Kwanini Kanisa Katoliki linahamasisha umaskini na halitaki kabisa watu waponywe na maradhi? Au wanafaidika nao

Shetani alimjaribu Yesu kupitia utajiri. Kuna uhusiano mkubwa kati ya utajiri na shetani upande mmoja; na ufukara, msalaba na Kristu upande mwingine.
We jamaa bhana......aliekuambia utajiri lazima uwe na uhusiano na Shetani ni nani ?...hata wafuasi wa Kristo wameahidiwa baraka na Utajiri.

2 Wakorintho 8:9
Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
 
Ukisikiliza mahubili ya maaskofu wa kanisa katoliki au mapadre, wanapiga vita sana wachungaji wanaowaombea watu kufanikiw kifedha au maisha kiujumla. Kwa sasa maaskofu wote wa katoliki wamemlia kolabo mwamposa. Mahubili yote ni yeye.

Wanaponda sana kwamba kwa nini anawaombea watu wafanikiwe. Na watu wanazidi kumiminika sana kwake which means wanaponywa na wanafaidika.

Ushauri wangu kwa maaskofu au mapadre, hubirini injili ya kweli na watu watawafuata msitumie nguvu mtaaibika
Katoliki wanasaidia kuondoa watu katika ujinga na upotofu. Mafanikio ya kweli hayapatikani kwa kuombewa na mitume na manabii wa uongo, bali ni kufanya kazi kwa kujituma na bidii mafanikio yatapatikana. Uliza nchi tajiri ulimwenguni oa utajiri wao unatokana na maombi ya akina Mwandosya
 
Kuna utofauti mkubwa sana kati ya "lazima" na "uhusiano mkubwa".

Marko 10:25
"Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.
 
Hawajiulizi ni kwa nini hao wanaojiita mitume na manabii wanahangaika (wanafanya kazi) kuandaa mahubiri badala yake kumbe nao pia wangefanya maombi kujiombea? Kwani wao hawautaki utajiri au wamekatazwa kuwa matajiri ?
 
Kanisa katoliki ni taasisi ya umilele kanisa lipo hadi mwisho wa dunia.
Mwamposa sio taasisi hata miaka 10 ijayo hawezi kuwepo
 
Nani keshawai pata utajiri wa miujiza bila kazi.
Afanyacho Mwamposa ni ishu za manifestation ambayo hata wewe unaweza.
Manifestation ni hali ya kuziamsha hisia zako za ndani ili utende.
Laana na baraka vyote vipo ndani ya mtu mwenyewe ye ndie anachagua awe masikini au tajiri.
Mwanadamu kapewa freewill
 
Ni falsafa walizotoa kwa philosophers wakigiliki ambao kuna kipindi walikuwa na influence kubwa kwa mapapa kuliko Biblia.

Yesu alifanyika masikini ili sisi tulio masikini tupate kuwa matajiri. Huu mstari hawawezi kuusisitiza.
Hakumaanisha umasikini wa mali
 
Wakati babu zake Mwamposa wanaabudu mizimu kanisa katoliki lipo na linaendelea na shughuli zake
 
Ukisikiliza mahubili ya maaskofu wa kanisa katoliki au mapadre, wanapiga vita sana wachungaji wanaowaombea watu kufanikiw kifedha au maisha kiujumla. Kwa sasa maaskofu wote wa katoliki wamemlia kolabo mwamposa. Mahubili yote ni yeye.

Wanaponda sana kwamba kwa nini anawaombea watu wafanikiwe. Na watu wanazidi kumiminika sana kwake which means wanaponywa na wanafaidika.

Ushauri wangu kwa maaskofu au mapadre, hubirini injili ya kweli na watu watawafuata msitumie nguvu mtaaibika
Na wewe nenda ukaombewe uwe tajiri
 
Kuna utofauti mkubwa sana kati ya "lazima" na "uhusiano mkubwa".

Marko 10:25
"Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.
Kuna uhusiano mkubwa Sana kati ya Utajiri na kumfuata Kristo.

Mithali 8
17 Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.

18 Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia.
 
Back
Top Bottom