Kwanini ishara, maajabu na miujiza mikubwa inafanywa na watu wanaoiamini Biblia tu?

Moment of silent
Umeandika hoja nyingi bila ushahidi wowote. Naomba nikujibu kama ifuatavyo:

Yesu alitabiri kwamba Wakristo watapingwa na kuteswa. Hivyo siwashangai watu kama nyinyi mnaotoa mada za upinzani.
“Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu” — Mathayo 10:22.

Kwahiyo mada yako tu yenyewe inathibitisha ukweli wa Biblia.

Mafundisho ya Kikristo sio uzushi kama unavyodai.
“Kwa maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu...” — 2 Petro 1:16

Ukristo haujajengwa juu ya hekaya wala falsafa za wanadamu, bali juu ya ushuhuda wa watu waliomwona Yesu kwa macho au kusikia sauti yake "live" kama Paulo.

Ukristo si wa Wazungu au Wareno — ni wa Mungu
“Watu wa kila taifa chini ya mbingu…” — Matendo 2:5

Tangu siku ya Pentekoste, Ukristo ulienea kwa mataifa yote. Hauna uraia wa kizungu; ni injili kwa mataifa yote.

Ukombozi wa kweli hauji kwa historia, bali kwa njia ya Yesu
“Nanyi mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.” — Yohana 8:32

Historia inaweza kupotoshwa, lakini Yesu ndiye kweli — na hutuweka huru.

Kumwamini Yesu sio dhambi ya ukoloni — ni neema ya wokovu
“Wokovu haupatikani kwa mwingine awaye yote…” — Matendo 4:12

Ukristo sio matokeo ya shule wala hospitali, bali ni wito wa wokovu kupitia jina la Yesu pekee.

Ukiwachukia Wakristo unamchukia Kristo mwenyewe
“Atakayewachukia ninyi, amenichukia mimi kwanza.” — Yohana 15:18

Huwezi kupinga Ukristo kwa sababu ya wanadamu waliokosea; msingi wa Ukristo ni Kristo, sio Wareno wala Waingereza.

Watumwa ni wale walio mbali na Kristo
“Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.” — Yohana 8:34

Yesu hakutufanya watumwa wa mkoloni, bali alikuja kutuachilia huru kutoka katika utumwa wa dhambi.

Kama Ukristo ungekuwa wa uongo, usingesimama hadi leo
“Kama shauri hili linatoka kwa wanadamu, litavunjika… bali kama ni la Mungu, hamtaweza kulivunja.” — Matendo 5:38–39

Mamia na mamia ya miaka ya upinzani hayajaangamiza Ukristo. Huo ni uthibitisho kwamba chanzo cha Ukristo ni Mungu. Amen?
 
Kwanza ulitakiwa uikubali au uipinge kwa hoja ikiwa nimeongopa.

Mtu akijuwa historia yake sio rahisi kumpelekesha.

Turudi kwenye nukta zako ambazo unaona kwamba zimekukinaisha kuwa ukristo ni Dini ya Mungu.

Umeleta mistari ambayo hata yenyewe kwenye biblia inakinzana.

Nijibu maswali haya:-
# Nipe andiko la wazi linalothibitisha kuwa ukristo ni Dini kutoka kwenye biblia.

# Nipe andiko linalosema kuwa Yesu alikuwa mkristo? Yaani mwanzilishi wa ukristo.

Turudi tena;

Ni wapi kwamba Paulo( Sauli) alimdiriki Yesu? Mbona hapa unapotosha mkuu?

Mbona maandiko hayo hayo yanasema kuwa ukristo ni jina la kupanga kutoka Antokia( ugiriki) na wafuasi wa mwanzo waliitwa na wapagani wa Antokia kuwa hawa ni wakristo? Ukitaka andiko nitakuletea kwa usanifu wake halisi.
Maana yake kabla ya hapo wafuasi wa kristo(Yesu) hawakuwa wakiitwa wakristo tuelewane kwenye nukta hii.

