Kwanini Kenya inapendwa na wazungu ilihali tumezidi vivutio?

Kwanini Kenya inapendwa na wazungu ilihali tumezidi vivutio?

Nyie wakati mnashangaa flyovers enzi za Magufuli Kenya walikuwa nazo tangu enzi za Kibaki, halafu Kenya majimbo mengi tu yana flyovers tofauti na bongo ambapo ni Dar tu.
Jomo Kenyatta Airport ulikuwa uwanja mkubwa kimataifa kuliko Dar es Salaam muda mrefu sana.
Kenya ndio imekuwa nchi ya kwanza kuwa na SGR Africa Mashariki.

Jamaa walikua mbele ya muda kitambo. Ndo faida ya kuwaacha wakoloni muda mrefu
 
Kenya imekuwa ikipendwa na wazungu kwa sababu si tu ina vivutio, bali imewekeza sana kwenye marketing ya utalii (mfano “Magical Kenya”), ina miundombinu bora ya kufika kwenye mbuga na hospitality industry yao ilikomaa mapema kwa hoteli na tour companies za kiwango cha juu. Pia Nairobi ina urithi wa old money tangu enzi za kikoloni, familia za wazungu wenye mashamba makubwa, hoteli na clubs za kihistoria kama Norfolk na Muthaiga, pamoja na safari lodges zinazouza “colonial elegance.” Zaidi ya hayo, Nairobi ni makao ya mashirika makubwa ya kimataifa na UN, hivyo ina expat community yenye ladha ya old money lifestyle (golf, polo, private schools) jambo linalowafanya wazungu wajisikie wako karibu na mfumo wanaouzoea.
 
Ukimuuliza mzungu what is your favourite country in East Africa anakujibu Kenya wakati ukiangalia sifa nzuri tumewazidi.tukiacha hali za kisiasa ila kuanzia vivutio na historia yetu ni ya kuvutia halafu wakenya makauzu makauzu Sana yaani hata wanavyoongea kwa Ku shout tofauti na Sisi tuko calm kwenye negotiations.. What's the extra about Kenya?
Mtoa mada na wengine humu hizi ni data za zamani, tushawapita wakenya kwa case ya Vivutio vya utalii na ku attract watalii.

Zamani enzi ambazo hakuna utandawazi Kenya walikua maarufu na walitupita source za habari zilikua magazeti, TV etc.

Siku hizi Enzi za Google kila mtu anajua Kilimanjaro, serengeti, Ngorongoro etc zipo wapi.

Mwaka 2024 Kenya walipata watalii wa nje Milioni 2.5 na mapato ya 400 billion ksh, hela za madafu Takriban Trilioni 8.

Mwaka 2024 Tanzania imepata watalii wa nje 1.7M na mapato ya 3.25B Usd sawa na hela za madafu Trilioni 8.4

Hivyo wazungu (na wageni wa nje kwa ujumla) waliingizia Tanzania Bilioni 400 zaidi kuliko Kenya kwa mara ya kwanza kabisa. Hivyo si kweli kwamba wao sasa hivi wametuzidi.
 
Hesabu gani hizi? Yani watalii milioni 1.7 waingize pesa nyingi kuliko watalii milioni 2.5??
 
Wazungu wakiamua upo mwaka waliwapigisha watu kura eti kuushindanisha Table Mountain na Kilimanjaro nilishangaa sana kwa kweli na baadae huo Table Mountain ukaja kushinda wazungu sio watu wakiamua jambo lao watashinda tu..
 
Huwezi kuwa bora kwa chochote kama unataifa lenye misingi mibovu ya kishenzi na linaendeshwa kishenzi na mataahira kama Tanzania, nchi inanuka ignorance na upuuzi, mtalii ana anzaje kuja huku , research zenyewe tu zinaonyesha kuwa hata hao watalii wachache wanaokuja huwa wana experience huduma mbovu na hawarudi tena nchi hii.
Kuwa na vivutio vingi vya utalii si sababu ya kuwa kinara kwa kupata watalii wengi , yaani ni sawa na kuwa na mali nyingi za urithi na huna akili .Utakuwa failure Tu
 
Hesabu gani hizi? Yani watalii milioni 1.7 waingize pesa nyingi kuliko watalii milioni 2.5??
Unahisi mtalii toka Burundi na mtalii toka Norway wanalipa sawa?

