Alikuwepo mtume wa kizigua pale KWAMSISI na aliasisi maajabu yake
kama ifuatavyo;
1. kwamba mjerumani alishindwa kutoza kodi na hata mwingereza pia alishindwa hadimzee mkapa hakutoza kodi ya kichwa lile eneo.
2. Pia waligoma magogo ya mapori yao kusombwa na wakoloni na waliyategea USINGA yale malori yalikuwa yakikanyaga yanakatika spring (Leaf spring) na kubaki hapo na alipotokea mzungu alikumbana na king cobra.
3. Wakati ya vita ya kwanza ya dunia na hata ya pili vijana walikuwa wanachukuliwa kwenda vitani baada ya kupimwa uzito kilo kuanzia 50 na umri kuanzia 18-50 hivyo huyo mtume aliwanywesha KOLOBWA iliyochanywa na LIKANG'AMBWA walipopimwa uzito hakuna aliyefikisha 5Kgs hivyo wengi hawakwenda vitani.
4. Aliamuru jogoo wote wachinjwe kwani walikuwa wakiwika wale wazungu walikuwa wanafata hizo sauti na kuwafikia watu ikumbukwe kipindi hicho kulikuwa hakuna vijiji kila mtu alikuwa anaishi kivyake.
5. Kiukweli mtume KIKWANYULO DIUKIZULA alale mahala pema peponi amen.