Kwanini hamtaki kujibu haya maswali kwenye Biblia?

Kwanini hamtaki kujibu haya maswali kwenye Biblia?

Idadai ya Waisrael wakati wanatoka utumwani Misri kwenda Nchi ya Kaanani, walikuwa watu laki 6, bila kuhesabu wanawake na watoto
Yesu aliwalisha kwa samaki mmoja na mikate mitano watu elfu tano, bila kujali wanawake na watoto
Sijui kama nitakuwa nimejibu swali lako
Swali linahusu kazini na mkewe, na sio Yesu
 
Habari zenu,

Naombeni majibu ya haya maswali kwenye maneno ya Biblia.

Ukisoma mwanzo unaambiwa adam na Hawa walimzaa kaini na Habili baadaye kaini alimuua nduguye Habili baada ya hiyo hali Mungu akamfukuza Kaini ("kaini akatoka mbele za uso wa Bwana akakaa katika nchi ya Nodi mbele ya Edeni.

Kaini akamjua mkewe naye akapata mimba akamzaa henoko") swali liko hapo HUYO MKE WA KAINI ALITOKA WAPI NA KATI MUNGU ALIKUWA AMEUMBA WATU WAWILI TU NA WALIZAA WATOTO WAWILI NA KAT YA HAO MMOJA ALIKUWA ASHAKUFA? HUYO MKE ALITOKA WAPI EM TUPENI MAJIBU
Biblia inajichanganya kwenye Adam kubwa mtu wa kwanza,maana Inasema baada ya Adam kufukuzwa edeni,huko walikoenda wakakuta watu,sishangai wazungu kukataa dini,ukiichimba Imani ya kikiristo sharti uone kizunguzungu
 
hii itazua taharuki

ila nakumbuka mwalimu wangu wa bible knowledge kasomea theology alikua anatuambia kuna nadharia kwamba adam na hawa walikua na watoto wengine wa kike, lakini tamaduni za kipindi kile watoto wa kike walikua hawahesabiwi ndo maana hawajazungumziwa....

hata mtoto wa yakobo, dinah hakuzungumziwa sana kama mnakumbuka na wala hawakusema kama alipewa ardhi kule kwenye nchi ya ahadi

kiufupi bibilia ya agano la kale inakandamiza sana wanawake

lakini uhalisia ni kwamba kuanzia mwanzo 1-8 ni hadithi za kutungwa, sema hii itakua ngumu kwa wanaoamini kuelewa
Hakuna cha kutunga. Kila kitu ni Halisia. Mwalimu wa wa theology alikueleza ukweli. Biblia katika mwanzo 5:1-2 inasema "Adamu alizaa wana wa kike na kiume". Mwanzo 6:1-2 pia inasema Wana wa "Wanadamu waliopoongezeka juu ya uso wa nchi, wana wa Mungu wakijitwalia wanawake miongoni mwao na wakazaa nao watoto"

Umeeleza vizuri na mwalimu wa theology alikueleza vizuri. Hawakuwa wanahesabu wanawake na pia wasingeweza kuandika majina ya watu wote wawe Bible Characters lakini baadhi ya maandiko nje ya Biblia"Abrahamic Texts" kama 'The book of Jubilee" kinaeleza mke wa Kaini alikuwa ni mmoja wa Dada yake yaani pacha wake aliyekuwa anaitwa "AWAN" na pia ndio chanzo cha kifo cha Habili kwani walimgombea Dada yao.
 
Habari zenu,

Naombeni majibu ya haya maswali kwenye maneno ya Biblia.

Ukisoma mwanzo unaambiwa adam na Hawa walimzaa kaini na Habili baadaye kaini alimuua nduguye Habili baada ya hiyo hali Mungu akamfukuza Kaini ("kaini akatoka mbele za uso wa Bwana akakaa katika nchi ya Nodi mbele ya Edeni.

