DOKEZO Kwanini fremu Dodoma zinafungwa sana na biashara kufa kila uchwao?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Dodoma ni mji wa gharama utakuja kuvunja rekodi hapo ...Hali ya ule mji utakuwa zaidi ya Dar hawana uzalishaji hata mazao ya kilimo...Kila kitu wanaagiza mkoani Dodoma samaki ni bei sana
Yaan mkuu umenichekesha haswa..πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚...kwa hyo wamekuudhi kwenye bei ya samaki... dah saf sana binafsi napenda sana samaki
 
Huo mji utakuwa kama motoni kwa gharama, chukulia ongezeko la watu halafu mji wenyewe hauna uzalishaji hata wa chakula,samaki ,nyama ...Hakuna shughuli yeyote ya maana hata maji ni shida ....Hapo panafaa kuishi mijusi na kenge.

Mji huo watu wajipange kila kitu hela ,hali ya hewa ndio hivyo ni jangwani.
 
Over framing πŸ˜†πŸ˜†

Sasa kama Kila mtu Ali rash kununua maeneo na kujenga fremu au kuanzisha biashara ulitegemea nini?

Hata hivyo Kwa sisi wakulima tunashukuru sana maana tumepata soko jingine la uhakika baada ya Dar.
 
Lakini Kodi gani hizo ambazo ziko Dom pekee?

Labda useme wanaosema hivyo ni wale wametojea Dar ambako biashara nyingi sana ndogo ndogo hazilipi Kodi Wala tozo za Halmashauri Kwa sababu TRA Wana deal na Biashara kubwa kubwa nk

Sasa Mikoani hakuna hivyo vyanzo Vikubwa vkibwa kiasi kwamba TRA na mamlaka zingine wanapiga Kila Chocho kuhakikosha pesa imekusanywa.Hii ndio inaleta tofauti.
 
Mkuu nina ofisi mbili mkoani...moja nalipa laki nane kwa mwez na nyingine nalipa laki tano kwa mwezi...ukibisha njoo inbox nakupa na receipts kabisaa...yaan ukishindwa umeshindwa wewe...
Leta business plan Yako tuione hapa,
 
Dodoma ni mji wa kiserikali si mji wa kibiashara. Ukitaka biashara nenda Dar. Kunawakati eti Dodoma ilikusanya kodi kubwa kuliko dsm, dsm wakalumiwa kwa uzembe. Mimi nilisema hili tukio la uda mfupi tu soon dar itarejea kwnye sehemu yake.
Kwa waliokwenda dodoma kufanya biashara walipaswa kujua kuwa biashara hiyo ni ya muda mfupi tu, piga hela then rudi dsm uendeleza biashara yako halisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…