Kwanini ishara, maajabu na miujiza mikubwa inafanywa na watu wanaoiamini Biblia tu?

Kwanini ishara, maajabu na miujiza mikubwa inafanywa na watu wanaoiamini Biblia tu?

Kwanini?

Kama huo sio ushahidi kwamba Biblia ni Neno la Mungu, nitajie sababu yako wewe...
Kwanini ishara, maajabu na miujiza mikubwa inafanywa na watu wanaoiamini Biblia tu?
Naomba nijikite hapa kwenye bold 👆

Ishara na maajabu

Matendo Mitume 5:1-11

Mungu NI maskini Sana mpaka kutegemea Mali za anania ?

Haya NI maajabu na ishara.

Asante Sana Setfree Kwa kunielimisha
 
Miujiza ni upumbafu kwa wapumbafu pekee.Mtu anaponya na kufufua wafu alafu anashindwa kumfufua mchizi wake aliempa ubunge huu si ushenzi
Billie, kama hujui maana ya mpumbavu soma aya hii:
Zaburi 53:1
Mpumbavu
anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, na njia zao ni za uovu kabisa, hakuna hata mmoja atendaye mema.
 
Naomba nijikite hapa kwenye bold 👆

Ishara na maajabu

Matendo Mitume 5:1-11

Mungu NI maskini Sana mpaka kutegemea Mali za anania ?

Haya NI maajabu na ishara.

Asante Sana Setfree Kwa kunielimisha
The Coin Man soma Biblia kwa ufahamu. Kosa la Anania ni kusema uongo. Adhabu ya waongo ni kutupwa motoni
Ufu 21:8
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
 
Mpaka Leo miujiza ipo tu. Gwajima kila siku anafufua watu.
Usisahau kuna kifo cha kimwili na kiroho, my friend Percival
Waliokufa kiroho ni wengi na wanafufuliwa almost daily kote duniani. Na huo ndio ufufuo muhimu zaidi kuliko wa kimwili. Maana hata ukifufuliwa kimwili utakufa tena tu. Lakini ukifufuliwa kiroho hata ukifa utaendelea kuishi.
Yn 11:25-26
Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?
 
Hata wewe umesikia tu, maana sidhani kama ulikuwepo mwaka 1936 alipofariki.
Najua tofauti ya uganga na uchawi ila nafikiri tukianza kuelezana maana ya maneno hayo ya Kiswahili tutakuwa tumetoka nje ya lengo la mada. Au sio gallow bird?
Kuponya kipofu ni uganga si uchawi
 
Kuponya kipofu ni uganga si uchawi
Sijaelewa gallow bird unataka kusema nini. Kwamba waganga wanakubaliwa na Mungu? Waganga na wachawi lao moja tu. Angalia andiko hili:
Kut 7:11
Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao.
 
Ulokole ni upungufu wa akili....
Sasa wewe Mindray kama una akili timamu, kwanini unapoteza muda wako kusoma na ku-comment mada za walokole wenye upungufu wa akili?
Warumi 1:22
Wanajidai kuwa wenye hekima, kumbe ni wapumbavu.

Kama mwenye akili timamu anaongea na kichaa basi yamkini na yeye ni kichaa 😎
 
The Coin Man soma Biblia kwa ufahamu. Kosa la Anania ni kusema uongo. Adhabu ya waongo ni kutupwa motoni
Ufu 21:8

Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Setfree Ila wewe hahaha Acha Tu.

Yeremia 4:10 " Hakika Bwana umewadanganya watu hawa..."

Mungu WA Setfree atupwe motoni Kwa sababu ameongea "uongo"

Na wote kwa Jina la shetani tuseme

"Amen"

Maana yake imekua.
 
Miujiza ni tafsiri ya kiimani, si uthibitisho wa imani moja kuwa ya pekee.

Kinacho matter sana ni imani ya mtu wala siyo Biblia kama unavyo elezea.
 
