Kwanini Hospitali ya St. Benedict, Ndanda, Mtwara huuliza wateja dini zao?

kwa pwani watu wa dini zote washachafuka na usodoma huo, hapo sitakubaliana na wewe though maeneo kama tanga na zanzibar ni extreme kwa wanawake karibia wote.ila kwa kuishi na waislam kwa miaka mingi, nimekuja kugundua kuwa hawataki kabisa hata umguse tu mke wake, sembuse akienda hospitali ashikwe na kupimwa kwa vidole, ashikwe kalio achomwe sindano, n.k. na wanawake wengi wa maeneo hayo ukikutana nao wanavaa kwa kujifunika utafikiri wa dini fulani kumbe sio ni utamaduni wa maeneo hayo tu.
 

Ile ni hospitali inayomilikiwa na taasisi kidini. Hivyo, ni dhahili inapata ufadhili kutoka kwa wafadhili na wabia mbalimbali. Hawa wafadhili/wabia huwa wana masharti kadhaa ikiwemo kutokuwa na upendeleo wa kidini katika kutoa ajira na kuwahudumia wateja. Na lazima kuwe na uthibitisho kuhusu hili.
Sasa; kwa upande wa ajira ni rahisi kupata hizo taarifa maana unapoajiriwa kwenye datasheet kipengele cha dini yako kinakuwepo hivyo ni rahisi kupata uwiano.

Upande wa wateja sio rahisi kuthibitisha hilo. Ndio maana hizo taarifa zinaombwa ili mwishoni kuthibitisha watu wote wanahudumiwa bila kigezo cha dini.

Hata hivyo, hapa nimetumia mfano wa hospitali tofauti na hiyo ambayo taarifa za dini ya mgonjwa zinaombwa kwa lengo hilo. Sina uhakika kama na hospitali hii inaziomba kwa lengo linalofanana na hili.

Asante
 
Hizo taasis za dini zingine bado zinajiendesha kwa michango ya waumini wao mf kuna seminaries kibao waumini wanachangishwa pengine lengo ni kuwatambua ili wapate discounts wakipatiwa huduma.

BTW:Wakati wa ujenzi wa Chuo cha SAUT kulikuwa na Michango na Harambee za kufa mtu parokia zote jimbo Kuu katoliki la Mwanza miaka hiyo 2001 nafikiri wao pia walihitaji utaratibu wa kuwatambua walioshiriki ujenzi ili kuwapunguzia ada walau mtoto mmoja.

Wawe wanatoa IDs kama za wachangia damu ili wapate vipaumbele kwenye huduma.
 
hii hoja sio nzito. hospitali za wakatoliki kama ile hawawajibiki kwa wafadhili kihivyo, na hata wafadhili wangekuwepo wangependa zaidi waislam watibiwe kwa sababu ndio imekuwa njia ya kuiwaita watu kwenye dini yao tangu wamisionari walipokuja hapa nchini miaka hiyo. labda kama wangependa watu wengi wanaotibiwa wajulikane ni waislam ili wafadhili (kama kweli wapo) wawape pesa kwa sababu wafadhili wangependa kuhudumia zaidi hao walio nje ya dini ili kuwavuta waingie ndani. ila napenda kuwahakikishia waislam kuwa, hao wakatoliki wasingejenga hospitali kuwahudumia ninyi kama wanawaachukia, never, hawawachukii.
 
Sasa hii hospital umeambiwa ya wakristo
 
Kuna watu hawana dini
Unajibu sina dini hakuna shida.
Yeye atajua kwenye mfumo ajaze nini.
Hiyo hospital imeanzishwa na wajerumani wa Benedictine Fathers wakati wa ukoloni enzi hizo wateja wao karibu 70 ni wapagani.
Unadhani hawakutibiwa?
 
Kwani umezuiwa kutukana,we tukana tu
 

Unajibu sina dini hakuna shida.
Yeye atajua kwenye mfumo ajaze nini.
Hiyo hospital imeanzishwa na wajerumani wa Benedictine Fathers wakati wa ukoloni enzi hizo wateja wao karibu 70 ni wapagani.
Unadhani hawakutibiwa?
Lengo lao hasa ni nini kama sio racism?
 
Lengo lao hasa ni nini kama sio racism?
Kwanini unahitimisha udini wakati hujui lengo lao?
Ukijua utakuwa na nafasi nzuri kuhukumu.
Unajuaje kama lengo ni kutoa zile sakramenti ya watu walio karibia kufa (wagonjwa) endapo magonjwa akiwa kwenye hali hiyo?
Unajuaje labda wanatembelea wakatoliki wenzao kuwapa sakramenti za kitubio na ibada zingine wodini?
Hakuna muislam anaye katazwa au lazimishwa kwenda pale.

Punguzeni malalamiko,kujihisi, inferiority complex na prejudice!
 
Wanauliza ili kama utatumia jeneza au sanda kuondosha usumbufu.
 
Me mwenyewe mkristo ila sion logic yake na me nkienda kwenye hiyo hospital ntawauliza maswali ya kutaka kuelewa unless otherwise mnasema sina dini. Mtu anahitaji Panadol we unataka kujua dini yake ufanye nayo nini ? Unadhani prejudice ilianzaje huko mashariki ya mbali ? Itafika muda wa mgonjwa kuwekewa drip mtu anaenda ukimpa mtu sacrament sijui ya kitubio we huoni kama hapo kuna controversy inatengenezewa?.. kwanza MUNGU hana dini kama ishue ya dini inahusiana na MUNGU. Kimsingi hapo wanatakiwa wacut the crap waache kuuliza mambo ya dini watibu watu wote sawaaa
 
Mkuu huwezi kujibu bila kutukana ?
 
Sijatafsiri udini mkuu. Nashukuru kwa jibu lako. Je waonaje sensa ya nchi ikahusisha dini ili kusaidia kila mwenye lengo la kukusanya taarifa za kidemografia kwakuwa imeonekana hilo ni jambo muhimu.
Kwa maelezo yako tu unaonekana una lengo la kuleta udini hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…