Kwanini katika wanasayansi wakubwa hakuna mwanamke hata mmoja?

Kwanini katika wanasayansi wakubwa hakuna mwanamke hata mmoja?

Kisaikolojia sisi wanaume ni watu wa Material world, tunapenda Vitu, ndio maana mambo ya Field kama Engineer wapo wengi.

Wanawake ni Emotional wanapenda zaidi watu kuliko Vitu, btw University ya kwanza Duniani ilianzishwa na Mwanamke.
University(universe knowledge) ya kwanza duniani ni Timbuktu ila sina uhakika kama ilianzishwa na mwanamke, maana kabla ya hapo Haku kuwa na university kulikuwa na gnotics temples for spiritual knowledge japo ndo huko Sayansi ilipoanzia
 
Unamfahamu mume wake Pierre Curie aliye mpush mpaka kufanikiwa kupata hiyo nobel?
Marie Curie kamkuta Pierre utafiti wake umejikita kwenye Crystals ndiyo akambadilisha na kuhamia kwenye radioactivity. Siyo sahihi kusema kwamba eti ni Pierre ndiye alimpush Marrie katika utafiti wake. The woman was workaholic and totally committed to her research. Naam! Ndiye mwanamke wa kwanza kupata Ph.D ya Fizikia Sorbonne....na kufundisha pia!

Unafahamu kuwa Marie Curie alipata zawadi ya Nobel nyingine miaka mingi baada ya mumewe kufariki? Mpaka leo bado anashikilia rekodi ya kuwa mwanamke pekee aliyewahi kushinda zawadi hiyo mara mbili?

Na utafiti wake na binti yake Irene katika Kemia nao ukaja kumpatia Irene Nobel nyingine?

This is one of her best biographies. A true giant of Science! 👇👇👇

20230602_195329.jpg
 
Fuatilia mnipe majibu !! Mie sijaelewa?

Wewe hiyo orodha umeitoa wapi? Wewe ni 'scientist'?Ulishawahi kumsikia Madam Curie? Huo ni mfano mmoja tu, wapo na wengine.

Lakini pia usisahau 'mfumo' dume. Huu haukuanzia huku kwetu tu, ilikuwa ni dunia nzima. Ni mwanamke gani angeacha kulea watoto nyumbani, kufua nguo na kupika, halafu aende kukesha ndani ya maabara.
 
sio mfumo dume ni majukumu
 
Mbona hata majenerali wa majeshi duniani hakuna wanawake hata China wala Urusi hata US hakuna raisi mwanamke hadi leo? Acheni kulazimisha mambo mwanamme ni mwaname na mwanamke ameumbwa hivyo kiaslii
Hapana mkuu 'Mzalendo Halisi', hili la "mwanamke ni mwanamke na mwanamke ameumbwa hivyo kiasili", ni dhana potofu sana kutoka kwa mtu mwenye uelewa kama wewe.

Nikukumbushe tu, siyo wanaume wote ni hodari katika nyanja mbalimbali au zote. Hawa wanaume wasiokuwa na uwezo katika nyanja fulani, lakini mwanamke akaiweza na wao tusemeje?

Hizi 'declarations' za jumla jumla namna hii zinawafaa wasiokuwa na akili timamu kichwani.

Ndiyo, kama rais mwanamke ni mbovu, tuchukulie ubovu huo kuwa wa kwake, na wala siyo wa wanawake wote.
 
sio mfumo dume ni majukumu
Wewe yachukulie hivyo unavyotaka, lakini hali ndivyo ilivyokuwa toka huko zamani, na kama huoni uhusiano wa mambo hayo na hili swala unalotaka lijadiliwe kwenye mada yako hii, basi utakuwa una 'a presumptive notion' juu ya swala lenyewe.

Haya, tuhamie kwa mtu mweusi (mwanaume), yeye majukumu yaliyozuia asiwemo kwenye orodha hiyo nayo utasema ni majukumu yaliyomhusu, au siyo? Naogopa hata kuyataja hayo majukumu.

Mkuu hayo ya 'Wiki' uliyoniwekea huko, tulishapita siku nyingi mno kwenye 'level' ya namna hiyo.
 
Fuatilia mnipe majibu !! Mie sijaelewa?

