanaishiwa mwanzoni tu mwa mwezi.......vipi watu wa tabaka la chini watakuwa na hali gani? utawasikia chawa kila uchwao wanaimba mama anaupiga mwingi.​
 
Varities = varieties. Congratulations my brother. You really have a calling in BROKEN ENGLISH
 
sasa dodoma ni pakuweka frem kwa shilingi laki saba?
 
Hao wanaofunga maduka ni wapuuzi. Ni wale watu wenye mihemko wakisikia kitu badala ya kufanya utafiti. Kuna wakati kulikuwa na upepo wa gesi ya Mtwara watu wakakimbilia kujenga hadi mahoteli ya kisasa matokeo yake ni kilio. Dodoma inakuzwa sana ila kiuhalisia hakuna kitu. Kusipokuwepo na mikutano Dom huwa ni ya hovyo. Mfanyabiashara smart hatakiwi kuwa na mihemko ya kijinga.
 
Siyo Dodoma tu ni Nchi nzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…