Kwanini kampuni ya Maboto haina Application Number ya mkopo katika mfumo wa ESS

Kwanini kampuni ya Maboto haina Application Number ya mkopo katika mfumo wa ESS

🔹 Kama hajajiunga saccos yoyote na haukopi saccos

🔹 Kama hata milango ya Benki zinazojulikana huzioni

🔵 Unajipeleka kwenye kitu kilichoandikwa " MICROFINANCE" ambazo riba zao Wana kufanganya kwa kukuambia ya mwezi badala ya mwaka.na tena unachukua huko mkopo wa miaka 9 na unafanya top up huko huko

🚮 Wewe huna miaka 5 kitu kiitwacho " magonjwa ya afya ya akili " kinakuhusu
Bora maboto kuliko bank, maboto ni 40% na inakua hivyo kweli bank wanakuambia 17% deni utakalokutana nalo kwenye salary slip hutaamin macho yako!
Et unajipeleka kwenye kitu kinaitwa microfinance, unajua kirefu cha bank ya NMB! Kuwa makini acha kukariri au labda we ndio unasumbuliwa na afya ya akili
 
Kiongozi mfumo unatambua tasisi ulizoomba mkopo tu kama ujaomba mkopo hiyo tasisis tembelea hiyo tasisi tambua mahitaji yao ukielewa watakupa taratibu zao baada ya hapo details za bank husika utaziona endapo utachukua mkopo kwao
Bado sio digital Sasa na umuhim was eloan. Haupo!!benki zote ziweke menu zao mle!tupate mikopi bila kwenda tawini!
 
Mimi kinacho nisikitisha kwenye mfumo was ess hakuna uainishaji wa benki zote Ili mteja achague na kujaza form Moja Kwa moja zaidi ya top up kwa wale tayari waliokopa tayari kwenye mabenki husika!!

Ess kwenye e loan kungekuwa na Benki kabisa kama nmb,crdb n k moja kwa moja unachagua mwenyewe na sio kuweka TU historian ya mikopo na topup tu!wangeweka hata BOT kabisa mtu anachagua anataka akope Benki gani kuliko kubandika mikopo Ile ile TU aliyokopa mtu!!
Mbona wameweka mkuu
 
Jina tu linasound ukurutumbi.
Ile ni kampuni ya kihuni. Haina leseni ya BOT, ndiyo maana hawauzi madeni. Mie wamenikera miaka miwili naomba balance wanarukaruka tu. Tena makao makuu Yao si pale Mwanza nadhani nyegezi. Wahuni tu. Yule anayejifanya meneja wao ukimpigia simu hata Sasa hivi anasema ametoka kikazi Yuko Arusha na kumbe Yuko buhongwa tu. Wenye mikopo Maboto kazi ipo.
 
Hizo taasisi za microfinance sijuwi maboto n nyingi zinaonekana kutokea kanda ya ziwa nk zimewaumiza watanzania wengi kwasababu ya changamoto wanazokutana nazo.Ajabu ni kwamba hakuna mtetezi aijitokeza kuzuwia uhuni wa hizi taasisi.
Kuna siku nimepita Wilaya ya Korogwe mkoa wa Tqnga nilishangaa sana kuona kila frem ina taasisi ya kukopesha(microfinance)KAUSHA DAMU/JINI/CHUMA ULETE nk zikiwa zimechipua kama uyoga.Nilitafakari sana.
Bank zilizo rasmi kama nmb,crdb nk mngetoa mikopo midogo midogo hata ya miezi SITA SITA ili kuuwa hizi kausha damu binafsi.
 
Hivi watumishi wa umma huwa hamsomi terms za mikopo mkazielewa? Mbona wafanyabiashara wengi ambao sio watumishi hawalalamiki? Au huwa mkiambiwa na hizo MICROFINANCE kuwa riba ni 4% kwa mwezi huwa hamjiulizi ni 4% ya Tsh ngapi? Mimi naona mpigwe tu hadi akili ziwakae sawa.
 
Bora maboto kuliko bank, maboto ni 40% na inakua hivyo kweli bank wanakuambia 17% deni utakalokutana nalo kwenye salary slip hutaamin macho yako!
Et unajipeleka kwenye kitu kinaitwa microfinance, unajua kirefu cha bank ya NMB! Kuwa makini acha kukariri au labda we ndio unasumbuliwa na afya ya akili
Duh! Ndugu mbona wewe ni mjinga sana? Mkopo wenye riba 40% unaurudisha kwa kufanya biashara gani? Halafu haujui kuwa kama ukilipa mkopo kwa muda mrefu riba inakuwa kubwa? NMB ina riba kuliko hizo kampuni uchwara. Tatizo nyie watumishi mnachukua mikopo ya kulipa kwa miaka hata zaidi ya mitano.
 
