Biblia huaga unasoma mwenyewe au unasomewa? Sina Biblia hapa, lakini kama kweli hiyo sura ulioinukuu kama ulisoma mwenyewe then siamini kama ingekupa shida kuelewa. Kama ulisoma utagundua kwamba the idea ya kuumba alicho kiumba, aliitamka hata kabla hajafanya hivo. Kabla ya kumuumba Hawa, ipo sehemu imeandikwa, "mtu mke na mtu mume aliwaumba...." cause alitaka kazi ya uumbaji isifanywe na yeye tena, alifanya delegation kwa viumbe wake including binadamu. Soma with positive mind, ukisoma kwa kutaka kukosoa utakutana na vingi tu.
Let me add this as well, coming from my own testimony. Mwaka 1994 kupitia tape za radio cassettes za wakati huo, nilimsikia sheikh mazinge na "askofu" mwaipopo wakisema hivi, "1Wakorinto 15:15 kwamba naamu na sisi tumekua mashahidi wa uongo kwa kumshuhudia Mungu kwamba alimfufua yesu ambaye HAKUFA" Nilistuka sana, kwamba kumbe Yesu hakufa? Na wamesoma kwenye Biblia? Kumbe pasaka sio sherehe ya ukweli? Mimi sikua najua chochote kuhusu Biblia but miezi kadhaa baadae nikakutana na wasoma Biblia, nilitaka kujiridhisha kama hilo andiko lipo na linasema hivo cause niliukariri ule mstari...., baada kusoma kutoka juu hadi baada ya huo mstari wa 15 nilishangaa sana, kwamba inakuaje kiongozi wa dini anakua muongo namna hi? Nilichukia hadi na dini yake. Nakushauri na wewe, usije kua kama kina Mazinge, wanahubiri kwa kutumia uongo ili kumpendeza mungu wao, mungu anaependezwa na uongo nadhani sio mungu wa kweli, huyo atakua shetani