Kwanini jirani zangu hawanichangamkii?

Hili ni muhimu sana usisahau.
Katika maisha jitahd kadri iwezekanavyo sehem uliyopanga kuishi ununue kiwanja bei ghali zaid. Ni bora ununue kiwanja bei ghali ujenge nyumba ya kawaida kuliko kununua kiwanja bei ndogo ukajenga ghorofa la bei ghali halafu hapo mtaani wewe ukaoneka star wa eneo.
Sehemu unayoishi unaponunua unanunua majiran wa familia na connection ya watoto ukubwani. Ni kama vile unavyosomesha watoto. Zile ada kubwa ni pamoja na kumkonect mtoto na watoto wa wakubwa so katika life lake hawez start from nothing but kuna watu anaojuana nao tayar wazazi wao either ni wafanyabiashara wakubwa au big names ambao kazi ni chap anapata.
 
Vipi mahusiano yako na majirani kipindi unajenga hiyo nyumba? Au umekuja kuwaarika tu wakati nyumba unahamia na huko nyuma ulikuwa unawalia bati na kuwapita kama ng'ombe?
 
Hata ingekua mimi jirani siji
Ushawahi ona wapi mtu anaingia ukumbini tu kwenye harusi kisa ukumbi uko karibu na kwake?
Mwaliko lazima mkuu especially kwenye sherehe ingekua msiba kweli
 
Mkuu
Social life haifundishwi shule yeyote ile.

Badilika now or ever you will

Nimesoma between lines ya hoja yako inaonesha hauna good terms na jirani zako.

Badilika
 
Kama haujichanganyi sahau kuzoeleka si ajabu tangu uhamie umetembea baada ya gari kushindwa kufika nyumbani.

Kujichanganya ni kushiriki shughuli za kijamii kama mikutano, misiba na nyinginezo zinazowakusanya wanajamii pamoja.

Sijapewa mwaliko hata awe ni mtu tunafahamiana siwezi hudhuria.
 
Umeingia kwa nyodo za kishamba mtaa utakushinda

[emoji23][emoji23][emoji23] Halafu anasema amekuta shimo akagundua kwamba bomba limekatika na njia imefungwa, akaenda kwa mjumbe kwamba Kwann njia imefungwa bila yeye kupewa taarifa [emoji23][emoji23] jamaa mtemi sana. Tatizo lipo hapo. Ndio maana mjumbe akasema tutalifanyia kazi Halafu kamute.
 
Kwa maelezo haya, wewe ni ile aina ya majirani wanoko.
Uliopakana nao wana kazi ya ziada!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…