Kwanini Kenya inapendwa na wazungu ilihali tumezidi vivutio?

Utalii wa kuangalia Nyumbu na wanya umepitwa na wakati, hebu nendeni Zanziber June July muone number ya wazungu.. Mazingira ustaarab wa watu ni Muhimu..kisiwa cha Mafia kina minwya ila miongoni mwa vivutio vikubwa Tanzania. Jina wangebadirisha na likawa ( Coconut Island) hili la Mafia linatisha kidogo.
 
Toa ushauri kwa Mamlaka mkuu jina zuri hilo ila kwenye Utalii wa wanyama ni zaidi ya utalii huo aisee..Tanzania kuanzia kule Nyerere Park,Mikumi,Ruaha Park huko Pangani mpaka Sumbawanga ni mbuga tupu za Wanyama ila Watanzania wapo hoi kama hawana hata mbuga moja aisee daah Nchi ngumu sana hiyo..
 
Kenya is a central of African foreign policy Kwa USA .... Yaaan mtoto pendwa wamarekani, na wa USA wakisha kukubali tuu nchi nyingine za western zinapita mule mule Kwa USA....ndio maana mashirikia mengi makubwa Yana makao makuu Kenya na si tz
 
Kenya ni ma snitch wa Africa. Wanatumika sana kuingilia mambo ya ndani ya nchi za Afrika. Kenya siyo watu wazuri kabisa. Base ya kijeshi ya Marekani iko kwao. So hawaamiki
 
Umepatia sana
 
Kenya is a central of African foreign policy Kwa USA .... Yaaan mtoto pendwa wamarekani, na wa USA wakisha kukubali tuu nchi nyingine za western zinapita mule mule Kwa USA....ndio maana mashirikia mengi makubwa Yana makao makuu Kenya na si tz
Na wakenya US wapo kama njugu
 
Tatizo ni zaidi ya ushuru. Ni historia inayoanzia tangu tujitange kuwa nchi ya kijamaa na kutaifisha mali za ''mabeberu''. Taratibu tukajikuta tunajitenga na nchi za Mgharibi ambazo ndiyo zenye idadi kubwa ya watalii. Tukashindwa kuwekeza kwenye huduma, vivutio na matangazo. Inajulikana wazi kuwa watalii hawaendi sehemu tu kwa sababu kuna vivutio. Huwa wanaangalia watalala wapi, wakipatwa na dharura kama ugonjwa watatibiwa wapi bila kusahau matangazo ya kuwavutia na pia urahisi wa kusafiri wakati wa kwenda na wakiwa kwenye utalii. Kenya wao waliendelea na siasa za soko huru, na wazungu wengi hawakubughudhiwa.
 
Na wakenya US wapo kama njugu
Sisi kwenda kutafuta maisha nje ni Jambo gumu saana, Kwa sababu still our resource as a country support us ardhi bado IPO na nafasi ya vibarua zipo

Wenzetu it's a big challenge tangu miaka ya mwanzo mwanzo huko, so the best option kwao ni kwenda nje kutafuta

Just like Nigerians
 
Exactly huu ni ukweli
Huwa nashangaa baadahi ya wazungu nawasiliana nao wengi wanaifahamu Kenya zaidi Kwa East Africa
 
Yes umeeleza vzr saana.

But still kwenye lile wazo lakufata ujamaaa lilikuwa sahihi,

Hao hao wakenya pamoja na kuwa na ubepari mapemaa but Wana maisha ya hivyo saana na magumu.

Watu masikini Kenya ni wengi, Teena masikini haswaa, with no land, yaan uchumi wakenya sio jumuishi, ni wachache wanamilik njia kuu za uchumi


Unlikely Tanzania, Ile ncome gap sio kubwa saana japo SASA hivi inakuwa Kwa Kasi ya ajabu
 
Mkuu hata mimi sikuwahi na sitakaa niseme kufuata ujamaa ilikuwa ni kosa japo nitasema tungeweza kufanya modification zaidi. Kwa mfano kubadilisha mfumo wa elimu bila matayarisho kulitu-cost sana. Nemebahitika kufika nchi za Scandinavia, mfumo wao hauna tofauti sana na kile alichotaka kufanya mwalimu Nyerere.
 
Ni kweli kabisaa.
 
Nipo Johannesburg bara bara kubwa ya kuelekea Oliver Tambo International Airport(Albertina Sesulu) maeneo ya Isando lipo Bango la Visit Zanzibar na wana ndege ambayo inapeleka wageni moja kwa moja Zanzibar airlink hapa kaburu wengi na wazungu wanaisimulia sana Zanzibar hii niliwahi kuona Water front kule Cape Town pamoja na Durban matangazo makubwa ya Zanzibar hata Spain pia ninachoshangaa upande wa Bara tumedumaa sana aisee ila safari za wakubwa ni nyingi hakuna kitu wanafanya kwenye Utalii..
 
halafu wakenya makauzu makauzu Sana yaani hata wanavyoongea kwa Ku shout tofauti na Sisi tuko calm kwenye negotiations
Hiki ndicho wanachowapendea Wakenya, wabongo sio makauzu hata kidogo
 
Haijawahi kutokea watalii wakaipenda nchi ambayo serikali yake ina miliki vikundi vya wafiraji vilivyoundwa kuwashughilikia wakosoaji
 
upande wa Bara tumedumaa sana aisee ila safari za wakubwa ni nyingi hakuna kitu wanafanya kwenye Utalii..
Si hii Chan2024 ninaona kale katangazo uchwara Unforgettable sijui nini au halifiki huko Spaine na Joburg linaishia hapo Kisemvule tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…