Kwanini Hayati Dkt Magufuli aliichukia sana Kaskazini lakini sasa Rais Samia anaipenda sana hii Kanda?

Ndugu una roho ya husuda haijapata tokea. Kwanza mambo mengi anayosema Rais Samia kafanya ni ya uongo mfano mradi wa maji unaojengwa kwa ajili ya Arusha mradi huu uliasisiwa tangu enzi za Kikwete na ni kwa mkopo wa AfDB 560 billion. Wala sii Rais Magufuli wala sii Mama Samia(Rais). Uache kuwadanganya watanzania. Kuzinduliwa Royal tour ARUSHA sii kwa upendeleo bali Arusha imekuwa center ya utalii siku nyingi na unajua asingeweza kuzindulia Burigi hata kidogo. Hakuna issue ya upinzania hapa kwani wapinzani nao ni watanzania naona unataka leta mambo ya mwendazake na kuwapachika marais wengine waliopita kuwa waliwachukia watu wa kaskazini, mbona walifanya nao kazi bila ubaguzi kama wa mwendazake. Hoja mfu kabisa hii.
 
Taarifa:
Upinzani.
Hili neno linavyotumika katika mada hii, pamoja na neno "mchagga" ni ya kuleta taaharuki na utenganisho katika Jamii ya Mtanzania na makabila mengine.

Mleta mada amejikita kuonyesha kuwa neno Upinzani ni hasi na ametumia mbwembe nyingi kuonyesha 'upinzani' huo kuwa lina Ukabila! Na amelenga Kaskazini.

Kama hayo juu ni uwongo, jiulize kwanini hakuweka Kabila la Raisi Samia Suluhu Hassan? Kulikuwa na Ulazima gani wa kuandika "Mchagga" kila anampomtaja Mh. Mrema? Mrema alikuwa mpinzani au alikuwa Kiongozi wa chama cha Siasa?

Kama kweli mleta mada alikuwa na lengo zuri, kutumia "Mchagga" na "Upinzani" katika maudhui yake aweke bayana na kabila la Mh. Raisi Samia Suluhu Hassan.

Zaidi ya hapo Uzi huu ni kama mada nyingine nyingi zinazotaka kuleta Uhasama hasi katika Jamii na Siasa baina ya Wananchi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Mleta mada na genge lake ni wakusuritishwa na wafikishwe mbele ya vyombo husika vya Usalama wa Nchi hii.

Karibuni JF. Muache tabia na desturi zenu Hasi, zenye Uhasama hasi katika Jamii ya Watanzania.

Hakuna Wapinzani bali wachangiaji wa maendeleo ya Nchi na mustakhabali wake. Vyama vya Siasa sio "Upinzani" wa nchi bali ni wakosoaji wa Sera za Chama tawala.

Aluta Continua.
 
Madai yako ni ya uwongo Kwani Hayati Raisi John Pombe Magufuli hakuepo madarakani kwa miaka 20.
 
Usipende kubishana na ukweli.
Hakuna rais mkabila na wa upendelea kwao kama Magufuli.
 
Kanda ya kaskazini inategemea kupokea wageni wengi .

Nadhani tumeelewana ..niishie hapa
 
CCM ya kina Kinana hii, imejaa upuuzi tu hamna hata wasomi wa kujenga hoja za kueleweka. Majungu na fitna. CCM sio baba yenu wala mama yenu, tutawatoa upepo 2025.
Uongozi ni character, msimamo wa Mangula sio cheo ile kaliba. Yule ndio alivyoumbwa vile na Kinana haupo hivo.
Katibu wa CCM unatembea na helikopta kwenda kuongea na wananchi vijijini kweli? Mangula hawezi kufanya hivyo.
Hii nchi vita itatokea na sisi tunajua tutakuwa upande upi.
 
Rais Samia ndio mtu Sahihi 2025 kama kweli tunahitaji na sisi wa kaskazini kutambulika kama WATANZANIA,

Hii tupende tusipende, Ila tukiendelea na ma-CHADEMA yetu tutabaki wa hivi hivi tu,
Tutampa kura,
 
Kuanzia Mkapa pamoja na kuwa alioa mchaga, Kikwete na Magufuli waliipa mgongo hasa Kilimanjaro.

Nyerere, Mwinyi na sasa Samia anapeleka maendeleo kila sehemu bila kubagua!!

Samia kwa kipindi kifupi sana ameisaidia sana kaskazini hasa Arusha!!
 
Sisi wakaskazini hatuitaji shobo za serikalini Wala Nini ..sisi tunapambana kivyetu vyetu.
Tanzania hizi bila kaskazini ni bure.
 
Hata kanda ya ziwa alisahau isipokuwa Chato
 
Ku plan mradi fulani halafu usipeleke pesa ni sawa haujafanya chochote! Huu mradi wa maji unawezekana ulikuwa ni mpango tangu awamu ya Kikwete lakini kama Samia ndo amepeleka pesa kwa asilimia 100 anafaa kupongezwa sana kwenye ili na sio awamu ya nne!!

Biashara ya utalii Arusha hata kabla ya Covid ilianza kufanya vibaya. Yule aliyekuwa DC wa hai - anayejisahidia kwenye ndoo sasa hivi - alichangia sana kuiharibu. Ulisikia alikuwa hakivamia mahoteli ya kitalii usiku na kuimiza wamiliki kutoa rushwa. Mahoteli makubwa kama Impala yalianza kufa, bureau de change zilifungwa. Jitihada nyingi zilitumika kuamishia wanyama mkoa mwingine.

Samia ameonyesha nia za kuinyanyua tena hii sekta ya utalii kupitia Royal tour na miradi aliyopeka Arusha. Lakini Changamoto bado zipo, waliopo chini yake waanze kufikiria nje ya boksi!!!!
 
Riz moko alisema Hadi dunia iishe haitokaa itokee Rais kutoka kaskazini,wakati huo mamvi alikuwa na mafuriko balaa
 
Nampenda sana Rais Samia
 
Ukweli wanao wananchi tembelea wananchi wa kawaidahujaniambia utaupata ukweli. Pia watanzania ubaguzi wa Kanda NI wa kukemewa sio wa kushabikia Kama tunataka kubaki Kama taifa. Tuombe maendeleo yetu hayahitaji ukanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…