Hili jamaa sijui limeolewa na muarabu?? Kila siku linakeshaga kuwasifia humu
Kwahiyo unataka niwachukie ama kusapoti haters wanaowazunguka!!
Slaverly of the mind....Afadhali ile minyororo ya miguuni waliyotufunga ya kutuuza kuliko hii minyororo ya akili waliotuachia kupitia dini yao.
Unazungumzia minyororo ipi hiyo? Unafuata zile picha za kuchorwa vitabuni ikionyesha waafrika wakiteswa!! Bado tu tuna mawazo ya namna hiyo!!!
Hebu lete picha halisi inayoonyesha waarabu wakifanya huo ushenzi mliokaririshwa!!!
Mkuu mimi ni muislamu na ningependa uweke angalau ushahidi wa hadithi kuthibitisha maneno yako hasa hapo kwenye "waarabu ni ndugu zetu katika imani"
Lini uislamu uliangalia ethnicity?
WAISILAMU WOTE NI NDUGU
Aya katika Qur'an tukufu inasema👇🏽
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ
Al-Hujurat 49:10
Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe.
KATIKA maisha yake, mwanadamu analazimika kuwa na mahusiano baina yake na watu wengine. Mahusiano hayo kwa lugha rahisi yanaitiwa Udugu. Udugu umegawanyika katika sehemu nne. Udugu wa kuzaliwa (damu), udugu wa ndoa, udugu wa ubinadamu na udugu wa imani.
Udugu wa damu una mipaka yake, ndoa hata ubinadamu pia una mipiaka yake. Lakini udugu wenye nguvu na unaotiliwa mkazo sana na Uislamu ni udugu wa imani. Udugu huu ni ule unaotokana na watu kuwa na imani moja.
Udugu huu ndio ambao IshaAllah tutautizama katika mada yetu hii. Allah (s.w.) anatupa khabari katika Qur'an tukufu sura ya 49:10: "
Kwa hakika Waislamu wote ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu (msipuuze jambo la kupatanisha) ili mrehemewe".
Kwa mujibu wa aya hii tunafahamishwa kuwa Waislamu wote ni ndugu moja, ummah mmoja na ni sawa na mwili mmoja ambao kidole kimoja tu kikipata maumivu mwili wote unakosa raha na amani.
Vile vile aya hii inatuonesha kuwa Uislamu hauna mipaka ya jiografia ya mtaa kwa mtaa, wilaya kwa wilaya, mkoa kwa mkoa, nchi kwa nchi na kadhalika. Bali Waislamu wote kokote waliko ni ndugu moja na ummah mmoja ni sawa na ndugu wa baba mmoja na mama mmoja au hata zaidi ya hapo, tatizo la mmoja wao linakuwa ni tatizo la Waislamu wote kote duniani bila kujali tofauti za kabila, rangi, hadhi nafasi na kadhalika kama tufahamishavyo katika Qur'an 49:13:
"
Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanamume (mmoja, Adamu) na yule mwanamke (mmoja, Hawwa). Na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbalimbali) ili mjuane. Hakika ahishimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mungu zaidi katika nyinyi..." (49:13)
Kama nilivyokwishaeleza hapo juu, kuwa Uislamu ni ummah mmoja na hatuna mipaka ya jiografia. Ummah huu mmoja wa Kiislamu unaitwa "Ummat l-Islam" yaani Ummah wa Kiislamu.
Mipaka hii ya kijiografia tunayoiona leo iliwekwa na wakoloni kwa lengo la kutaka kututawala kwa kuanza kutugawa, ili kurahisisha utawala wao.
Waislamu kote ulimwenguni ni sawa na mwili mmoja, hivyo raha ya Muislamu mmoja ni raha ya wote na tatizo la Muislamu mmoja ni tatizo la wote.
Yanayotokea leo ulimwenguni dhidi ya Uislamu kama vile Chechnya, Bosnia, Cossovo, Kashmir, Afghanistan, Palestina na kadhalika yanatakiwa yamguse kila Muislamu popote alipo hapa duniani na tatizo hilo lishughulikishe hasa vichwa vya Waislamu na kuangalia jinsi ya kulipatia ufumbuzi stahiki