Wakusoma 12
JF-Expert Member
- Jul 3, 2017
- 4,035
- 11,462
Hili suala limekaaje kitaalamu, mfano benki kama NMB ukitaka kutuma pesa kwa mtu kutoka kwenye Akaunti ya benki kwenda kwa namba yake ya simu Cha mtema Kuni utakiona. Je hii ni sawa wakuu? Kwanza gharama za makato hazionekani kabla ya kutuma pesa, ila utakutana nazo tu ukishatuma tayari. Hii si sawa benki kama taasisi muhimu za kiuchumi zijaribu kuwa wawazi katika mchakato mzima wa utumiaji wa huduma zao kwa njia ya simu.