Kwanini Kanisa Katoliki hawavunji Mkataba wa Fedha MoU?

Kwanini Kanisa Katoliki hawavunji Mkataba wa Fedha MoU?

KANISA KATOLIKI KWANINI HAWAVUNJI MKATABA WA FEDHA ZA MOU?

Katika hati hiyo, iliyotiwa saini Februari 21, mwaka 1992, upande wa serikali uliwakilishwa na mmoja wa mawaziri wake waandamizi wa wakati huo.

Makubaliano hayo yalifanyika kwa kuzingatia mambo kadhaa, ambayo ni pamoja na hali ya uchumi nchini kutomudu kuiwezesha serikali kutoa huduma za elimu na afya kwa kiwango bora.

Msingi mwingine wa makubaliano hayo ni makanisa kuhakikishiwa kuwa serikali itaweka mazingira mazuri kwao kutoa huduma za elimu na afya.

Makubaliano hayo yamegawanywa katika maeneo makubwa mawili, ambayo ni sekta ya elimu na afya na kila sekta ikiwa imetengenezewa bodi yake ndani ya mtandao wa makanisa kupitia CCT na TEC.

Kwa mfano, sehemu ya kwanza ya hati ya makubaliano hayo, kifungu cha kwanza, kinaeleza kuwa makanisa yataanzisha kamisheni ya uratibu wa utoaji huduma hizo.

Katika kifungu hicho cha kwanza, sehemu ‘a’ hati hiyo inaeleza kuwa jukumu la kamisheni hiyo ni kuandaa sera zinazohusiana na huduma za afya na elimu zinazotolewa na makanisa.

Kifungu kidogo cha nne, sehemu hiyo ya kwanza ya hati hiyo, kinaeleza kuwa kamisheni hiyo itakuwa ikiratibu na kusimamia matumizi ya fedha, mikopo kwa ajili ya kuboresha huduma za elimu na afya.

Hati hiyo pia inaeleza kuwa wajumbe wa kamisheni hiyo watatoka katika CCT na TEC na mashirika wafadhili na kwamba ni lazima shughuli zote ziendeshwe kwa mujibu wa sera na sheria za nchi.

Serikali kupitia hati hiyo pia imekubaliana na makanisa kuanzishwa kwa Mfuko wa Huduma za Kijamii ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kupokea mikopo na misaada.

Pia kwa upande wa elimu, serikali ilikubali kutoa nafasi za masomo ya mafunzo wa ualimu kwa wanafunzi wa ualimu.
Serikali imezuhiwa na nani kuuvunja mkataba huo?
 
Wananchi wanata reforms na katika reforms hizo basi makanisa yasipewe fedha zao wananchi

Fedha zao wapewe wenyewe kila kijiji kila kata kama ruzuku kwa ajili ya kujiletea maendeleo

Makanisa yana vyanzo vingi vya mapato kulingana na katiba zao alafu tunawapa manoti ya kazi gani?
Hizo hela unawapa wewe na nani mzee?

Swali dogo tu,unadhani huo mkataba ungekuwa mbovu kama mnavyotaka kuiaminisha jamii hapa ungekuwa hai mpaka leo?kwanini usivunjwe au serikali isipanue wigo kwa kuwaingiza wengine (waislam ) wenye interest nao?
 
Sisi wananchi tunata uvunjwe.

Swali dogo huo mkataba unao hapo?
 
Sisi wananchi tunata uvunjwe.

Swali dogo huo mkataba unao hapo?
Nikuulize wewe unaesema upo na kwamba uvunjwe,yupo mwenzako huko juu amedai anao nimemwambia aupandishe hapa amekimbia.
 
Serikali mbona inajenga misikiti je huoni? Misikiti kwenye maeneo ya serikali, nenda Ferry, nenda Coco Beach, nenda kwenye masoko mbalimbali ni Kodi zetu zinajenga misikiti hiyo
Malaria ana udini kama bibi yake Mozilla FireFox ,anashindwa kutambua kwamba serikali ya JMT haina dini.

Huyo nilichogundua ni UDINI tu umejaa wakati hizo shule na hospital wanatibiwa hadi waislam na wanasoma pia waislam wenzao.

Kukosa cathoric asingesoma ,angeishia kumeza juzuu 30 tu.
 
Kama ni hivyo mbona makanisa yanaulumu huduma mbovu za afya wakati wanachotewa mabilion ya fedha hata CAG hayakaguwi
 
Mbona kuna sehemu ambazo wakati wa JPM, serikali ilijenga hospital zake na kuachana na za dini
Hospital kubwa,kcmc,bugando,ndanda, hospital kama muhimbili, benjamin mkapa hutoziona mwanza,moshi,mtwara
 
Kama ni hivyo mbona makanisa yanaulumu huduma mbovu za afya wakati wanachotewa mabilion ya fedha hata CAG hayakaguwi
Hayo mabilioni yanapelekwa kwa ajili ya nini? Nadhani haujui dhumuni la hiyo MOU?
 
Back
Top Bottom