The Coin Man
JF-Expert Member
- Jan 2, 2025
- 1,471
- 1,879
Naomba nijikite hapa kwenye bold πKwanini?
Kama huo sio ushahidi kwamba Biblia ni Neno la Mungu, nitajie sababu yako wewe... Kwanini ishara, maajabu na miujiza mikubwa inafanywa na watu wanaoiamini Biblia tu?
Billie, kama hujui maana ya mpumbavu soma aya hii:Miujiza ni upumbafu kwa wapumbafu pekee.Mtu anaponya na kufufua wafu alafu anashindwa kumfufua mchizi wake aliempa ubunge huu si ushenzi
The Coin Man soma Biblia kwa ufahamu. Kosa la Anania ni kusema uongo. Adhabu ya waongo ni kutupwa motoniNaomba nijikite hapa kwenye bold π
Ishara na maajabu
Matendo Mitume 5:1-11
Mungu NI maskini Sana mpaka kutegemea Mali za anania ?
Haya NI maajabu na ishara.
Asante Sana Setfree Kwa kunielimisha
Usisahau kuna kifo cha kimwili na kiroho, my friend PercivalMpaka Leo miujiza ipo tu. Gwajima kila siku anafufua watu.
Kuponya kipofu ni uganga si uchawiHata wewe umesikia tu, maana sidhani kama ulikuwepo mwaka 1936 alipofariki.
Najua tofauti ya uganga na uchawi ila nafikiri tukianza kuelezana maana ya maneno hayo ya Kiswahili tutakuwa tumetoka nje ya lengo la mada. Au sio gallow bird?
Sijaelewa gallow bird unataka kusema nini. Kwamba waganga wanakubaliwa na Mungu? Waganga na wachawi lao moja tu. Angalia andiko hili:Kuponya kipofu ni uganga si uchawi
Sasa wewe Mindray kama una akili timamu, kwanini unapoteza muda wako kusoma na ku-comment mada za walokole wenye upungufu wa akili?Ulokole ni upungufu wa akili....
Setfree Ila wewe hahaha Acha Tu.The Coin Man soma Biblia kwa ufahamu. Kosa la Anania ni kusema uongo. Adhabu ya waongo ni kutupwa motoni
Ufu 21:8
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Kiswahili hujui, zamani tukienda hospital tuliingia vyumba vilivyoandikwa 'mganga'...yesu kutibu ukoma,kufukuza majini, alifanya ugangaSijaelewa gallow bird unataka kusema nini. Kwamba waganga wanakubaliwa na Mungu? Waganga na wachawi lao moja tu. Angalia andiko hili:
Kut 7:11
Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao.
Umejitega kwa kamba yako mwenyewe gallow birdKiswahili hujui, zamani tukienda hospital tuliingia vyumba vilivyoandikwa 'mganga'...yesu kutibu ukoma,kufukuza majini, alifanya uganga
Angalia waganga hawa baada ya kuokoka walivyochoma makabrasha yao ya ugangaKiswahili hujui, zamani tukienda hospital tuliingia vyumba vilivyoandikwa 'mganga'...yesu kutibu ukoma,kufukuza majini, alifanya uganga
Wanaandikaje?Umejitega kwa kamba yako mwenyewe gallow bird
Kumbe ni zamani? Kwanini sasa wameshtuka hawaandiki "Mganga" π π π
Biblia ni hekaya za abunuwasiAngalia waganga hawa baada ya kuokoka walivyochoma makabrasha yao ya uganga
Mdo 19:19
Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote...
Doctor of Medicine (M.D.)Wanaandikaje?
Imani si tiketi ya miujiza, ni uhusiano na Mungu,hata Tomas aliona kabla ya kuamini, lakini bado Yesu alimfunulia. Karama si malipo ya imani, ni mapenzi ya Mungu.Duh, The redemeer unamsahihisha Yesu aliyesema hivi:
Mk 16:17
"Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya."
Unapewaje karama ya miujiza kama huamini?
Hakika.Miujiza ufanywa na mtu yeyeto aliyepewa karama za miujiza haijalishi anaeamini au la
Hekaya? Soma uzi huu unaothibitisha kuwa Biblia ni kitabu cha kweliBiblia ni hekaya za abunuwasi
Unahangaika sanaKatika historia ya ulimwengu, tumeshuhudia matendo makuu yasiyoelezeka kwa akili ya kibinadamu, kama vile wagonjwa kupona, viwete kutembea, mabubu kuongea, vipofu kuona, wafu kufufuka, na bahari kugawanyika. Jambo la kushangaza ni kwamba, ishara hizi kubwa zimefanywa tu na watu wanaoiamini Biblia kuwa ni Neno la Mungu. Kwanini?
Mifano ya haraka:
Musa, aliyeiamini Torati, aliigawanya Bahari ya Shamu (Kutoka 14:21).
Elia, nabii wa Mungu, alileta moto kutoka mbinguni (1 Wafalme 18:38).
Mitume, waliohubiri Injili, walifanya ishara nyingi: Petro alimponya kiwete, Paulo alimfufua Eutiko (Matendo 3:6-8; 20:9-12).
Labda utasema hiyo miujiza ilifanywa zamani. Siku hizi hakuna miujiza! Mimi sio wa zamani. Sawasawa na andiko la Yohana 14:12, nimeshuhudia miujiza mikubwa maishani mwangu...
Nimepona makumi ya magonjwa kwa kuweka mkono tu sehemu inayouma na kukemea kwa Jina la Yesu. Mara nyingi, nimeyafukuza mapepo yaliyokuja kunishambulia.
Kwa Jina la Yesu, 'nimewapiga stop', si mara moja, majambazi waliojaribu kunidhuru, nk, nk, nk
Mambo haya mazito siyasikii au kuyaona nje ya watu wanaoiamini Biblia na Yesu mtenda miujiza. Kwanini?
Kama huo sio ushahidi kwamba Biblia ni Neno la Mungu, nitajie sababu yako wewe... Kwanini ishara, maajabu na miujiza mikubwa inafanywa na watu wanaoiamini Biblia tu?