Kwanini huyu bondia Mtanzania aliyeshinda Uingereza anajiita Hassan Mwakinyo?

Kwanini huyu bondia Mtanzania aliyeshinda Uingereza anajiita Hassan Mwakinyo?

Wanandugu leo katika pita pita zangu nikasema ngoja niangalie boxing records za huyu ndugu yetu Hassan Mwakinyo lakini cha ajabu nikakuta anaitwa Halfan Hythan Hamza, sasa nimeshindwa kuelewa hilo jina la Hassan Mwakinyo amelitolea wapi? Au anatumia cheti cha mtu maana anadai ana miaka 23 lakini ukimuangalia sura inaonesha kabisa yupo kwenye 30+ huko.


Ila kingine ninachomkubali huyu ninja amewachana wale wote wanaojifanya wanamjua jua na kujifanya watu wake wa karibu wakati alipata shida hata namna kusafiri ili akapambane aliwekewa kila aina ya vigingi lakini Mungu akamsaidia akafanikisha safari na akaenda kufanya alichokifuata kule Uingereza.


Miongoni mwa watu waliojifanya wanamjua jua sana Mwakinyo ni pamoja na waziri Mwakyembe ambaye bila aibu anadai kuwa wanafahamiana siku nyingi jambo ambalo sio la kweli bali ni unafiki mtupu.

Hassan atapanda tena ulingoni mwezi october kupambana na Wanik Awdijan raia wa Ujerumani.



Swali linabaki pale pale jina la Hassan Mwakinyo limetoka wapi wakati jina lake ni Halfan Hamza , kama angekuwa na jina la kikristo kidogo isingekuwa kuwa tabu maana tungejua huenda amebadili dini na kuwa muislamu , sasa shida ni kwamba majina yote ni ya kiislamu, ambao mnamjua huyu bondia embu toleeni ufafanuzi kidogo suala hili.View attachment 866189View attachment 866190
Mshaanza kumletea uchawi....wabongo bana uchawi uchawi tuuu😬 haya sasa tuseme ana miaka 35 na anatumia cheti cha mtu then what u gonna do?
 
Ukitaka kujua wabongo roho mbaya subiri ufanikiwe, kumbavuu sana.....
 
Labda kagushi na ngumi

Hata angejiita uchi kwetu sisi haimake any difference so long as anashinda kwa KO
 
Ni kawaida kwa wanamichezo kuwa na Majina ya PASSPORT na Majina ya Media. Arsenal waliwahi kuwa na mtu anaitwa GERVINHO lakini Passport yake ilisomeka: GERVAIS LOMBE YAO KOASSI, jamaa alifanana sana sura na K. R. Mulla wa TMK WANAUME!
 
Back
Top Bottom