Kwa maana sisi tunawaita wakristo kwa kuwa mliitwa na wapagani wa Antokia kuwa nyingi ni wakristo na wala sio dini, na jina hilo la wapagani wa Antokia mkalipokea vyenginevyo sijui tungewaitaje?

Maana dini ni mfumo wa maisha ya kila siku.
So ukristo ni jina sio dini!!

Kama lipo andiko lilete hapa usibabaishe kwa kukuwepa na kuleta mistari mingi ya biblia ambayo wala haihusiani na swali nililo uliza.
 
Mkuu naona umezungumzia Musa kupasua bahari hapo sasa Musa alitumua TORAT au biblia maana hiyo bibilia hata yesu haijui
Hakuna nabii alopewa biblia labda akina zumaridi mwamposa na wengine
 
sawa kachomoe wawili tu wa mfano pale lumumba wengine waache kama yesu alivowaacha
 
"Nimepona makumi ya magonjwa kwa kuweka mkono tu sehemu inayouma na kukemea kwa Jina la Yesu. Mara nyingi, nimeyafukuza mapepo yaliyokuja kunishambulia".
 
Katika vitu ulivyoandika na kujinasibu navyo wala sijaona muujiza hapo.
Wamasai wakiumwa huwa wanapona bila kwenda hospitali kwa hiyo tuseme nao wana miujiza?
Na kuhusu ishu ya kuzuia majambazi ili tuamini inabidi siku wakivamia benki uende ukasimame mbele yao kisha useme"kwa jina la yesu mshindwe" ukinusurika hapo wakashindwa kufyatua risasi hapo sawa tutakyamini kwamba una miujiza ila sio kwa kujifungia chumbani halafu majambazi wakisitisha zoezi eti unasema wameogopa miujiza yako haiingii akilini.
 
Asante sana kwa majibu mazuri
 
Musa na torati kichwa cha habari biblia mbona ni maji na mafuta
 

Miujiza ipo na naikubali na naamini mtu akitumia jina la Yesu ambaye ndiye alipewa hiyo Nguvu na Mungu anaweza kufanya mengi. Kwa sisi wengine tuliosoma kusudio la kila mtume, akiwemo Mussa, na wengine waliomtangulia, Kila mmoja alitumwa duniani kipindi chake na kwa kazi maalum.

Mfano: Kuna kipindi dunia iligubigwa na wimbi kubwa sana la watu kuamini Uchawi na Ushirika. Wachawi ndio walionekana kama Miungu. Mungu mwenye mamlaka yote akaona atume mjumbe (mtume) na kumpa uwezo wa kufanya zaidi ya hao wachawi na washikina ili watu wajue kuwa yupo Mungu mmoja tu mwenye mamlaka yote. Ni wakati huo ambapo Mungu akamtuma Yesu huku akipewa uwezo mkubwa kuliko wachawi na washirikina; ni kwa bahati mbaya sana WANADAMU WAKAMTAMBUA YESU KUWA YEYE NDIYE MUNGU, BADALA YA KUMUAMINI MUNGU ALIYEMPA HIYO NGUVU NA KUMTUMA HUKU DUNIANI kwa kazi maalumu kama mitume wengine walio mtangulia walivyo tumwa huku duniani..

Ikumbukwe kuwa Yesu sio wa Wakrito pekee, bali Yesu ni mtume wa Mungu hivyo ni mtume wa wote wanao Muamini Mungu mmoja mwenye mamlaka yote!
Kwa maana hiyo, hata mtu wa dini nyingine Inayo mtambua Yesu kama mjumbe wa Mungu, anaweza kuomba kwa kutumia jina lake na kusaidika kwani ndiye mtume alipewa nguvu hiyo.
 
Duh yani mbao za safina ziwepo adi leo, anyway.
 
