Kwanini January Makamba unakataa kutambua nguvu na juhudi za hayati Magufuli kwenye JNPP?

Kwanini January Makamba unakataa kutambua nguvu na juhudi za hayati Magufuli kwenye JNPP?

Ukweli lazima usemwe, kuna tatizo gani kutambua juhudi za hayati Magufuli kwenye mradi huu wa umeme (JNHP), hasa kwenye hotuba zenu?

Wazo lilikuwa la Mwalimu Nyerere akashindwa, awamu zilizofuata kuanzia ya pili mpaka ya NNE, hawakuwa na habari na mradi huo, waliupa kisogo.

Hayati Magufuli kwa nguvu kubwa na ujasiri usio na shaka akaamua kutekeleza wazo hilo.

Miongoni mwa waliohujumu juhudi hizi ni waziri wa sasa wa nishati, January Makamba kwa kisingizio cha uharibifu wa mazingira, ikapelekea kuondolewa baraza la mawaziri.

Leo hotuba ya mkurugenzi mkuu Maharage Chande na waziri wake wamejificha kwenye kichaka cha mipasho hasa waziri Makamba.

Nijielekeze kwenye usanii wa waziri Makamba kutambua juhudi za watangulizi kwenye ujenzi wa bwawa hilo, katengeneza zawadi za kutambua michango ya mzee Mwinyi ,na Jakaya, wana mchango gani ikiwa mradi waliupa kisogo?

Makamba junior kawapa medali za kinafiki sana, hata wao wamejisikia aibu sana kupewa medali za ushiriki wao kwa mradi wakati hawajashiriki hata kidogo.,dhambi kubwa sana ikiambatana na unafiki wa hali ya juu.

Huyu kijana ndio anawaza kuwa rais wa hii nchi. Tuna hasara kubwa kama taifa.

Nimpongeze rais Samia kwa kujaribu kuusema ukweli kuhusu kazi kubwa ya hayati Magufuli katika kufanikisha mradi huu.

Kumekuwa na syndicate kupoteza Juhudi za hayati Magufuli kwa kuzimeza kijumla jumla na wasiostahili. Mojawapo ni hilo tukio la kinafiki la kutambua mchango wa hao watanguli kuhusu bwawa hili, wakati si washiriki.

Namalizia kwa kumwambia waziri Makamba na walio nyuma yake kwamba watanzania hawadanganyiki tena, Magufuli aliwafumbua macho.

Huu mchezo wa kujaza vijana mitandaoni kumdhihaki, mmeona leo jinsi likitajwa jina lake makofi na shangwe kama lote.

Nikiashiria kwamba kimwili hatuko naye ila kifikra tukonae, acheni majungu dhidi ya marehemu.
Mimi nakumbuka wakati Edward Lowassa alipopewa nafasi kwenda Ikulu wakati huo akiwa bado kiongozi ndani ya CHADEMA aliongea mengi kumpongeza JPM but what was so conspicuous alisema anampongeza sana mno kwa kuanzisha Stiglers gorge. Baadhi yetu ndio hapo tulipoanza kutafiti hiyo Stiglers gorge ndio nini.
 
Itakua kweli , huyu jamaa Kwa Sasa ni mtoto pendwa .

Alafu ana ujanja ujanja Fulani ivi ambao Kwa Sisi akili kubwa, tunamuona mjinga.


Anamtanguliza Samia mbele, yeye anakua nyuma
Aliyewaibia kura chadema 2015 akampa JPM kwenye mfumo wa NEC ni nani kama sio huyo Makamba
Na ndio mana walipogombana jamaa aligoma kuomba msamaha
Makamba sio nappe Mzee uchaguzi ujao anawaibia tena kura na kumpa Samia hahaha
 
Makamba ni mdudu tu kwa JPM. Jina la Magufuli litasurvive test of time na litaimbwa vizazi na vizazi. Familia ya makamba itasahaulika na kupotea kama moshi kwenye hewa
Siasa umeanza juzi unalijua daraja la mkapa limeishia wap nani analisemea kwa Sasa
 
Nimemsikia kinana akisema, utekelezaji wa mradi ni ilani ya ccm bila kumtaja mfanikishaji. Huu ni uovu, watende haki kumkumbuka jpm
Mwaka 2011 nilikaa na Jakaya kikwete mahali alinambia tunataka Tanzania ya viwanda
That time hakukuwa na kampeni yyt wala haikuingia alikilo nin maana ya viwanda na ajira zilikua njenje

Baadae baada ya JPM kuingia madarakani akazundua Tanzania ya Viwanda ndio akili ikanijia kuw a kumbe nchi taitaweza kutoa ajira kama zamani hivyo vision ya viwanda ya JK ilikuwa sahihi ingawa that time hatukuelewa ana maanisha nn mana tayari tulilamba shavu serikalini

Kwaio kusema anatekeleza ilani ya CCM ni sahihi kabisa
 
Mama Sa100 aliniboa sana alipowarudisha wanafki Makamba, Nape na Madelu kwenye baraza la mawaziri.
Wale na JPM waligombana Kwa ajili ya pride
Makamba na Nappe walitaka JPM awape some respect Kwa sababu walipambana sana ili JPM ashinde matokeo yake JPM aliwageuka na kuwakumbatia Makonda, Mnyeti Gambo Hapi ambao hawakuwepo kwenye battle field ya uchaguzi

Hio ndio maana JPM na Makamba hawakuiva na bila unafiki Makamba hakuwahi kumuomba msamaha baada ya kurekodiwa
 
January Makamba hapendi unafiki na Watz jinsi walivyo ukisimamia Ukweli jiandae kukosolewa

January Makamba hapendi unafiki na Watz jinsi walivyo ukisimamia Ukweli jiandae kukosolewa
louse.jpg
 
Ukweli siku zote humweka mtu huru,bila JPM huyo Makamba angeenda leo kutoa hiyo hotuba? Kwanini hakwenda kipindi cha Awamu ya nne?
Kama Makamba angekuwa ndio Rais Nina hakika ilo bwawa lisingejengwa lingeishia hapo Kwa jinsi walivyokuwa hawamatch

JPM aliwapuuza waliompa ushindi na wao wanampuuza
Makamba hakuwahi kumuomba msamaha JPM usisahau ilo
Nappe, kinana, makamba Mzee walienda kuomba msamaha Makamba Jr hakunda usisahau ilo na JPM hakuwahi mfanya kitu
 
Back
Top Bottom