Poleni na mizunguuko ya dunia na karibuni
(1) Kwanini hakukua na nabii au mtume MWAFRICA
(2) Nini M/MUNGU ametuficha au kuna baadhi ya mataifa ambayo sio ya AFRICA yametuficha vitu sisi Waafrika
(3) Au hawa manabii na mitume wa sasa wa AFRICA M/MUNGU ametuletea kama malipizi na sisi tupate manabii na mitume kama ni kweli mbona hatuwasikilizi tunawadhalau na wao mbona wanaonekana kama wanaongoza ibada zao kwa tamaa na mambo yasiyo sahihi KIUUNGU
(4) Labda kwa kigezo cha AFRICA tumepewa mali wao wamepewa akili; hapana hata wao mali wanazo tena nyingi kuliko zetu na bado wanakuja kuvuna mali AFRICA
(5) Na mbona wanasema binaadamu wa kwanza mwafrica alikuwa nyani.. na wao hawakuwa nyani mbona hiko kizazi cha nyani cha mwafrica akiendelei au waliwakusanya wale nyani wote waliokuwa wanageuka au wanazaa binadamu wakawaua KUNA HAJA YEYOTE YAKUENDELEA KUTUMIA VITABU(PROTOCOL) AMBAVYO HAVINA MSINGI NA VINA HISTORY MBAYA WALIOPAKAZIWA WAAFRICA..
Mpendwa wenu katika ujenzi wa taifa
Nimejibu hili ila ngoja nikujibu na wewe personally.(Nitajibu kama Mkristu)
Taifa la watu wa Israel kiasili sio watu weusi.Ni weupe ambao wanaasili ya kiarabu.Ingawa palikuwa na mchanganyiko wa watu weusi wachache kutoka Ethiopia(Cush) hawa hawakuwa sehemu ya meseji ya ukombozi wa mwanadamu kama ambavyo tunatambua Mungu alichagua taifa la Israel kiwa taifa teule na kupitia taifa hili watu watamjua yeye na Ukombozi utapatikana.
Kwa mantiki hiyo basi manabii na mitume wote kwa sababu ni descendants wa Yakobo yaani watoto 12 wa Yakobo na kiasili ni weupe hivyo sio kitu cha kushangaza wote wakiwa weupe.
Pia sio kila jina la kitabu la kwenye Biblia linawakilisha Nabii au Mtume kuna vitabu kadhaa vimeandikwa lakini waandishi wake hawayambuliwi kama manabii au watume.Nitakupa mifano kadhaa,
Musa hakuwa nabiii wala mtume
Joshua hakuwa nabii wala mtume
Waamuzi wote wakijumuishwa na Samson hawakuwa manabii wala mitume
Samweli alikuwa Kuhani tu hakuwa nabii wala mtume.
Hata Daudi pamoja na kuandika kwake Zaburi hakuwa nabii wala mtume,wakati wa Daudi ujume wa kinabii alikuwa anaupata Kwa Nathan.
Solomoni hakuwa nabii wala mtume
Hii List ni kubwa sana kwa hiyo tujifunze namna ya kuwatofautisha hawa watu.
Pia sio tu hakuna Nabii au mtume mweusi,hapakuwa hata na nabii mchina au muhindi.
Hoja yako ya mwisho kabisa kuhusu nyani ni ya kuachana nayo hakuna kitu cha namna hiyo.Binadamu alianza kama mtu kwa kuumbwa.