Kaini akamjua mkewe naye akapata mimba akamzaa henoko") swali liko hapo HUYO MKE WA KAINI ALITOKA WAPI NA KATI MUNGU ALIKUWA AMEUMBA WATU WAWILI TU NA WALIZAA WATOTO WAWILI NA KAT YA HAO MMOJA ALIKUWA ASHAKUFA? HUYO MKE ALITOKA WAPI EM TUPENI MAJIBU
Biblia haielezi umri wa Kaini wakati alipomuua ndugu yake Habili (Mwanzo 4:8). Kwa kuwa wote walikuwa wakulima, lazima wawe walikuwa watu wazima, hata pengine na jamii zao.

Adam na Hawa walikuwa wamepata watoto wengine mbali na Kaini na Habili wakati Habili alipouawa. Walipata wengi wengine baadaye mwanzo 5:4.

Ile hali ya Kaini kuhofu sana juu ya usalama wake baada ya kumuua Habili mwanzo 4:14 inathibitisha kulikuwako na watoto wengi wengine pia na wajukuu na hata vilembwe wa Adamu na Hawa.

Kwa kuwa Adamu na Hawa walikuwa wanadamu wa kwanza duniani, watoto wao hawakuwa na lengine ila kuoana.

Mungu hakukataza kuoana kwa jinsi hii mapema mpaka dunia ilipokuwa na watu wakutisha ndipo akakataza aina hii ya kuoana mambo ya walawi 18:6-18.

Sababu ya madhara ya ndoa za kaka na dada ni kwamba kama kila mmoja wao alikuwa na hali Fulani ya kilema ndani yaoya kurithi basi atakayezaliwa atakuwa mwenye kurithi kutoka kwa wote wazazi wawili, hivyo basi kuwa hali mbaya zaidi kuliko waliomzaa
 
Ili uelewe unahitajika maarifa ya kiroho sio kukurupuka...
 
Kuna mengi kwenye biblia hajaamdikwa maana yangeandikwa yote yasingetosha kujaa hata kwa karatasi zote zilizopo hata leo.
Uamuzi ni wako kuamini au kuona stori za Abunuwasi nk
 
Biblia katika mwanzo 5:1-2 inasema "Adamu alizaa wana wa kike na kiume". Mwanzo 6:1-2 pia inasema Wana wa "Wanadamu waliopoongezeka juu ya uso wa nchi, wana wa Mungu wakijitwalia wanawake miongoni mwao na wakazaa nao watoto"

Wakati wa zamani, tamaduni za kiebrania hawakuwa wanahesabu wanawake na pia wasingeweza kuandika majina ya watu wote wawe "Bible Characters" kwani Biblia sio kitabu cha history kinaeleza kuhusu uumbaji, Anguko la Mwanadamu, Mpango wa ukombozi wa mwandamu na "lineage kati ya Uzao wa nyoka na uzao wa Mwanamke" pia namna gani mwanadamu anatakiwa kuishi maisha matakatifu ili siku 1 waurithi uzima wa milele.

Lakini baadhi ya maandiko nje ya Biblia"Abrahamic Texts" kama 'The book of Jubilee" kinaeleza mke wa Kaini alikuwa ni mmoja wa Dada yake yaani pacha wake aliyekuwa anaitwa "AWAN" na pia ndio chanzo cha kifo cha Habili kwani walimgombea Dada yao.
 
Biblia ni hadithi za kutungwa sawa na Hekaya za Abunuwasi au riwaya za kusisimua za joka la Mdimu.

Bible is a Fairytale, Mythology, Fictional book.
Mzee, vipi kuhusu Quran nayo ni ya kutunga ama vipi
 
Wewe umeyajuaje kama hayakuandikwa??
Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.
And there are also many other things which Jesus did, the which, if they should be written every one, I suppose that even the world itself could not contain the books that should be written. Amen.

Yohana 21:25
 
Back
Top Bottom