Shida nyie mnataka wakatoliki waendelee na trend zenu za kihuni
Kitu ambacho hujui katika ukatoliki kila kitu kinatiliwa maanani kwa uzito wake na utaratibu wake. Katika kanisa katoliki Kuna warsha, na semina na makongamano mbalimbali yanayohusu malezi, uchumi, huduma za kufunguliwa kiroho, makusanyiko ya watoto, vijana, akina mama, wababa, wazee, wanandoa, waseja, wajasiriamali na kadhalika
Kwahiyo kanisa katoliki linapokuambia njoo upate mafanikio sio kwa maombi tu Bali maombi na njia za kufuata kufikia hayo mafanikio. Na katika hizo warsha ambazo husimamiwa na makasisi au wasomi huduma za maombezi ni muhimu ambazo huambatana na huduma kamili za maisha ya watu na sio maombi tupu ya mdomo ndiyo maana tunaona haya makanisa ya mabati na mahema ni kama wahuni tu, wanawaombea watu sawa je mnawaonyesha njia ipi wachukue ili maombi yakaimarishe hizo njia?
Mimi binafsi tangu udogo nimelelewa katika utoto mtakatifu, viwawa, vyama kadhaa vya kitume na Sasa Niko pamoja na UWAKA na huko kote nimefanikiwa kutanua fikra bila kuruka hatua.
Mafanikio hayana miujiza ni mchakato ndo maana waSwahili husema kazi na sala au mnataka Sasa na wakatoliki nao waanze kufanya promo kwenye maredio na tv "ooh njoo ufunguliwe, njoo upokee" upokee kutoka kwa nani aliyevitelekeza?
Mnaibiwa sana ndugu zetu kwa kupenda mkato mnadanganyana huko kuwa wakatoliki hawana upako, hawaombei kwahiyo mnataka faragha za huduma za kiroho nazo ziambatane makamera na voice tapes si ndiyo? Huo ni uhuni na uigiza tu kama wa akina mkojani?
Sisi tuna akili kuliko nyie ndo maana hatuwezi kufanana njia