Asante Mparee2 kwa kuchangia mada. Yesu ni zaidi ya Mtume. Yesu ni Mungu. Naomba usome uzi huu utapata maelezo ya kina:
 

Najua kuna vifungu kadhaa watu wana unga unga na kujenga hoja ya kumtambua Yesu kama Mungu ila kwa akili aliyonipa Mungu bure (Mungu mmoja mwenye mamlaka yote) siwezi kuamini kama Mungu anaweza Kuzaliwa na binadamu, KULALA USINGIZI, kula na kuenda haja kama sisi, kutumia muda mwingi akikesha kumuomba "Mungu, halafu eti huyo awe tena ni Mungu", Yaani Mungu alimuumba Binadamu, Binadamu akamkosea Mungu, halafu Mungu akakubali auwawe na Binadamu ili amsamehe Binadamu., Mh nafikiri hapa ndipo Yesu alishaonya kuwa..tutakuja kuangamia kwa kukosa maarifa?
Lakini sishangai kwani...
Kuna Mwana theologia mmoja mbobezi kule Italy (Vatican) aliniambia; Baadhi ya vifungu vya Biblia, kama Marko 16:9-20 na Yohana 7:53–8:11 na vinginevyo vilitengenezwa tu ili kuboresha imani ya waamini ILA, havipo katika maandiko ya kale kabisa, hivyo wahariri wa Biblia wameamua kuvi delete... na utafiti unaendelea kuiboresha. Pengine karne ijayo tukapata BIBLIA MPYA itakayo mtambua Yesu kwa nafasi yake ya utume na sio kwa nafasi ya Mungu mmoja tu mwenye mamlaka yote!
 
Mungu atateswa na kuuliwa na viumbe aliyewaumba mwenyewe na kumtundundika msalabani?

Mbona huu ni wendawazimu wa kiwango cha hali ya juu.

Imani ya kikristo ni imani ya kibubusa isiyokuwa na logic yoyote ndani yake.
''Elloi Elloi lamma sabkhataniii.''
''Mungu wangu Mungu wangu mbona unaniacha?".
 

Attachments

  • 29a7a33ef7b5a4e70555ce30f2413f59.mp4
    12.1 MB
Bro, I get your shock, maana fumbo la msalaba haliwezi kueleweka kwa akili peke yake.
Lakini fikiria hivi: Is it weakness or greatness when the Creator chooses to suffer for His creation?
Yesu hakuteswa kwa kushindwa, alikubali kuteswa kwa hiari.
Yohana 10:18
"Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu, na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena. Amri hii nimepewa na Baba yangu."

Na hiyo kauli “Mungu wangu mbona umeniacha” ni kutoka Zaburi 22 — prophecy fulfilled live. Si kilio cha kushindwa

Ukristo si "imani ya kibubusa," ni imani inayomjua Mungu aliye tayari kushuka chini hadi kwenye maumivu yetu. That’s not madness, that’s divine love.😎
 
mbona biblia hiyo hiyo inasema ameelaaniwa kila atundukiwaye kwenye msalaba?

shida yenu nyinyi ni wabishi, mnapewa vitu vyenye mantiki ila tu kugeuza geuza maneno.
ili mpate wajinga wa kuwapotoa.

hapo juu hukujibu hata kimoja kielimu umebabaisha tu.
kubishana na nyie ni kupoteza muda tu.

Hapo ulipo Mungu wako humjui nani?

Mpaka leo hii wakristo hamumjui Mungu ni yupi... Hadi kuandika napata kichefu chefu jinsi mlivyompa mwandamu cheo cha Uuungu na wengine kusema ni mtoto wa Mungu daaah....

Qur'an : Angalia jinsi tunavyowabainishia aya zetu, alafu angalia jinsi gani wanavyogeuzwa.
 
mbona biblia hiyo hiyo inasema ameelaaniwa kila atundukiwaye kwenye msalaba?
Hilo andiko umelinukuu nusu tu ndugu yangu Moment of silent. Aya nzima inasema hivi:
"Kristo alitukomboa katika laana ya sheria kwa kuwa alifanyika laana kwa ajili yetu, kwa maana imeandikwa: Amelaaniwa kila atundikwaye juu ya mti."(Gal 3:13)

