Kwanini jirani zangu hawanichangamkii?

Wahaya mna taabu sana kwahiyo hujui kosa lako ni nini hadi usawa huu? achenio mashauzi ishini na jamii vizuri.
 
Sijaelewa tatizo lako hasa ni majirani kutokuja kwenye tafrija yako bila kuwaalika au bomba la maji kupasuka kufanya njia isipitike?

Nahisi kuna hali fulani ya maisha umejiaminisha unayo tofauti na wenzio kutarajia watu wakupapatikie.
Kutopata attention uliyotarajia ndicho hasa kinachokuumiza mengine ni ngonjera tu.
 
Majiranii wale wanaoka kibarazani asubuhi mpaka jioni wanapiga majunga kula yenyewe ya Tabu unategemea Wakupende?? Unategemea wampende Mkeo?? Ni ngumu sana yani Ukiishi na waswahili wewe kidogo maisha yako yana Nafuuu amini Watakuchukia tu unaweza mpa mtu salamu anakaa kimyaa kama hajasikiaaa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] mjini hapa fanya mambo yako na usiumie wengine wakikuchukia maana sio shida zako labda kama wew bado hujajifunza una shobo nao.
 
bila kuwaalika Umeacha geti wazi waje waingie kama mbuzi,waliona ni dharau hizo "
nikaalika ndugu na marafiki zangu wa karibu"
 
 
Mimi sio mtemi lakini nina haki ya kupewa taarifa sijajua hapo unapoishi wewe maana huyu balozi anazo namba za wakazi wote wa eneo lake Incase Kuna shida kama hizi taarifa ni muhimu kutolewa mapema
 
Ishi na watu vizuri nyumba yako itashika moto ukiwa kazini na hawatafanya kitu.

Mimi nilipohamia huku nikitoka asubuhi simpiti mtu bila kumsalimia. Nikifika kwa mama wa vitumbua napunguza mwendo "habari za saivi jirani zangu" halafu nawaungisha vitumbua nakuja navyo kazini.

Vijiwe vyote nawasalimia hadi vijiwe vya boda boda nikipita napiga horn Piii, afu nawapungia na wao wanajibu piii piii piii piii. Daah raha sana.

Sichangamani nao kupiga umbea ila nashiriki nao matukio. Msiba ukitokea nitatoka kazini mapema nitaenda msibani. Sherehe zao nachangia na ninaenda.

Acha kuringa .
 


Ni kwenye msiba tu ndio mtu haalikwi na sio kwenye sherehe.
 
Teh!
 
Yani ndugu uwaalike alafu majirani wajilete tu kama wahuni?

Ungewaakika hata wawili watatu ungepungukiwa?
mashataka yake hayana mashiko yaani ufungue tu mlango kisa umepika pilau watu waje? majirani wanaalikwa tena one week before...hata wa5..swala la mabomba kupasuka kawaida na hao ni dwasco...alafu njia ni yake au ya mtaa?
 
mashataka yake hayana mashiko yaani ufungue tu mlango kisa umepika pilau watu waje? majirani wanaalikwa tena one week before...hata wa5..swala la mabomba kupasuka kawaida na hao ni dwasco...alafu njia ni yake au ya mtaa?
Tajiri kuhamia tu anataka mtaa mzima umshobokee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…