KERO Kwanini gari moja la mizigo linaweza kuonekana lina uzito tofauti kwenye mizani tofauti ya barabarani?

KERO Kwanini gari moja la mizigo linaweza kuonekana lina uzito tofauti kwenye mizani tofauti ya barabarani?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwa kuwa kila siku magari yanapita katika mizani mbalimbali, kuna changamoto inayowakabili madereva na wamiliki wa magari ya mizigo. Unaweza kupita mizani A, ukaambiwa umezidisha uzito na kupewa faini. Baada ya kulipa, unapanga upya mzigo na kuendelea na safari.

Ukifika mizani B, unapimwa tena na kuambiwa bado umezidisha uzito, hivyo unaombwa kulipa faini nyingine na kupanga tena mzigo. Safari ikiwa bado ni ndefu, unaweza kufika mizani C na kukutana na hali hiyo hiyo.

Swali ni, ikiwa mizani yote ni ya Serikali na inatumia vipimo rasmi, kwa nini gari moja linaweza kuonekana kuwa na uzito tofauti katika mizani mbalimbali?

Hali hii inawaweka katika usumbufu na gharama zaidi madereva na wamiliki wa magari, ambao hulazimika kulipa faini mara kwa mara licha ya kuwa gari hilo hilo limepimwa kwenye mizani nyingine.

Naomba suala hili lifanyiwe uchunguzi ili kubaini usahihi na ulinganifu wa vipimo katika mizani mbalimbali.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Back
Top Bottom