Andiko hilo halina maana kwamba Yesu alikuwa na dhambi hivyo alilaaniwa. Hapana. Badala yake, alijitoa kwa hiari kuchukua laana zetu, yaani, adhabu ya dhambi zetu juu ya mwili wake, ili kutuokoa. Ndio sababu andiko jingine linasema:
Lakini alijeruhiwa kwa ajili ya makosa yetu, alichubuliwa kwa ajili ya maovu yetu; adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake[kwa kupigwa kwake] sisi tumepona. (Isaya 53:5)
 
Miujiza? Nimeuliza mbona hao wahubiri wa miujiza hawaombei watu waliokatwa mguu au mkono warudishiwe viungo vyao? Hakuna aliyejibu. Is their God limited in his miracles? Wamebaki na hadithi za kupona uvimbe,kansa,ukimwi..... basi. Mtihani wangu wameshindwa. Kwa hiyo nasema hiyo si miujiza ni mazingaombwe tu!
 
Mazingaombwe ni nini? Kwanini unataka kushindana na neno la Mungu? Unataka muujiza uone wewe ndio upate kusimulia anza kwa kuamini tu maana hata mtumishi gani akimuombea mwenye uhitaji huku anawaka moto kama hana imani hii ni kazi bure! pia nikufafanulie uepukane na hii dhambi unayojiamini nayo…na asante kwa hii hoja ya kuhoji kwa nini wahubiri wa leo hawafanyi miujiza kama kurudisha kiungo kilichokatwa ni hoja ya kupotosha imani ya watu kwa kutumia mantiki za kibinadamu kumjaribu Mungu. Tunaweza kuitetea imani kwa kutumia maandiko…

1. Mungu Hajaribiwi
Mathayo 4:7 "Yesu akamwambia, Imeandikwa tena, Usimjaribu Bwana Mungu wako.”
Yesu mwenyewe alikataa kumjaribu Mungu hata alipokuwa na uwezo wa kufanya miujiza. Hii inatufundisha kuwa miujiza si kitu cha kuamuliwa na wanadamu kwa kupenda bali hufanyika kwa mapenzi ya Mungu.

2. Miujiza Sio kwa Show au Kujionyesha
Luka 11:16 “Wengine wakamjaribu, wakitaka ishara itokayo mbinguni.”
Lakini Yesu hakuwapa. Hii inaonyesha kuwa Yesu hakufanya miujiza kwa kushinikizwa au kwa lengo la kuwafurahisha watu waliokuwa na mashaka.. kwahiyo ni wewe kuchagua either uache mashaka umfuate Mungu kwa kutafute kweli, ila kwa hizi kejeli na dhihaka utasugua hapo..

3. Miujiza Hufanyika kwa Imani na Mapenzi ya Mungu
Marko 6:5-6 “Wala kutaka kushuhudia ili ukose la kusema hakuweza kufanya muujiza wowote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache akawaponya. Akastaajabu kwa sababu ya kutokuamini kwao.”
Miujiza hutegemea imani na mapenzi ya Mungu, si kila mahali au kila mtu anastahili kuona muujiza.

4. Lengo la Miujiza ni Kumtukuza Mungu, Siyo Kutosheleza Mashaka ya Watu..
Yohana 20:30-31 “Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki; lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini...”
Miujiza ni kwa ajili ya kuthibitisha ujumbe wa Mungu, si kwa kushindana au kudhihirisha uwezo kwa masharti ya watu..

Kupinga miujiza kwa msingi wa "mbona hawarudishi mikono au miguu" ni kujaribu kumwekea Mungu masharti kama vile ni mwigizaji wa maajabu..Mungu hafanyi kazi kwa presha ya mashaka ya watu. Anajifunua kwa aliowachagua na kwa wakati anaotaka.
Waebrania 11:6 “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu...”

Hoja hiyo si hoja ya utafutaji wa kweli, bali ni ya kujaribu.. sasa endelea kumjaribu Bwana Mungu wako kijana mjuaji!
 
Umemjibu vema. Ubarikiwe sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…