Kenya wana Attract sana watalii wanao ongea kingereza kama Usa na UK, wametupita ila linapokuja Nchi ambazo hazitumii kingereza kama Ufaransa, Italy, Urusi, Poland etc tumewapita sana.

Pia Tanzania kuna vivutio ambavyo ni premium watu wanalipa pesa ndefu, sehemu kama Thanda ipo top 10 Dunia nzima kwa hotel zenye Gharama. dola 33,000 kwa siku kwa kichwa kimoja na unakuta kuna msururu wa Booking.

Hapo bado premium service Nyengine Serengeti na Ngorongoro ambazo zinajulikana worldwide na "Elites", ni rahisi kumdanganya kayumba wa Usa na Uingereza kwamba Kilimanjaro ipo Kenya ila huwezi wadanganya hao Elites ambao wanajua kabisa Serengeti ni real deal.
 
Hivi ni kweli Kenya imetuzidi miundombinu?
sana tu, kwa mfano tafuta barabara zenye lami kenya ni nyingi kuliko kwetu ilihali kwa eneo ni kenya ni ndogo kuliko kwetu; Wana mashule mengi na pia wameimarisha shule zao za serikali ndio bora zaidi kuliko za binafsi, Wana hospitali nzuri nyingi, wana wafanyakazi wanaojituma sio hawa wa kupiga blaa blaa; wana wasomi wengi, wana viwanda vingi, wanakusanya kadi nyingi sana ukilinganisha na sisi nk nk nk
 
Juzi Ruto kaipongeza Tanzania tumewapita tayari kwenye East Africa inter trade, kifupi sasa hivi East Africa Yote Tanzania ndio anaongoza kusuplly majirani,

Kuhusu Barabara pia tumewapita hizi nyuzi za zamani ila pitia

Hospitali pia tumewapita, wana Hospitali nzuri chache za wenye pesa ila Hospitali za wala la hoi Tanzania ipo juu ndio maana wakenya wengi huja Tanzania Kutibiwa...

Fanya homework yako vizuri
 
Ukimuuliza mzungu what is your favourite country in East Africa anakujibu Kenya wakati ukiangalia sifa nzuri tumewazidi.tukiacha hali za kisiasa ila kuanzia vivutio na historia yetu ni ya kuvutia halafu wakenya makauzu makauzu Sana yaani hata wanavyoongea kwa Ku shout tofauti na Sisi tuko calm kwenye negotiations.. What's the extra about Kenya?
Because of historical relationship between Kenya and Europe especially United Kingdom.
Wants more?
 
Ukimuuliza mzungu what is your favourite country in East Africa anakujibu Kenya wakati ukiangalia sifa nzuri tumewazidi.tukiacha hali za kisiasa ila kuanzia vivutio na historia yetu ni ya kuvutia halafu wakenya makauzu makauzu Sana yaani hata wanavyoongea kwa Ku shout tofauti na Sisi tuko calm kwenye negotiations.. What's the extra about Kenya?
Kenya ni nchi inayoabudu wenye pesa.

Kenya imewawekea mazingira mazuri wageni wa Kenya kuishi kama kipaumbele cha kwanza.

  • Wanapata vibali vya kuishi kirahisi (residency permits)
  • Wanaweza kupewa uraia bila kukana uraia wao, dual citizenship
  • Wanaruhusiwa kumiliki ardhi watakavyo
  • Nairobi kuna apartments nyingi sana mazingira mazuri ya wao kuishi.
  • Nairobi kuna MALLS, RESTAURANTS, HQ za Makampuni ya teknolojia mengi kwahiyo hawahangaiki sana
  • Wakenya wengi wanajituma kujua Kiingereza, kwahiyo ni rahisi wazungu ku-integrate, hakuna language barrier.
 
Juzi Ruto kaipongeza Tanzania tumewapita tayari kwenye East Africa inter trade, kifupi sasa hivi East Africa Yote Tanzania ndio anaongoza kusuplly majirani,

Kuhusu Barabara pia tumewapita hizi nyuzi za zamani ila pitia

Hospitali pia tumewapita, wana Hospitali nzuri chache za wenye pesa ila Hospitali za wala la hoi Tanzania ipo juu ndio maana wakenya wengi huja Tanzania Kutibiwa...

Fanya homework yako vizuri
Ungefanya homework yako ungejua Kenya kwa ukubwa ni kama nusu tu ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom