Kwanini kataa ndoa wengi ni vijana wa kikristo

Kwanini kataa ndoa wengi ni vijana wa kikristo

Gol D Roger

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2023
Posts
2,316
Reaction score
6,082
Ngoja tu nianze kwa kusema, This is all "Allegedly".

Observation yangu ni kwamba vijana wengi wa kataa ndoa asilimia kubwa ni vijana wa kikristo, au wana background ya kikristo au ni atheists.

Yes kila mtu ana experience zake but kwa mm, watu ambao nime interact nao(kweny mada za ndoa na mahusiano) watu ambao hawana imani au hawamini katika taasisi ya ndoa, karibia wote ni wakristo, ngoja tu niseme ukweli, sio "karibia wote", wote ni wakristo, sijajua kwa experience yenu, but for me huo ndio uhalisia.

Mimi ni mkristo na hii trend inanifikirisha sana, why is this so??
Je, ni malezi ya wazazi wa kikristo?
Je, ni mafundisho ya kikristo??
Ni kitu gani kimechangia kuwa hivi?

Katika vitu ambavyo hawa wenzetu waislamu nawapongeza sana, ni kwamba bado wana imani sana na taasisi ya ndoa, ni nadra sana kukuta kijana wa kiislamu anakwambia hatooa au haamini katika ndoa, au anasema "ndoa ni utapeli", wapo very optimistic kweny maswala ya ndoa, na wengi wao wanatamani kuoa na kuolewa mapema.

Kama una idea yoyote ebu tuambizane kwann hii ipo hivi?

Angalizo;
Sina data wala takwimu yoyote, ni kitu tu ambacho nimeki-observe kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki.
 
Nyumbu huwa wanamfata yule wa mbele hata kama anaelekea shimoni wapo nae mpaka wote watumbukie.

Sio jambo baya kua tofauti na majority, waislam wako strictly sana wao ni dini kwanza, wakristo hawakazii sana mawazo huru.

Pia waislam wana option ya kuacha(talaka) chap mambo yakienda kombo,wakristo talaka zao ni kipengele.
 
%kubwa ni wazinzi... Wazinifu wanajificha kwenye kichaka Cha ulokole. Mzinzi anawezaje kihusudu ndoa? Wao vichwani mwao wanaangalia negatives za ndoa tu... Jua likishazama ndio wanaowaza kwamba mwanzo nilikuwa wapi... Kijana ukisha vuka umri 25yr hakikisha mipango ya familia umeianza kinachofata tazamia kutafuta sehem ya kudumu ya kustiri mbavu zako na kizazi chako hatua ya tatu Jenga future ya kizazi chako baadae hapo najua utakuwa umeshagonga 35yrs+
 
wanawake wengi wa kikristo wameelimika,much know,businesswoman,feminist,independent etc hawaoni umuhimu wa ndoa wanajiona wamepata sasa matokeo yake treatment ya ndoa inakuwa ni third priority usishangae hata nabii akathaminiwa kuliko mume wa ndoa.
OUTPUT:
Watoto wanakuzwa katika malezi ya kuigiza mwisho wanawaathiri psychologically bila wao kujua (trauma)
 
Binafsi mimi sio kataa ndoa ila niii yani bado bado au tuseme badooooooooo sana. Sijapata fomla ya kuhendo vidada ambavyo havina mwili .na ndo ntaoa kwa baadaeeeeee.
 
Kikawaida wakristu wengi pia huchelewa kuoa kwa sababu ya "ndoa ya mara moja pasipo talaka" Lakini pia gharama za harusi, send off plus kitchen party..

Halafu pia jamii za kiislamu nyingi ni za pwani ambazo bado zina ujamaa kiasi mtu akishindwa kuoa anaweza kutolewa mahari na wanandoa wakaishi ukweni kwa muda. Ila wakristo wengi wanatokea jamii za bara ambazo ujamaa ni mdogo hivyo ukiyavagaa majukumu. Watu kukutelekeza ni dakika

Sababu zipo nyingi Ila kwa uislamu ndoa ni nyepesi zaidi sio kwa kuingia ama kuachana. Kwa wakristu ni tofauti ndio maana wengi wanachelewa
 
Thanks
 
Ndoa zao ni ndoano ukimeza umekwenda na maji. Mwanamke anaweza kuficha make changes yake akiolewa tu ndio kila rangi utaiona anajua hakuna kuachana milele wengi wanaishi kwenye mateso makubwa
 
%kubwa ni wazinzi... Wazinifu wanajificha kwenye kichaka Cha ulokole. Mzinzi anawezaje kihusudu ndoa? Wao vichwani mwao wanaangalia negatives za ndoa tu... Jua likishazama ndio wanaowaza kwamba mwanzo nilikuwa wapi... Kijana ukisha vuka umri 25yr hakikisha mipango ya familia umeianza kinachofata tazamia kutafuta sehem ya kudumu ya kustiri mbavu zako na kizazi chako hatua ya tatu Jenga future ya kizazi chako baadae hapo najua utakuwa umeshagonga 35yrs+
Kwenya uzinzi hakuna kuchekana mkuu. Siku hizi access ya ngono ni kubwa na wengi wanajifunza mapema.. Kwa hiyo kinachotenganisha nadhani ni urahisi wa ndoa za kiislamu na jamii zake kuweka dini na maisha ya kijamii ikiwemo ndoa kama kipaumbele kikubwa.
 
Sema nasumbuliwa sana kuhusu ndoa ,unakut mtu anakuambia umri huo haujaoa halafu ni wewe muislamu 😅 kijana anayeniambia hajaoa kanizidi mwaka mmoja kisa yeye ni mkristo.

Ila tusiwe biased sana kwenye dini ,tufanye mambo mazuri ya kumpendezea Mungu kwa pamoja ...Tushikane mikono jamani.
 
Back
Top Bottom