Huyu hajui historia ya sayansi. Marie Curie alikuwa mwanamme? Au Ada Lovelace naye alikuwa mwanamme? Inawezekana hata hajui Noether's Theorem ni kitu gani kwani pia angejua kuwa Emmy Noether alikuwa ni mwanamke.
 
Fuatilia mnipe majibu !! Mie sijaelewa?

Mkuu 'Zalemba', siku nyingine lete mada hii hii ukihoji mtu mweusi (mwanaume au mwanamke) kutokuwemo kwenye orodha hiyohiyo uliyoiweka hapo (kwenye mada yako ondoa tu 'mwanamke', na badala yake weka mtu mweusi.
 
Unamfahamu mume wake Pierre Curie aliye mpush mpaka kufanikiwa kupata hiyo nobel?
Pierre yeye alivumbua kifaa cha kupima Charge, Marie akatumia kifaa hicho kufanya ugunduzi wa radiacative materials. Walipublish paper yao pamoja lakini mgunduzi mkuu alikuwa Marie.
 
Pierre yeye alivumbua kifaa cha kupima Charge, Marie akatumia kifaa hicho kufanya ugunduzi wa radiacative materials. Walipublish paper yao pamoja lakini mgunduzi mkuu alikuwa Marie.
Bila kutumia hicho kifaa angewezaje?

Ndio maana kwenye hiyo rekodi wanatajwa wote wawili

Kwenye crystal anatajwa Perrie na kaka yake mkubwa.

Yani kiufupi alikuwa jamaa ambaye alikuwa ni cooperative sana
 
Bila kutumia hicho kifaa angewezaje?

Ndio maana kwenye hiyo rekodi wanatajwa wote wawili

Kwenye crystal anatajwa Perrie na kaka yake mkubwa.

Yani kiufupi alikuwa jamaa ambaye alikuwa ni cooperative sana
Wanatajwa wote wawili kwa vile Marie alikuwa main author na Pierre alikuwa coauthor wa paper iliyowapa umaarufu.

Kutengeza kifaa ni tofauti kabisa na kukitumia kugua jambo jingine lisilokuwapo. Kwa mfano, aliyegundua kifaa cha kupima charge kwenye waya ni Coulomb lakini Ohm alikitumia kifaa hicho kugundua Ohm's Law na wala Coulomb hawjawahi kupewea credit yoyote kwenye Ohms Law.
 
Ni ngumu wanawake kuwa kwenye hiyo orodha kwanza walikuwa awaruhusiwi kusoma elimu ya juu hadi 19th century.

Wachache waliotoka familia bora na kuonyesha uwezo; wazazi wao waliwatafutia walimu wa kuwafundisha. Mfano Madame Lavoisier anamchango mkubwa kwenye chemistry.

Wengine walifanya makubwa as assistants kwenye research michango yao ikatumika na wengine; mfano Henriëtta Swan Leivety, yeye ndio wa kwanza kugundua variable stars na kuona kuna nyota nyingine zipo mbali sana na Milky Way galaxy. Kazi iliyosaidia ‘Edwin Hubble’ kugundua galaxies zingine.

Cecilia Payne, aligundua pulsurs; ambayo ilipelekea mtu mwingine kuchukua Nobel prize. Ila nadhani baadae alipewa due credit zake. Kuna ‘Mileva Maric’ mke wa kwanza wa Einstein na yeye alikuwa physists kamsaidia sana Einstein kwenye research na kufanya calculations zake apewi credit, mumewe akuwa mzuri kwenye hesabu.

Halafu kuna wengine wanasimama wenyewe; kama ‘Rosalind Franklin’ mvumbuzi wa DNA and several others.

Hiyo list ni choice tu ya huyo jamaa maana kuna wanaume wengi tu hapo awapo pia ambao ni giants kwenye dunia ya science hasa physics.
 
Wanatajwa wote wawili kwa vile Marie alikuwa main author na Pierre alikuwa coauthor wa paper iliyowapa umaarufu.

Kutengeza kifaa ni tofauti kabisa na kukitumia kugua jambo jingine lisilokuwapo. Kwa mfano, aliyegundua kifaa cha kupima charge kwenye waya ni Coulomb lakini Ohm alikitumia kifaa hicho kugundua Ohm's Law na wala Coulomb hawjawahi kupewea credit yoyote kwenye Ohms Law.
Lakini kwenye radioactive credit zinaenda kwa wote mume na mke na huku Pierre akitajwa mara nyingi
 
Back
Top Bottom