Kwanini huyu Msanii aliruhusiwa kuingia Ubalozini?

Umeongea kweli, kuimba mapenzi na matusi...ni sanaa nzuri maana ametengeneza ajira na amekuza sanaa wengine wameingia kuimba matusi na mapenzi. Ila wote si sawa...Yale majizi ya suti yanalindwa na chama Cha mapinduzi, ndicho mmekipa kiongoze serikali haya ndio matokeo..hakiwezi waadabisha wezi badala yake kinawakingia kifua wasisumbuliwe
 

Free mind
 
Watu kibao wanajipatia riziki zao na familia zao kupitia huyo jamaa so mavazi hayana issue.
 
Samahani sana ndugu zangu, naomba tu ufafanuzi...je, ndani ya bunge letu, mavazi haya yanaruhusiwa?
 
Tuache kutetea ujinga, na tupunguze ujuaji. Kwa hiyo mtu akibeba jembe akiwa kavaa suti na kwenda shamba hatutamshangaa! Hivi tumekuwaje? Angekutana na Mh. Balozi huko mgahawani na hayo mavazi wala isingekuwa shida.
 
Labda anatoa ujumbe kuwa hiyo ndio thamani halisi ya hiyo ofisi, kwamba Haina Ukuu huo ambao wengi mnafikiria upo.
 
Hii ndio athari ya kwanza kukosa elimu ya etiquettes na pili kutumia punga kama designer anaekuvalisha.

Kwa level aliyofikia Diamond kuna baadhi ya mambo inapaswa ajifunze ikiwemo aina ya mavazi kwa mlingano wa eneo husika.

Sasa yeye kila kitu anachukulia usela kutokujua kuna dress code ya sehemu zenye hadhi.
 
Tuache kutetea ujinga, na tupunguze ujuaji. Kwa hiyo mtu akibeba jembe akiwa kavaa suti na kwenda shamba hatutamshangaa! Hivi tumekuwaje? Angekutana na Mh. Balozi huko mgahawani na hayo mavazi wala isingekuwa shida.
Wabongo wanaa sana. Wanaangalia ushabiki wake kwa msaani badala ya kumwambia ukweli.
 
Kwani huyo msanii anaye
jadiliwa humu ndio nani huko Daslam?

Mleta mada naona hukuweka japo jina lake ili na sisi wa huku vijijini tumjue!
 
Sasa kizazi cha saa hi i ni kutembeanusu uchi tusilalamike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…