Kwanini hamtaki kujibu haya maswali kwenye Biblia?

ts9_dna

Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
33
Reaction score
121
Habari zenu,

Naombeni majibu ya haya maswali kwenye maneno ya Biblia:

"Ukisoma mwanzo unaambiwa Adam na Hawa walimzaa Kaini na Habili, baadaye Kaini alimuua nduguye Habili. Baada ya hiyo hali Mungu akamfukuza Kaini (Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana akakaa katika nchi ya Nodi mbele ya Edeni). Kaini akamjua mkewe naye akapata mimba akamzaa Henoko."


Swali liko hapo; Huyo mke wa Kaini alitoka wapi wakati Mungu alikuwa ameumba watu wawili tu na walizaa watoto wawili na kati ya hao mmoja alikuwa amefariki? Huyo mke alitoka wapi, embu tupeni majibu?
 
Idadai ya Waisrael wakati wanatoka utumwani Misri kwenda Nchi ya Kaanani, walikuwa watu laki 6, bila kuhesabu wanawake na watoto
Yesu aliwalisha kwa samaki mmoja na mikate mitano watu elfu tano, bila kujali wanawake na watoto
Sijui kama nitakuwa nimejibu swali lako
 
hii itazua taharuki

ila nakumbuka mwalimu wangu wa bible knowledge kasomea theology alikua anatuambia kuna nadharia kwamba adam na hawa walikua na watoto wengine wa kike, lakini tamaduni za kipindi kile watoto wa kike walikua hawahesabiwi ndo maana hawajazungumziwa....

hata mtoto wa yakobo, dinah hakuzungumziwa sana kama mnakumbuka na wala hawakusema kama alipewa ardhi kule kwenye nchi ya ahadi

kiufupi bibilia ya agano la kale inakandamiza sana wanawake

lakini uhalisia ni kwamba kuanzia mwanzo 1-11 ni hadithi za kutungwa, sema hii itakua ngumu kwa wanaoamini kuelewa
 
Biblia ni hadithi za kutungwa sawa na Hekaya za Abunuwasi, Hadithi za Alfu Lela ulela au riwaya za kusisimua za joka la Mdimu.

Bible is a Fairytale, Mythology, Fictional book.
 
Kwahiyo watoto wa Adamu wa kike walizaa na Kaini?? Kama hivyo kwann hairusiwi kuzaa na ndugu yako
 
Eti wanyama wote Waliingia wawili wawili kwenywe safina , hii story na ya uwanja wa ngoma ya ngozi ya ng'ombe ya juma na uledi inatofauti gani?
 
Adam na Eva waliiwahi kuzaa watoto wa kike pia, ila hawakutajwa kwenye Biblia na mmoja wao ndiyo huyu aliyekuja kuolewa na Kaini. Walikuwa wanaruhusiwa kuoana mtu na dada yake
Kwanini hawakuzungumziwa na ilikuwaje wakakatazwa kuoana ? Wewe umejuaje kama Adam na hawa walikuwa na watoto wa kike Imeandikwa wapi leta jibu
 
Kuna wengne wanadai bustani ya edeni ilikua ni maabara ya kufanya modification ya mtu, kutoka viumbe wa sayari za mbali , ndio wakatuletea hawa ngozi nyeupe wote , ila mtu ambae ni mweusi alikuwepo tu ,hao viumbe ni wana wa adamu, na ulikua ni mpango wa hao viumbe kuitawala dunia kupitia hao wanadamu ( weupe) dhidi yetu sisi watu , hizi ni dhana ambazo bado zipo kama story ila zinafkirisha coz inaaminika mtu mweusi kaishi miaka mingi duniani kuliko mweupe .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…