sio wakae wasubiri... kama wamefanya mipango ya kijeshi na kufanya shambulio kama lile.. maana yake its a no brain kuangalia na possible outcome.. wangeweka kwenye mizani impact yake itakuwaje.. na kutoka kwa sponsors wao wangewaambia kuwa tunahitaj msaada wa aina hii ili tuweze ku lunch an attack inayoweza kutoa impact kubwa..
Palestina walitakiwa wabadilike kutokana na dunia... maana yake wangeweza kufanya yafuatayo (nahisi hawafanyi kama wanafanya basi ni wakiwango kidogo)
1. Espionage activities ( upelelezi wa kupandikiza watu ili kuweza kusoma nyendo za adui na kuweza kujua hata weakness zao) hiki kitu maana yake ukiangalia huu mgogoro una miaka zaid ya 30 then palestina walipaswa kuanza kupandikiza watu israel ili kuweza kujua wakiamua ku attack then wana attack ambako kutaweza kuwa cripple Israel . hata israel wakijibu haitakuwa deadly kama ilivyokuwa sasa.. maana yake wangepandikiza watu ambao wanaoa kuolewa na kuishi katikati ya wayahudi hata kuweza kushika kwenye vitengo muhimu wangeweza hata kupandikiza vitu vya mlipuko ikitokea siku wakiamua waki lunch military attack kama walivyofanya.. yaani israel anapigwa kutoka nje and within...sio namna hii kuingia kama mnakwenda kuvamia shopping malls..
2. Millitary training and millitary equipments. hapa hawa jaamaa sababu ya kuwa wako sorrounded na israel ilitakiwa wajikite kutrain watu wao then kuanza kuunda silaha zao wenyewe..
NARUDIA TENA HAYO NILIOSEMA HAPO JUU YALIPASWA KUWA KWENYE "DRAWING BOARD" ya palestina na washirika wake.. mipango ya kimkakati ambapo utekelezaji wake mnaweka hata baada ya miaka 20.
angalia wayahudi na washirika wake walivyofanya kila kitu kimkakati kutoa kuundwa kwa taifa lao hadi saa.. walikuwa kila angle wanaifanya kimakakati..kisiasa ( wamehakikisha wayahudi wameshika ulaya kwenye vitengo muhimu kunakoweza ku influence maamuzi ya nchi husika. kibiashara, kielimu ( Kijeshi na had kiteknolojia)...
kukomboa taifa sio kama unakomboa kijiji.. au mtaa.. historia inaonyesha vita ya nchi kwa nchi kwa ajili ya kukomboa/kushika madaraka ya sio kitu rahis ni vitu ambavyo kuna operation zinazofanyika behind the scene kwa mda mrefu sana hadi watu kuja kutupiana risasi.
angalia Kagame na rwanda mikakati aliiifanyia Uganda.. almost 10 ( from 1987) years before ya ku lunch an attak.
Palestina hawajaweza ku match hata level ya support kwa manaa ya huku dunian majority ya mataifa wana side na isreal. walio upande wa palestina aidha watoe suppot ya kijeshi ndogo au wabakie kupiga kelele za kulaani .
Mkuu unaongea hayo kirahisi kwa sababu ww uko huru ndani ya nchi yako.
Kwa hiyo kipindi unafanya mikakati Hiyo Israel na washirika wake wamekutizama tu?
Kwanza nikwambie kitu kimoja ya kuwa hakuna taifa linalo wasaport Hamas kijeshi zaidi ya Iran tu na penyewe sio sana, silaha nyingi zinazo tumiwa na Hamas ni kujitengenezea wenyewe kuanzia maroketi, risasi na ant tank nadhani wanacho agiza kutoka nje kwa sana ni bunduki na baadhi ya silaha chache.
Mataifa mengine yaliyo baki yana toa fedha kwa mamlaka ya Palestina iliyo West bank na fedha hizo zina pita kwanza kwenye mikono ya Israel na wao ndo wanapanga itumike vipi hiyo hela.
Hiyo mikakati unayo isema imekaa kinadharia sana kuliko uhalisia.
Vita ya ukombozi haijawahi kuwa kama vita nyingine kwa sababu huyo mkoloni hawezi kukupa nafasi ya kujipanga ili uje uhitimishe ukoloni wake, kupigana vita na mkoloni ni sawa na kupambana na serikali yako maana yenyewe ndo anakuwa ana control kila kitu.
ANC ya S.africa ingesubiri ijijenge kwa mikakati uliyo itaja hapo, alafu ndo ianzishe mapambano dhidi ya wakoloni wa makaburu mpaka sasa tunavyo ongea S.africa ingekuwa chini ya makaburu na wangekuwa wamesha kita mizizi ambayo hapo baadae ingekuwa ngumu kuingoa.
Hata Wapalestina kinacho wagharimu sasa ni matokeo yao ya kutumia miaka mingi sana kwenye mazungumzo kupitia PLO na Israel badala ya shinikizo la silaha.
Nakuhakikishia Israel ingekuwa na shinikizo kutoka kwa makundi yenye silaha kama analo lipata sasa hivi kutoka kwa hamas toka mwaka 1967 Israel ingekuwa ilisha kubali kuanzishwa kwa taifa huru la palestina.
Hivi unajua chanzo cha Israel kujiondoa kwenye ukanda wa gaza mwaka 2005?
Ni kwa sababu ya makundi yenye silaha kuweka shinikizo kwa kufanya mashambulizi ya kushutukiza dhidi ya wanajeshi wa Israel na walowezi walio kuwa ndani ya gaza ina maana Israel ilijiondoa ndani ya gaza baada ya kuona ni eneo hatari kwa wanajeshi na raia wake wa kilowezi , sasa hali kama hiyo walitakiwa waipitie waisrael wanao ishi ndani eneo lote la ardhi za wapalestina yaani kila ardhi ya wapalestina watakayo ikalia iwe chungu kwao.
Tena kama huyo Mohamud Abas ni kikwazo kikubwa sana kwa wapalestina kupata haki zao maana anawafanya Wayahudi walirax ndani ya ardhi za wapalestina kwa kujifanya ni mpenda amani kwa kuamini eti Israel itakuja kumkabidhi nchi kwa maneno tu.
Kila mwaka huko west bank maelfu ya wapalestina wanafungwa jera,kuuawa na wengine kufukuzwa kwenye ardhi zao yeye ametizama tu ,na mbaya zaidi anashirikiana na Israeli kudhibiti organization wapalestina zenye silaha zinazo endesha mapambano ndani ya eneo hilo.
Ebu mkuu jiulize maswali machache tu tena rahisi hivi unadhani Usoviet ingeondoka nchini Afghanistan bila shinikizo la silaha kutok kwa mujahidina?
Au unafikiri bila shinikizo la Talban Marekani ingekuwa hata na mpango wa kijiondoa Afghanistan?