DOKEZO Kwanini fremu Dodoma zinafungwa sana na biashara kufa kila uchwao?

DOKEZO Kwanini fremu Dodoma zinafungwa sana na biashara kufa kila uchwao?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mbona mkuu unacomment kimwamba sana?

Fuatilia kujua frem anazolalamikia kufungwa ni za biashara za mtaji wa kiasi gani.

Let say umefungua biashara ya duka la vyakula na vinywaji kwa mtaji wa sh. Millioni 5, hiyo kodi ya pango pamoja na kodi zingine za manispaa pamoja na kulipa msaidizi, utaziweza na ubaki na faida?

Wafanyabiashara wengi mjini mitaji yao ni midogo, hivyo ukubwa wa kodi za pango pamoja na utitiri wa kodi nyinginezo haziwezi kumwendeleza mfanyabiashara mdogo.

Na land lords wasipobadilisha misimamo yao kwa over expectations za kipato walizonazo kwa wapangaji wao, milango ya frem zao zitabakia closed bila faida yoyote.
Yes tena kimwamba hasa...kwa kifupi...hajui biashara..landlords afanye nn...jenga na ww upangishe...kabla ya kuanza biashara yako fanya utafiti wa kutosha...jua walaji wa biashara yako...location...mtaji wako...nk..vingine utajiongeza
 
Nipo dodoma kikazi ila ninachojionea ni balaa ,

Fremu nyingi zinafungwa na watu wameshindwa biashara,

Najiuliza tatizo ni nini , Nilijaribu kuuliza baadhi ya wadau , wengi wameniambia Cha kwanza bei za fremu ,

Utakuta fremu dodoma Hadi laki 7 ukija hizo Kodi za kufanya biashara mji huu ni utitiri wa Kodi , ambazo hazina kichwa wala miguu

Naomba viongozi wa Jiji la dodoma fatilieni hili swala , Pana haha Gani mtu alipe TBS ,tra, mzani , bibi afya, usafi , mzani ,mlinzi,fire,

Jamani uongozi wa Jiji la DODOMA mnaumiza wafanyabiashara ,
Naomba wenye mamlaka ingilieni kati,

Hii inafanya bidhaa dodoma kuwa kubwaa mno , inafanya watu kuishi dodoma ni changamoto
Kama viongozi wote wa nchi wapo dar, nani atanunua kwa fremu yako
 
Laki saba kwa mzungo gani wa biashara ,
700000/30= 23,333.33
Kwa siku lazima aweke 23,334 kwa ajili ya Kodi.
Alipe Kodi TRA
Alipe umeme
Alipe ushuru
Alipe usafiri per day
Ili biashara iwe vizuri lazima uwe na uwezo wa kupata faida laki moja na nusu kwa siku hafu ukitoa gharama zote hapo ubaki na hata 50000 kama net profit per day. Hapo biashara itasonga .
Hiyo biashara faida laki na nusu sio mchezo. Lazima mauzo kwa siku yawe 750k hadi 1m ambapo hapo kama ni nguo basi za jumla au sehemu yenye mzunguko mkubwa kama KKOO.
 
Hivi wewe...hyo mbona bei ya kawaida sana...kama unafanya biashara lakin...tena unaambiwa ulipie kwa miaka miwil...na ukishindwa tuu siku tatu nyingi inapata mteja harqka sana...NB: location mara nyingi ni towns...lakin kwa laki saba ni kawaida haswa..
Sio bei ya kawaida acha upotoshaji unajua vipato vya watanzania wengi ni milion kwa mwaka mzima

Laki 700 kwa mwezi ni ela kubwa sana ni bei za kariakoo hizo hata dar ukitoa kariakoo huku mtaani huwezi kuta laki 7 kwa mwezi
 
Yes tena kimwamba hasa...kwa kifupi...hajui biashara..landlords afanye nn...jenga na ww upangishe...kabla ya kuanza biashara yako fanya utafiti wa kutosha...jua walaji wa biashara yako...location...mtaji wako...nk..vingine utajiongeza
Sawa, pia formula yako ipo sawa.
Isipokuwa wenye hasara hapo ni landlords kwa sababu ya kukariri wanashindwa kwenda na bei na wakati kama kanuni ya soko inavyotaka.
 
Sio bei ya kawaida acha upotoshaji unajua vipato vya watanzania wengi ni milion kwa mwaka mzima

Laki 700 kwa mwezi ni ela kubwa sana ni bei za kariakoo hizo hata dar ukitoa kariakoo huku mtaani huwezi kuta laki 7 kwa mwezi
Mkuu nina ofisi mbili mkoani...moja nalipa laki nane kwa mwez na nyingine nalipa laki tano kwa mwezi...ukibisha njoo inbox nakupa na receipts kabisaa...yaan ukishindwa umeshindwa wewe...
 