Sijaelewa gallow bird unataka kusema nini. Kwamba waganga wanakubaliwa na Mungu? Waganga na wachawi lao moja tu. Angalia andiko hili:
Kut 7:11
Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao.
Kiswahili hujui, zamani tukienda hospital tuliingia vyumba vilivyoandikwa 'mganga'...yesu kutibu ukoma,kufukuza majini, alifanya uganga
 
Kiswahili hujui, zamani tukienda hospital tuliingia vyumba vilivyoandikwa 'mganga'...yesu kutibu ukoma,kufukuza majini, alifanya uganga
Umejitega kwa kamba yako mwenyewe gallow bird
Kumbe ni zamani? Kwanini sasa wameshtuka hawaandiki "Mganga" 😀 😀 😀
 
Kiswahili hujui, zamani tukienda hospital tuliingia vyumba vilivyoandikwa 'mganga'...yesu kutibu ukoma,kufukuza majini, alifanya uganga
Angalia waganga hawa baada ya kuokoka walivyochoma makabrasha yao ya uganga
Mdo 19:19
Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote...
 
Biblia ni hekaya za abunuwasi
 
Wanaandikaje?
Doctor of Medicine (M.D.)
Doctor of Dental Surgery (D.D.S.)
Doctor of Pharmacy (Pharm.D.)
Doctor of Veterinary Medicine (D.V.M.)
Doctor of Optometry (O.D.)
Doctor of Nursing Practice (D.N.P.)
Doctor of Physical Therapy (D.P.T.)
Doctor of Podiatric Medicine (D.P.M.)
Doctor of Chiropractic (D.C.)
 
Duh, The redemeer unamsahihisha Yesu aliyesema hivi:
Mk 16:17
"Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya."

Unapewaje karama ya miujiza kama huamini?
Imani si tiketi ya miujiza, ni uhusiano na Mungu,hata Tomas aliona kabla ya kuamini, lakini bado Yesu alimfunulia. Karama si malipo ya imani, ni mapenzi ya Mungu.
 
Biblia ni hekaya za abunuwasi
Hekaya? Soma uzi huu unaothibitisha kuwa Biblia ni kitabu cha kweli
 
Katika historia ya ulimwengu, tumeshuhudia matendo makuu yasiyoelezeka kwa akili ya kibinadamu, kama vile wagonjwa kupona, viwete kutembea, mabubu kuongea, vipofu kuona, wafu kufufuka, na bahari kugawanyika. Jambo la kushangaza ni kwamba, ishara hizi kubwa zimefanywa tu na watu wanaoiamini Biblia kuwa ni Neno la Mungu. Kwanini?

Mifano ya haraka:
Musa, aliyeiamini Torati, aliigawanya Bahari ya Shamu (Kutoka 14:21).
Elia, nabii wa Mungu, alileta moto kutoka mbinguni (1 Wafalme 18:38).
Mitume, waliohubiri Injili, walifanya ishara nyingi: Petro alimponya kiwete, Paulo alimfufua Eutiko (Matendo 3:6-8; 20:9-12).

Labda utasema hiyo miujiza ilifanywa zamani. Siku hizi hakuna miujiza! Mimi sio wa zamani. Sawasawa na andiko la Yohana 14:12, nimeshuhudia miujiza mikubwa maishani mwangu...

Nimepona makumi ya magonjwa kwa kuweka mkono tu sehemu inayouma na kukemea kwa Jina la Yesu. Mara nyingi, nimeyafukuza mapepo yaliyokuja kunishambulia.

Kwa Jina la Yesu, 'nimewapiga stop', si mara moja, majambazi waliojaribu kunidhuru, nk, nk, nk

Mambo haya mazito siyasikii au kuyaona nje ya watu wanaoiamini Biblia na Yesu mtenda miujiza. Kwanini?

Kama huo sio ushahidi kwamba Biblia ni Neno la Mungu, nitajie sababu yako wewe...
Kwanini ishara, maajabu na miujiza mikubwa inafanywa na watu wanaoiamini Biblia tu?
Unahangaika sana
 
Back
Top Bottom