Bado sio digital Sasa na umuhim was eloan. Haupo!!benki zote ziweke menu zao mle!tupate mikopi bila kwenda tawini!
Nadhani mfumo unaitaji afisa kwa awamu ya kwanza details zako ziingizwe na afisa utumishi baada ya hapo ndio unaweza jihudumia mfano top up na mambo ya repayment,, pamoja na hayo tuipongeze serikali kwani imeondoa umimi wa kubembelezana kuhusu repayment na kuchomekeana riba kubwa nje ya utaratibu wa B.O.T
 
Hizo takataka zote, lazima uwe na shida kwenye afya ya akili ndio ukope huko.
Kiongozi hata hizo tasisi unazoziamini milikuwa mnapigwa shukuru mfumo wa ess unaenda ondoa hizo janja za mafisa mikopo kuna pesa kibao mlikuwa mnawachia wao wanakula mgao na mafisa utumishi
 
Ile ni kampuni ya kihuni. Haina leseni ya BOT, ndiyo maana hawauzi madeni. Mie wamenikera miaka miwili naomba balance wanarukaruka tu. Tena makao makuu Yao si pale Mwanza nadhani nyegezi. Wahuni tu. Yule anayejifanya meneja wao ukimpigia simu hata Sasa hivi anasema ametoka kikazi Yuko Arusha na kumbe Yuko buhongwa tu. Wenye mikopo Maboto kazi ipo.
Kiongozi walikuwa hawauzi kwa sababu ya hii janja ambayo tumeiona kwenye mfumo maaana mfumo wa ess kwa sasa unakupa option ya kusettle deni na kujua kiasi unachotakiwa kulipa sasa maboto wao hawana application namba maana yake nini kuna uhuni ulifanyika hazina wakawapokea na ndio maana ukiwafuata maboto mettle deni wanazingua kwa sababu wakisema wakube deni halisi ukalipa mfumo utagoma kufuta deni lote kwa sababu mfumo hautambui deni halisi na deni la riba na ndio maana ukiwafuta mfute deni wanaitaji ulipe mpaka deni la riba ya miaka mitatu kwanini usajiri wao hazina wakihuni
 
Kiongozi hata hizo tasisi unazoziamini milikuwa mnapigwa shukuru mfumo wa ess unaenda ondoa hizo janja za mafisa mikopo kuna pesa kibao mlikuwa mnawachia wao wanakula mgao na mafisa utumishi
Kwenye mfumo wa Ess siwaoni Lestshego,Bay port,maboto
 
Maboto ni mpuuzi 1 nasali nae jumuia moja hapa Nyasaka centre Mwanza lakini hajitambui daraja lipo mbele ya nyumba yake limeanguka Kama halioni amebadili njia now anapita nje kwangu daily na Corolla yake old model baada ya Machina wa mabondo kujenga daraja jingine ni fedha za ndagu anakopesha wakopaji wanalia hazina maendeleo zaidi ya kuuziwa vitu vyako....Nyambafu zake na zao wakopaji
 
Duh! Ndugu mbona wewe ni mjinga sana? Mkopo wenye riba 40% unaurudisha kwa kufanya biashara gani? Halafu haujui kuwa kama ukilipa mkopo kwa muda mrefu riba inakuwa kubwa? NMB ina riba kuliko hizo kampuni uchwara. Tatizo nyie watumishi mnachukua mikopo ya kulipa kwa miaka hata zaidi ya mitano.
Mkuu mm sio mjinga kama unavyodhani, nilikopa tsh 17,000,000 NMB, baada ya salary kucheck natakiwa kulipa tsh 25,330,000 sasa hiyo ni %ngapi? hata hizo taasisi tunazoziamini zina riba kubwa tu.
Kuchukua mkopo kwa muda mrefu au mfupi ni kulingana na mahitaji yako maana muda mfupi mkwanja kidogo riba ndogo, muda mrefu mkwanja mrefu riba kubwa hapo kazi kwako.
 
Ilikua kwa muda gani?
 
Back
Top Bottom