Ninachokiona mimi kwa Dodoma wafanya biashara wanauza bei ya vitu kwa double price, hiyo inapelekea watu kuamua kuagiza mahitaji ya vitu kutoka DSM. Lakini pia Dodoma hakuna vitu vingi (varities) hivyo still watu wanaenda kuagiza vitu Dar. Nadhani hizo ni miongoni mwa sababu
Kuna factors zinazosababisha kuwepo na double price tofauti na Dar. Kama gharama za uendeshaji ni kubwa, kodi kubwa, kupangisha fremu ni hela nyingi lazima bidhaa ziwe gharama pia.
 
Hao wanaofunga maduka ni wapuuzi. Ni wale watu wenye mihemko wakisikia kitu badala ya kufanya utafiti. Kuna wakati kulikuwa na upepo wa gesi ya Mtwara watu wakakimbilia kujenga hadi mahoteli ya kisasa matokeo yake ni kilio. Dodoma inakuzwa sana ila kiuhalisia hakuna kitu. Kusipokuwepo na mikutano Dom huwa ni ya hovyo. Mfanyabiashara smart hatakiwi kuwa na mihemko ya kijinga.
Dodoma mjini inazidiwa hata na mbagala
 
Hivi wewe...hyo mbona bei ya kawaida sana...kama unafanya biashara lakin...tena unaambiwa ulipie kwa miaka miwil...na ukishindwa tuu siku tatu nyingi inapata mteja harqka sana...NB: location mara nyingi ni towns...lakin kwa laki saba ni kawaida haswa..
Hujawahi fanya biashara ndio maana unaandika hivi. Hata hiyo laki saba uliyosimuliwa unayoona nyingi bado kwa wengine ni ndogo sana. Kuna watu wanalipa milioni 5 kodi ya pango kila mwezi.

Hakuna mfanyabiashara analipa kodi kwa misifa kama unavyotaka kuaminisha watu, kodi inalipwa value for money. Mfanyabiashara huyohuyo anaweza kuwa analipa kodi ya 2M duka fulani, akaja kufungua branch ukataka alipe laki tano akakataa ila akasogea kidogo akaambiwa milioni moja akakubali.

Dodoma haina hadhi ya kulipisha laki saba kwenye fremu kwa mwezi, haina hadhi hiyo.
 
Tatizo watu wanaanzisha biashara wanazo zipenda wao...unakuta mtu anapenda vipodoz bas anaanzisha duka la vipodoz... mtu anapenda kuvaa na kupendeza bas anafungua duka la mavaz...mtu anapenda urembo bas anaanzisha biashara ya urembo...siku zote angalieni mahitaji muhimu yanayo enda tatua matatizo ya jamii...hivi leo hii nisipo vaa cheni...cjui hereni...nk napungukiwa nn? (Hiz ni luxuries goods) ambazo binafsi nitafanya purchasing endapo nina pesa ya ziada...hivi mkiuza vyombo vya majumban hamuoni kama ni basics sana kwa jamii...caz ni bidhaa isiyo kuwa na msimu...wanafunzi wanapangiwa vyuoni watanunua...anae enda anza maisha atanunua...zawadi zq maharus watanunua...sikukuu zote watanunua...kwenye migahawa na hotel watanunua yaan ...fanyeni biashasha inayo tatua matatizo ya jamii kiujumla
 
Hujawahi fanya biashara ndio maana unaandika hivi. Hata hiyo laki saba uliyosimuliwa unayoona nyingi bado kwa wengine ni ndogo sana. Kuna watu wanalipa milioni 5 kodi ya pango kila mwezi.

Hakuna mfanyabiashara analipa kodi kwa misifa kama unavyotaka kuaminisha watu, kodi inalipwa value for money. Mfanyabiashara huyohuyo anaweza kuwa analipa kodi ya 2M duka fulani, akaja kufungua branch ukataka alipe laki tano akakataa ila akasogea kidogo akaambiwa milioni moja akakubali.

Dodoma haina hadhi ya kulipisha laki saba kwenye fremu kwa mwezi, haina hadhi hiyo.
Peleka upuuzi wako huko...kwa hyo umeniajiri?
 
Ninachokiona mimi kwa Dodoma wafanya biashara wanauza bei ya vitu kwa double price, hiyo inapelekea watu kuamua kuagiza mahitaji ya vitu kutoka DSM. Lakini pia Dodoma hakuna vitu vingi (varities) hivyo still watu wanaenda kuagiza vitu Dar. Nadhani hizo ni miongoni mwa sababu
Dodoma ni mji wa gharama utakuja kuvunja rekodi hapo ...Hali ya ule mji utakuwa zaidi ya Dar hawana uzalishaji hata mazao ya kilimo...Kila kitu wanaagiza mkoani Dodoma samaki ni bei sana
 
Back
Top Bottom