Watu makini wanaweza kutoa angalizo kwa Madam President kuhusu utenguzi wa mawaziri vipenzi wa hayati JPM. Ni vyema angewapangia majukumu mengine kabla kuanza kuibuka wingi wa manung'uniko kutoka kanda ile pendwa kwa nyakati hizo.
Mbali ya Chato, maeneo mengi ya kanda ya ziwa yalikuwa ndiyo kipaumbele cha JPM, jambo hilo lilimfanya aonekane shujaa wao. Alichagua mawaziri hawa kimkakati ili waweze kuwa karibu na watu wa kanda hii ili kuwaletea maendeleo.
Kanda hii ilianza kusikia viongozi wao wakiitwa "Sukuma Gang" na kushutumiwa vikali hata pale walipofanya makosa ya kawaida. Chochote kile walichokifanya kiwe chema ama kibaya, kikaanza kuonekana kama wanamkwamisha Mama kuelekea 2025.
Angalizo sasa ni kisije kutokea kile ambacho wengi hawatarajii. Ni kuhusu "sympathy" ya wananchi wa kanda hii juu ya viongozi wao kuanza kutengwa muda mfupi tu mara baada kifo cha JPM. Kanda hii inaweza kugeuka kuwa ndiyo ngome kuu na imara ya upinzani, na mwanzo wa kuelekea katika hitaji la siku nyingi la wapenda mabadiliko la kutaka kupigilia msumari wa mwisho katika jeneza la marehemu mtarajiwa CCM.