Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
- Thread starter
- #61
Moment of silentUkristo ni janja janja za mind control za watu, hauna ukweli wowote hata wenyewe haujithibitishi kuwa ukristo ni dini kutoka hata katika hicho kitabu kinachoaminiwa na wakristo wote duniani, ni hekaya za uzushi na falsafa za wayunani wa kigiriki.
Iko hivi turudi kwenye historia ya kweli ya uingiaji wa ukristo katika pwani ya Africa mashariki ambayo hata wabobezi wa kihistoria wa kikristo katika madhehebu yao yote wanaikubali historia hii.
Dini ya mwanzo kuingia pwani ya Africa mashariki na Tanzania kiujumla(Tanganyika na Zanzibar) ilikuwa ni Uislamu, waarabu kutoka bara arabu na waajemi walifika mwambao wa pwani ya Africa mashariki walifika kwa ajili ya biashara na kukuta wenyeji wa pwani unguja, pemba,kilwa, mombasa, lamu wakiwa na tamaduni zao na dini zao .
Ila kutokana na uislamu kuwa ni dini ya amani basi wenyeji wengi wa mwambao walivutika na dini ya uislamu na kuingia katika uislamu pasina kutezwa nguvu au kushurutishwa.
Baada ya karne 6 kupita baada kuingia uislamu katika mwambao huu wachuuzi wa kireno wa kikatoliki walipofika katika mwambao huu kilwa na zanzibar n.k walikuta wenyeji tayari wapo katika ustaarabu wa hali ya juu.
Jambo hili liliwashangaza sana so wakapata mfadhaiko kukuta Uislamu tayari umeshatamalaki na wenyeji walio wengi.
Walipojaribu kuingiza mafunzo ya kikristo na kushawishi watu waingie katika ukristo walipata upinzani mkubwa kwa kupingwa hivyo iliwawia ngumu kuweka mizizi ya ukristo katika pwani ya mwambao.
Wareno Wakatumia mbinu ya kuiteketeza miji kwa kuilipua na mizinga kama miji ya kilwa na kwengineko na kuharibu miundombinu, na kutumia nguvu kwa kuuwa watu na kuwafanya watumwa.
Hapa tunajifunza kuwa uingiaji wa ukristo Tanzania ilitumika nguvu na mabavu tofauti na ilivyokuwa uislamu,, turudini kusoma historia.
Mpaka alipokuja mkoloni wa kiingereza na mjerumani waliwashawishi watu kuingia katika ukristo kwa kujenga mashule na mahospitali na sharti ili upate huduma hizo ni lazima uwe mkristo.
Binafsi nashangaa sana Mtanzania ukiwa unaijua historia yako vizuri unakubalije kuwa mkristo?
Ikiwa hawa wamishionari ndio waliowafanya mababu zetu kuwa watumwa tena kwa kutumia nguvu?
Turudini katika historia... hata ukiangalia athari mpaka leo za utumwa zipo makanisa ya kale na wala sio miskiti ya kale.
Mfano wa kanisa la waingereza la madhehebu ya anglikana, zanzibar ndio biashara ya utumwa ilipokuwa ikifanyika je hakuna mazingatio juu ya hilo?
Tukirudi katika historia safi ya nchi yetu wapiganiaji wa Uhuru wa Tanganyika kwa asilimia 98 walikuwa ni waislamu. Hakuna na kujifunza hapo?
Muamko wa waislamu ulikuwa ni wa mapema sana katika nyanja zote za maisha ila kuna propaganda nyingi zinafanywa za kielimu na kihistoria ili Uislamu uonekane sio chochote si lolote wakati historia ya nchi hii imebebwa na mababu zetu ambao kwa asilimia kubwa walikuwa ni waislamu.
Ukitaka mtu umpoteze mnyime historia yake na mtengenezee propaganda.
Umeandika hoja nyingi bila ushahidi wowote. Naomba nikujibu kama ifuatavyo:
Yesu alitabiri kwamba Wakristo watapingwa na kuteswa. Hivyo siwashangai watu kama nyinyi mnaotoa mada za upinzani.
“Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu” — Mathayo 10:22.
Kwahiyo mada yako tu yenyewe inathibitisha ukweli wa Biblia.
Mafundisho ya Kikristo sio uzushi kama unavyodai.
“Kwa maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu...” — 2 Petro 1:16
Ukristo haujajengwa juu ya hekaya wala falsafa za wanadamu, bali juu ya ushuhuda wa watu waliomwona Yesu kwa macho au kusikia sauti yake "live" kama Paulo.
Ukristo si wa Wazungu au Wareno — ni wa Mungu
“Watu wa kila taifa chini ya mbingu…” — Matendo 2:5
Tangu siku ya Pentekoste, Ukristo ulienea kwa mataifa yote. Hauna uraia wa kizungu; ni injili kwa mataifa yote.
Ukombozi wa kweli hauji kwa historia, bali kwa njia ya Yesu
“Nanyi mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.” — Yohana 8:32
Historia inaweza kupotoshwa, lakini Yesu ndiye kweli — na hutuweka huru.
Kumwamini Yesu sio dhambi ya ukoloni — ni neema ya wokovu
“Wokovu haupatikani kwa mwingine awaye yote…” — Matendo 4:12
Ukristo sio matokeo ya shule wala hospitali, bali ni wito wa wokovu kupitia jina la Yesu pekee.
Ukiwachukia Wakristo unamchukia Kristo mwenyewe
“Atakayewachukia ninyi, amenichukia mimi kwanza.” — Yohana 15:18
Huwezi kupinga Ukristo kwa sababu ya wanadamu waliokosea; msingi wa Ukristo ni Kristo, sio Wareno wala Waingereza.
Watumwa ni wale walio mbali na Kristo
“Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.” — Yohana 8:34
Yesu hakutufanya watumwa wa mkoloni, bali alikuja kutuachilia huru kutoka katika utumwa wa dhambi.
Kama Ukristo ungekuwa wa uongo, usingesimama hadi leo
“Kama shauri hili linatoka kwa wanadamu, litavunjika… bali kama ni la Mungu, hamtaweza kulivunja.” — Matendo 5:38–39
Mamia na mamia ya miaka ya upinzani hayajaangamiza Ukristo. Huo ni uthibitisho kwamba chanzo cha Ukristo ni Mungu. Amen?