Kwanini ishara, maajabu na miujiza mikubwa inafanywa na watu wanaoiamini Biblia tu?

Kwanini ishara, maajabu na miujiza mikubwa inafanywa na watu wanaoiamini Biblia tu?

Imani si tiketi ya miujiza, ni uhusiano na Mungu,hata Tomas aliona kabla ya kuamini, lakini bado Yesu alimfunulia. Karama si malipo ya imani, ni mapenzi ya Mungu.
Angalia hapa jinsi imani ilivyo muhimu ili watu wapate miujiza
Mt 13:58
Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutokuamini kwao.
 
Hata wewe umesikia tu, maana sidhani kama ulikuwepo mwaka 1936 alipofariki.
Najua tofauti ya uganga na uchawi ila nafikiri tukianza kuelezana maana ya maneno hayo ya Kiswahili tutakuwa tumetoka nje ya lengo la mada. Au sio gallow bird?
Dini zimeingia Afrika mwaka gani? , na je watu wa zamani walikuwa wakimtukuza Mwenyezi Mungu kwa njia ipi?
 
Angalia hapa jinsi imani ilivyo muhimu ili watu wapate miujiza
Mt 13:58
Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutokuamini kwao.
Ulidai mtu hawezi kuwa na karama pasipo kuamini, nikakukosoa kwa kukwambia kuwa karama ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu mwenyewe juu ya mtu fulani.

Ndiyo maana hata Petro kuna muda alianguka kiimani lakini bado kivuli chake kiliendelea kutenda miujiza (kuponya) , yote ni kwasababu alikuwa na karama ya Mungu(mapenzi ya Mungu).
 
Ulidai mtu hawezi kuwa na karama pasipo kuamini, nikakukosoa kwa kukwambia kuwa karama ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu mwenyewe juu ya mtu fulani.

Ndiyo maana hata Petro kuna muda alianguka kiimani lakini bado kivuli chake kiliendelea kutenda miujiza (kuponya) , yote ni kwasababu alikuwa na karama ya Mungu(mapenzi ya Mungu).
Notorious_Marcc unasoma Biblia ya wapi?
Miujiza ya kivuli cha Petro ilitokea baada ya Yesu kufufuka, wakati ambapo Petro alikuwa tayari ana imani thabiti na ameishajazwa Roho Mtakatifu. Soma vizuri Mdo.
 
Izi unazoandika ni ngonjera tu na hadithi.. Furahia maisha
Hahaa. Mungu anakupenda Friji la mtumba . Tubu dhambi zako uokoke. Ya kesho huyajui. Sikutishi lakini huenda
 
Kila mtu anaweza kutenda miujiza. Ila tunafanya kwa kujua na kutokujua. Ni suala la kuamua tu; Wengine wafanye miujiza wengine waende bar wakalewe.
 
Kila mtu anaweza kutenda miujiza. Ila tunafanya kwa kujua na kutokujua. Ni suala la kuamua tu; Wengine wafanye miujiza wengine waende bar wakalewe.
Sizitaki mbichi hizo 😎
Ingekuwa kila mtu anaweza kutenda miujiza watu wote wangekuwa na furaha tele, maana wangekuwa wanafanya miujiza ya kugeuza maji kuwa divai kila siku(Yn 2:1-25) au kubariki mikate 5 na samaki 2(Mk 6:41-42) wakala na kushiba miaka nenda rudi
 
Mimi sio Mkongwee kama wewe, ila habari nilizo nazo ni kwamba Ng'wanamalundi alifariki mwaka 1936 katika mazingira ya kichawi. Hakuwa anamuomba Mungu. Au kuna Ng'wanamalundi mwingine?
Hujajibu swali una uhakika gani Ng'wanamalundi alikua hamuombi Mungu
wake??
 
Nendeni hospitali kule ndo kuna wagonjwa kma kweli nyie mnaponyesha

Akili ndogo sana hii
Izo movie zenu mimi kama mimi hamnipati
 
Hata Yesu hakuponya watu wote kila mahali alipoenda.
Mt 13:58
Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutokuamini kwao.

Wewe Ibn Unuq unafikiri watu wote MOI na KCMC wanamwamini Yesu? Hujui kuwa huko nako kuna Atheists wasiotaka hata kuombewa?
Hospitalini hakuna mgonjwa anayeigiza, wale wote ni serious sick people, Ile siyo sehemu ya maigizo ndiyo maana wachungaji wenu waigizaji hawawezi kusogea.


Kwa nini Yesu anashindwa kuponya watoto wadogo wenye kansa na Sickle cell walio ICU?
Ni kwasababu wao pia hawana imani?
Mtoto mdogo anawezaje kujua maana ya Imani?
Huyo Yesu wenu inatakiwa siku ya mwisho atangulie yeye motoni maana ni muuaji asiye na huruma.


Madaktari wanaweza kutibu watu wote bila imani, Lakini yesu wenu anashindwa bila imani.
wachungaji wenu wenye vipawa pia huenda hospitali wanapoumwa siyo hao tu hata nyinyi.
hivi hapo nani ni bora kuliko mwingine?


Kama mnaweza kuponya, mlikuwa wapi wakati wa Corona, UKIMWI unaingia na wakati wa EBOLA kule Congo.
Hivi tofauti ya Yesu wenu na mganga wa kienyeji ni ipi?


Wale wakristo wanaokufa kwa magonjwa kanisani bado walikosa imani? Je, nyinyi ni bora kuliko wao?
Kama hicho kipawa cha uponyaji ni cha kweli, kwa nini T.B. Joshua mwenyewe hakuweza kujiponya alipougua?
 
Duh, The redemeer unamsahihisha Yesu aliyesema hivi:
Mk 16:17
"Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya."

Unapewaje karama ya miujiza kama huamini?
Karama hii apewayo mtu inaweza kuibiwa na mtu mwingine kwa njia za giza???
 
Karama hii apewayo mtu inaweza kuibiwa na mtu mwingine kwa njia za giza???
Asante sana Marcy kwa swali lako
Karama ya Roho Mtakatifu haiwezi kuibiwa na mtu mwingine kwa njia za giza. Karama ni zawadi ya kipekee kutoka kwa Mungu, inayotolewa kwa mapenzi yake na kwa utukufu wake. Imeandikwa:
“Lakini yote hutenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.”
(1 Wakorintho 12:11)

Karama ni ya kiroho, hivyo haiwezi kuibiwa au kuhamishwa kwa nguvu za giza, kwa sababu chanzo chake ni Roho Mtakatifu. Nguvu za giza hazina uwezo wa kuharibu kazi za Roho Mtakatifu.

Hata hivyo, kuna uwezekano mtu aliyepewa karama akamzimisha Roho au akasababisha karama aliyopewa isitende kazi kwa ufanisi iwapo atafanya mambo haya:
1. Dhambi (1 Wathesalonike 5:19 – “Msimzimishe Roho.”).
2. Kutotii au kuhama kwenye kusudi la Mungu.
3. Kuruhusu hofu au mashaka.

Kama umepewa karama na unaona haitendi kazi ipasavyo, sio kwamba imeibiwa. Bado ipo ndani yako. Inawezekana uliizimisha kwa namna fulani. Hivyo ichochee tena kwa maombi. Paulo aliona kitu kama hicho ndani ya Timotheo akamkumbusha aichochee karama yake.
2 Timotheo 1:6
"Kwa sababu hii nakukumbusha uchochee ile karama ya Mungu iliyowekwa ndani yako nilipokuwekea mikono yangu"
 
Usisahau kuna kifo cha kimwili na kiroho, my friend Percival
Waliokufa kiroho ni wengi na wanafufuliwa almost daily kote duniani. Na huo ndio ufufuo muhimu zaidi kuliko wa kimwili. Maana hata ukifufuliwa kimwili utakufa tena tu. Lakini ukifufuliwa kiroho hata ukifa utaendelea kuishi.
Yn 11:25-26
Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?
Sawa mkuu kwa ufafanuzi.
 
sikia wew nenda mtaa wa lumumba pale kuna viwete wa kutosha hebu kawaponeshe tuone
Hata Yesu hakuponya viwete wote wa Israeli. Ili mtu apate uponyaji sharti kwanza aamini. Usifikiri viwete wote wanamwamini Yesu au wanaamini kwamba wanaweza kupona kwa Jina la Yesu.
Mathayo 13:58
Naye[Yesu] hakufanya miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kwao.
 
Ukristo ni janja janja za mind control za watu, hauna ukweli wowote hata wenyewe haujithibitishi kuwa ukristo ni dini kutoka hata katika hicho kitabu kinachoaminiwa na wakristo wote duniani, ni hekaya za uzushi na falsafa za wayunani wa kigiriki.

Iko hivi turudi kwenye historia ya kweli ya uingiaji wa ukristo katika pwani ya Africa mashariki ambayo hata wabobezi wa kihistoria wa kikristo katika madhehebu yao yote wanaikubali historia hii.

Dini ya mwanzo kuingia pwani ya Africa mashariki na Tanzania kiujumla(Tanganyika na Zanzibar) ilikuwa ni Uislamu, waarabu kutoka bara arabu na waajemi walifika mwambao wa pwani ya Africa mashariki walifika kwa ajili ya biashara na kukuta wenyeji wa pwani unguja, pemba,kilwa, mombasa, lamu wakiwa na tamaduni zao na dini zao .

Ila kutokana na uislamu kuwa ni dini ya amani basi wenyeji wengi wa mwambao walivutika na dini ya uislamu na kuingia katika uislamu pasina kutezwa nguvu au kushurutishwa.

Baada ya karne 6 kupita baada kuingia uislamu katika mwambao huu wachuuzi wa kireno wa kikatoliki walipofika katika mwambao huu kilwa na zanzibar n.k walikuta wenyeji tayari wapo katika ustaarabu wa hali ya juu.

Jambo hili liliwashangaza sana so wakapata mfadhaiko kukuta Uislamu tayari umeshatamalaki na wenyeji walio wengi.

Walipojaribu kuingiza mafunzo ya kikristo na kushawishi watu waingie katika ukristo walipata upinzani mkubwa kwa kupingwa hivyo iliwawia ngumu kuweka mizizi ya ukristo katika pwani ya mwambao.

Wareno Wakatumia mbinu ya kuiteketeza miji kwa kuilipua na mizinga kama miji ya kilwa na kwengineko na kuharibu miundombinu, na kutumia nguvu kwa kuuwa watu na kuwafanya watumwa.

Hapa tunajifunza kuwa uingiaji wa ukristo Tanzania ilitumika nguvu na mabavu tofauti na ilivyokuwa uislamu,, turudini kusoma historia.

Mpaka alipokuja mkoloni wa kiingereza na mjerumani waliwashawishi watu kuingia katika ukristo kwa kujenga mashule na mahospitali na sharti ili upate huduma hizo ni lazima uwe mkristo.

Binafsi nashangaa sana Mtanzania ukiwa unaijua historia yako vizuri unakubalije kuwa mkristo?

Ikiwa hawa wamishionari ndio waliowafanya mababu zetu kuwa watumwa tena kwa kutumia nguvu?

Turudini katika historia... hata ukiangalia athari mpaka leo za utumwa zipo makanisa ya kale na wala sio miskiti ya kale.
Mfano wa kanisa la waingereza la madhehebu ya anglikana, zanzibar ndio biashara ya utumwa ilipokuwa ikifanyika je hakuna mazingatio juu ya hilo?

Tukirudi katika historia safi ya nchi yetu wapiganiaji wa Uhuru wa Tanganyika kwa asilimia 98 walikuwa ni waislamu. Hakuna na kujifunza hapo?

Muamko wa waislamu ulikuwa ni wa mapema sana katika nyanja zote za maisha ila kuna propaganda nyingi zinafanywa za kielimu na kihistoria ili Uislamu uonekane sio chochote si lolote wakati historia ya nchi hii imebebwa na mababu zetu ambao kwa asilimia kubwa walikuwa ni waislamu.

Ukitaka mtu umpoteze mnyime historia yake na mtengenezee propaganda.
 
Back
Top Bottom